Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, ukishindwa uchaguzi uko tayari kukabidhi Ikulu?

Itategemeana na nani kashinda ,ikiwa Maganja au shibuda mbona anaachia kwa mbwembwe kabisa
Shida itakuja ukiwa lissu atashinda mzee jiwe atafikiri juu ya mayanga construction company ,25000 hekari ,Mauza uza ya Acacia sijui wasiojulikana ataamua bora waniulie kwa kiti
Kuua hapana ila mahakamani ndiyo mahala pake,atafute Haki yake na ikibidi akose dhamana kama Mh.Lema tuone kama atatoka salama huko!Mkuki kwa nguruwe...
Watanzania tukatae utawala wa kiimla,dalili zinaonyesha CCM wamejipanga kumfanya Jiwe Rais wa kudumu.Take A Note!
 
JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea
Suala ni kukubali matokeo ya kura iwapo atashindwa.Hayo mawazo ya Jua kukucha kutoka Magharibi,sijui mvua inyeshe kutokea ardhini ni sawa?Ushindi wa Magufuli ni Natural? Mbona tunafanya Uchaguzi kama matokeo tayari mnayo?
 
Ni rahisi kwa ngamia kupita tundu la sindano kuliko Magufuli kushindwa Urais
Hakuna cha ziada na hakuna kilichopungua.
 
Ushindi kwa Magufuli siyo ombi kutoka kwa vijana wa BAVICHA au BAWACHA , ushindi kwa Magufuli ni mpango ulioidhinishwa na mwenye mamalaka.
 
Mara zote huwa napenda kuwakumbusha wakati wa uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

CCM ilihamasisha sana watu wake tofauti na nyie mlikuwa mnawaambia wagomee, tena wengine walikuwa wanapost picha mitandaoni kwa furaha kabisa kwamba vituoni hakuna watu na hilo ndio litawagharimu, msitegemee kupata ushindi eti kutoka kwa wana CCM wanaomchukia JPM
Your nailed it clearly
 
Kawekwa Kati kulia nguvu ya umma, kushoto, Robert Amsterdam anafile kesi direct the Hague, kaskazini usa, ulaya, china na jumuia za kimataifa zinataka ngoma ipigwe sawa ili kuleta haki.Huku Askari tegemeo awaaminiki awajaongezewa mishahara 5 yrs wanaweza wasitii maagizo, Huku wakiweka uchaguzi huru hofu ya kutoboa ni ngumu,
Wana mtihani mzito sana
Huyo Robert Amsterdam hawezi kuwa na impact yoyote. Ongea mengine tu.
 
Ile Picha ilikua kwenye kujiandikisha kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambayo tayari chadema walikua wameisusia Ndo maana uliona Picha za kucheka vituo kua wazi ila kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura watu walijitokeza tena kulikua na foleni kubwa tu especially kwa mazingira ninayoishi mimi

Watu wengi waliojiandikisha si kwa lengo la kupiga kura, bali kupata kitambulisho. Lkn sasa watu hao wamebadili upepo, watatumia kitambulisho chao kufanya wanao jua wao.
 
Magufuli anapigwa chini, siku tatu kabla ya uchaguzi ndipo atajua hilo. Kwasasa tunamwacha asije tusumbua
 
Mkubwa, unauliza swali ambalo hatathubutu kulijibu..

Yaani kwa CCM na Magufuli fomular wanayoitumia iko hivi:

KUSHINDA + KUSHINDWA = KUSHINDA...!

Wamesema, hawana msamiati wa "KUSHINDWA KATIKA UCHAGUZI HUU WA 2020" katika kamusi yao..

Wameshasema hivi kwa kutumia vinywa vyao mwenyewe, kwamba;

"....Iwe Mungu muumba ANATAKA ama awe HATAKI, wao CCM na Magufuli wao ni LAZIMA WASHINDE uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 na kuunda serikali..."

Duuh, hii ni kufuru dhidi ya Mungu Yehova iliyovuka mipaka. Kwa kweli wanachokitafuta watakipata...!

Kwa maneno haya, huyu mtu ni KIBURI mwanzo mwisho. Hawezi kutoka ama kuachia madaraka ya Urais kilaini. Lazima atatolewa kwa AIBU na kwa LAZIMA kwa kutumia WINCHI huku akiwa amefungashwa kwenye ndege kuelekea The Hague..!
 
Itategemeana na nani kashinda ,ikiwa Maganja au shibuda mbona anaachia kwa mbwembwe kabisa
Shida itakuja ukiwa lissu atashinda mzee jiwe atafikiri juu ya mayanga construction company ,25000 hekari ,Mauza uza ya Acacia sijui wasiojulikana ataamua bora waniulie kwa kiti
Na huu muda unakuja around the corner ....
 
Shida inaa
JPM kushindwa u Rais , ni sawa na jua lianze kutoka magharibi kwenda mashariki, au mvua ianze kunyesha kutokea ardhini kwenda mawinguni au mwezi uanze kuangaza mchana na jua usiku.

Epukeni kujipa matumaini hewa ambayo hapo baadae yatawaacha na simanzi kubwa huku mioyo imejaa machozi kwa kutokuamini kile kilichotokea
Shida inaanzia hapa mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi.
 
Tuna taasisi dhaifu sana ambazo hazina ubavu wa kumfuata Ikulu sitting president na kumuamuru aondoke Ikulu

NEC yenyewe kabla ya kutangaza matokeo bila shaka wataomba ruhusa kutoka TISS. Doomed!
 
Back
Top Bottom