mr yamoto
JF-Expert Member
- Oct 2, 2016
- 923
- 1,393
INAONEKANA Serikali inahitaji fedha, ndio sababu ya msingi kuongeza hizo siku 7. WAPO waliogoma kurejesha fedha. Kama watuhumiwa 467 wamejitokeza kurejesha bilioni 100 ni wazi wapo "MAPAPA" wamegoma kupiga magoti. Habinder Seth na Rugemalira pekee tuhuma zao ni 306bn. KAZI IPO!
Nimemsikiliza Rais akisema anaongeza siku nyingine 7 kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi kuomba radhi, kukiri kosa na kurejesha fedha, swali la msingi, mashtaka ya uhujumu uchumi, Rais anatajwa wapi katika sheria ya uhujumu uchumi kutoa msamaha kwa washitakiwa?
TAKUKURU wakamkamata Rugemalira, mahakama ya kuu, divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na rushwa ikamnyima dhamana kwa makosa ya uhujumu uchumi 350bn/- Mahakama ya rufaa ikagoma kutoa rufaa, Baadae RAIS anasema "kubali kosa, omba radhi, rejeshe fedha kuwa huru"
Maneno ya James Rugemalira 19.06.2019 mahakama ya rufaa
"kama ndivyo, naondoa rufaa. Sihitaji dhamana. Acha nibaki mahabusu hadi siku ya kusikilizwa shauri langu. Acha nibaki magereza, waache wanifunge kumaliza hili,natuhumiwa kuiba vitu ambavyo sijafanya. Naonewa bila kosa"
Baadae anakuja Rais anamueleza mtu huyu kwamba, akiri kosa, aombe radhi na alipe fedha hizo fedha anazotuhumiwa. UONEVU! DHULUMA! kukamata raia bila ushahidi, kubambikia mashtaka Baadae kuwataka walipe fedha ili waachiwe huru ni DHULUMA na UKATILI. Acheni kuwaonea watu.
Rais wangu nini tatizo.