Rais Magufuli, ukitoa ushauri unatakaje tena taarifa?

Rais Magufuli, ukitoa ushauri unatakaje tena taarifa?

Nashangaa wanaomuelewa na kusifia haya anayofanya
Yoyote anaeiba Mali ya Umma lazima kuna siku moja hiyo Mali itarudi kwa Umma kwa njia yoyote ile,hata Magu akichota akae akijuwa kuna siku isiyokua na jina Mali hizo zitarudi kwa Umma kwa hiyo anachofanya Magu ni kurudisha Mali iliyokwapuliwa kutoka kwa Umma!!
 
eti anashauri alafu anataka mrejesho wa 'utekelezaji wa ushauri', na anatoa na 'dead line'. huyu mtu ana matatizo ya uelewa wa mambo kwa ujumla, ni mtu mwenye akili za wastani na hekima pungufu.
Kitu ambacho sikukielewa, mwenye uamuzi wa kusamehe kisheria ni DPP. Yeye alitoa tu ushauri. Unatoaje ushauri na kutoa deadline ya ushauri wako kufanyiwa kazi ? Kingine inakuwaje mtu mwenye mamlaka kisheria aende kuomba aongezewe siku 3 zaidi na mtu aliyetoa tu ushauri ?
 
Serikali ilishindwa kesi kwenye mahakama ya uwekezaji. Ndiyo maana ikazitoa. Kwani si ni serikali hiyohiyo iliyozuia fedha kwenye akaunti ya escrow? Mbona leo inatafuta kuwanyang' anya? Kwanini wasthibitishe uhalifu wao. Anaekiri kosa no yule aliyelifanya. Sio asiyelifanya. Hoja ya IPTL ilikuwa capacity charge kubwa. Na ilikuwa kimkataba. Ubabe tu.
Siyo kila mkataba ni mkataba maana mikataba miingine ni upigaji mtupu, huwezi kukaa kimya huku unapigwa eti kisa mkataba ,sometimes haki ndiyo kiwe kipaumbele chetu cha kwanza alafu mengine yafuatie!!
 
Ukiongelea kuhusu kuiba kipindi hicho wote walikuwa wezi hata unaemshabikia wewe ukifunuliwa yake yote utalia sana....mana hayasemwi kutokana na alipo ila asingekuwepo hapo ungeyajua yote
Basi kama nae alikua mwizi arobaini yake bado kwa Sasa acha tu deal na hawa ambao arobaini yao imeshafika!!
 
Wakati wabunge walipochachamaa hasa wapinzani wakati ule Bungeni kwenye issue ya ESCROW mpaka wengine wakaitwa matumbili huyo mtoa msamaha unakumbuka alikuwa wapi? Umesikia akipinga chochote?
Nazani alikua anausoma mchezo kabla ya kuingia mchezoni!!
 
MAFIA STYLE SHAKE DOWN

KWA MUJIBU WA SENETA ADAM SCHIFF WA MAREKANI.

Jiwe kuna pesa amelenga kuwakamua hawa watu. Na walengwa wala siyo hao 467, ni wengine kabisa anaotamani kupora akiba na rasilimali zao wazizotafuta kwa jasho na damu.

Jiwe anaitafutia ardhi ya Tanzania laana ambayo hatutapona kama nchi. Dhuluma huleta laama.
Prove it!!
 
Kupora watu pesa kwa staili ya kuwabambikia kesi za uhujumu uchumi ndiyo kutafuta pesa? Kwanini asisubiri mahakama zitoe hukumu? Kwani mahakama haiwezi kumhukumu mtu arudishe hizo pesa alizoiba kama ni kweli aliiba? Kwanini awalazimishe watu wakiri makosa ambayo hawajayatenda?

ACHENI UJINGA WA KUTETEA DHULUMA
Mahakama zenyewe kuna wapigaji kibao ,wwe unazani jiwe hajui hilo au wwe huzijui mahakama zetu kwa kupindua meza muda wowote!!?
 
Hivi hili tangazo linawahusu waliokutwa na hatia tayari? Ama wote tu wenye hizi kesi za uhujumu uchumi bila kujali upo katika hatua gani?

Mliopo kwenye tetesi pia mnaweza ungana hapo ilimsije kumbwa na kadhia hii baadae. Jitokezeni mkiri kuwa mmehujumu uchumi na sasa mpo tayar kurudisha fedha.
Hata kama ulikua mwalimu na ukala pesa ya madarasa ni busara tosha kurudisha kwa hiyari yako hapo shuleni msisubiri mpaka Raisi aseme,yoyote yule hata kama ulizipiga wakati uko jeshini kila mtu arudishe alipopiga kimyakimya!!
 
Ningekuwa mm sina cha kupoteza heri nifie jela kuliko kupoteza hela ya familia. Natoka kisha nakuwa masikini nimefilisiwa.
Ukitoka unaweza piga zaidi ya hizo anything is possible never say never!!
 
eti anashauri alafu anataka mrejesho wa 'utekelezaji wa ushauri', na anatoa na 'dead line'. huyu mtu ana matatizo ya uelewa wa mambo kwa ujumla, ni mtu mwenye akili za wastani na hekima pungufu.
Kama DPP angejua nafasi yake kikatiba hii nchi ingesonga mbele.

Huwa napenda kusema hii nchi haina haja ya kuwa na katiba mpya,tunahitaji watu makini tu wa kuongoza hizi taasisi. Kikatiba Ofisi ya DPP ni ofisi huru na hairuhusiwi kupokea maelekezo kutoka kwa mtu yeyote yule. Ni nini kinatokea leo hii?

Je,bado tunahitaji katiba mpya kama watu tulionao ni hawa hawa ambao wakipewa vyeo wanaona kama wametolewa jalalani na kuwekwa peponi?

Hiyo katiba mpya itatoa nini cha zaidi kama watu hawawezi kuufanyia kazi uhuru walionao kwenye katiba hii ya sasa ndio wataweza kuufanyia kazi uhuru watakaopewa na katiba hiyo mpya?

Katiba ya nchi inasema Ofisi ya DPP itakuwa huru na haitopokea maelekezo kutoka kwa mtu yeyote,leo maelekezo yanapokelewa hadharani kabisa bila aibu.

Bado tuna safari ndefu sana,tukomboe fikra zetu kwanza ndio tuhitaji katiba mpya,vinginevyo hata hiyo mpya ni kupoteza muda na pesa tu.
 
1.5 trillion yaani bilioni 1500 hela za escrow ni mara 4 na usheee
Ukiongelea kuhusu kuiba kipindi hicho wote walikuwa wezi hata unaemshabikia wewe ukifunuliwa yake yote utalia sana....mana hayasemwi kutokana na alipo ila asingekuwepo hapo ungeyajua yote
 
Ruge alivyokuwa anabeba pesa kwenye masandarusi kama mchele alisahau?

Wakati wanakula walikua wanashinda angani kwenda ulaya

Leo wanatafuta huruma kwa Wananchi waliowaibia?

Sisi tulishazoea shida wao wameguswa kidogo tu kelele
Hata wakifungwa matajiri wote umasikini wako uliosababishwa na CCM,utabaki palepale au kuongezeka maradufu
 
INAONEKANA Serikali inahitaji fedha, ndio sababu ya msingi kuongeza hizo siku 7. WAPO waliogoma kurejesha fedha. Kama watuhumiwa 467 wamejitokeza kurejesha bilioni 100 ni wazi wapo "MAPAPA" wamegoma kupiga magoti. Habinder Seth na Rugemalira pekee tuhuma zao ni 306bn. KAZI IPO!

Nimemsikiliza Rais akisema anaongeza siku nyingine 7 kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi kuomba radhi, kukiri kosa na kurejesha fedha, swali la msingi, mashtaka ya uhujumu uchumi, Rais anatajwa wapi katika sheria ya uhujumu uchumi kutoa msamaha kwa washitakiwa?

TAKUKURU wakamkamata Rugemalira, mahakama ya kuu, divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na rushwa ikamnyima dhamana kwa makosa ya uhujumu uchumi 350bn/- Mahakama ya rufaa ikagoma kutoa rufaa, Baadae RAIS anasema "kubali kosa, omba radhi, rejeshe fedha kuwa huru"

Maneno ya James Rugemalira 19.06.2019 mahakama ya rufaa

"kama ndivyo, naondoa rufaa. Sihitaji dhamana. Acha nibaki mahabusu hadi siku ya kusikilizwa shauri langu. Acha nibaki magereza, waache wanifunge kumaliza hili,natuhumiwa kuiba vitu ambavyo sijafanya. Naonewa bila kosa"
Baadae anakuja Rais anamueleza mtu huyu kwamba, akiri kosa, aombe radhi na alipe fedha hizo fedha anazotuhumiwa. UONEVU! DHULUMA! kukamata raia bila ushahidi, kubambikia mashtaka Baadae kuwataka walipe fedha ili waachiwe huru ni DHULUMA na UKATILI. Acheni kuwaonea watu.

Rais wangu nini tatizo.
Wito haujatolewa kwa ambao tuliiba na tumeishakula zimeisha na hatuna za kurejesha, tufanyeje?
 
wanateka nyara afu wanadai ransom.

Gangstaz republic, this.
 
Kitu ambacho sikukielewa, mwenye uamuzi wa kusamehe kisheria ni DPP. Yeye alitoa tu ushauri. Unatoaje ushauri na kutoa deadline ya ushauri wako kufanyiwa kazi ? Kingine inakuwaje mtu mwenye mamlaka kisheria aende kuomba aongezewe siku 3 zaidi na mtu aliyetoa tu ushauri ?
Mapichapicha
 
Back
Top Bottom