Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

Rais Magufuli, Punguza confrontation na Wazungu

Kwenye US dollar yao wameandika we trust in god kumbe kirefu chake ni we trust in Gold Oil Diamond. Ngoja tuone
 
Sina katiba hapa but kinasomeka hivi; "Tanzania ni nchi ya ujamaa na kujitegemea...." Tena pages za mwanzoni kabisa.

Kumbe ni nchi, si watu wake.

Mimi siyo mjamaa (kwa maana ya mkomunisti) lakini ni mjamaa kwa maana kuna jamii inayonizunguka na nna uhusiano nayo mzuri sana na pia ni Mtanzania nnaejitegemea.
 
Wewe mleta mada ni hambwe ambaye huna hata robo ya UZALENDO.
Inawezekana ukamuona hivyo, lkn kumbuka kwamba wazungu ukishikilia mali zao kijinga jinga wanakuondoa, kama sio kukuwekea vikwazo vya kiuchumi. Aachane nao kabisa. Cha kufanya afanye revision ya mikataba ili tufaidike wote, dio kufanya unyang'anyi
 
Mleta post upo sahihi baadhi ya sehemu ni kweli hawa wazungu si watu wa kwenda nao hovyo watakumaliza huchukui round mkuu anatakiwa aplay very smart
 
MkamaP

Kuhusu la madini, kuna kitu kinasumbua sana akili za wengi

Hivi Magufuli si amekuwepo serikalini miaka 20, tena akiingia katika cabinet!

Ina maana hakujua hili kweli na kama alijua alifanya nini wakati huo?

Tusianze kuwalaumu 'wamagharibi' tujiulize kwanza role yetu kwa haya kutokea

Tunalaumu shoka, hatujiulizi kama linaweza kukata bila mpini!
 
Nguruvi3
Mkuu maswali yako ni mazuri. Na hata hivyo nafikiri kwa Rais afrika ana nguvu nyingi sana, mawaziri naamini hua ni kama polisi tu anapiga salute hata kama hakubaliani na jambo husika. Hii huwezi laumu sana mtu alipokuwa waziri kwa sababu ni desturi na mazingira wenda na hali halisi ndo inapelekea kuwa vile. Hili si kwa chama CCM tu na upinzani kiongozi wa chama akisema tutoke bungeni hata kama una mawazo tofauti lazima utoke tu nje.

Sasa cha mantiki zaidi hapa ni kuwa, kwa kuwa ameshakua Rais na inaonekana inamuumiza kweli kweli na maamuzi ya nyuma, hii utaona anaongelea jambo hili la madini hata kabla hajachukua fomu ya urais ktk video fulani iliyoko mtandaoni. Na kwa vile ameshaunda kamati ya kuchunguza hayo madini, basi ni vyema apate majibu sahihi kiasi cha dhahabu kilichomo na alimalize suala hili ktk meza ya mduara. Meza ya mduara ndo mwamuzi mzuri na sahihi kabisa ktk hali tuliyopo.
 
Mkuu, hoja yangu ni kuwa hata kama hakuwa na uwezo wa kukataa, kupinga au kutoa maoni, lipo jambo moja alililokuwa na ufahamu nalo i.e kuna tatizo katika sekta ya madini, mchanga una utata na mikataba haieleweki

Hili linashadidiwa na hotuba yake Ikulu akiongea na wafanyabiasha aliposema tunaweza kuwa 'furnace' na tunajua degree ya separations ya minerals.

Hivyo, alifahamu uwepo wa tatizo.
Moja, alitakiwa afanyie kazi baada ya kupata mamlaka
Mbili, kusubiri hadi aende kukamata makontena kunatia shaka, a year after!
Tatu, alitakiwa aunde kamati mapema sana kupata majibu kabla ya haya kutokea

Kwasasa hivi kazi inayofanyika ni ya zimamoto! kamati ifanye kazi chini ya mwezi mmoja
Ina maana ni suala la dharura!uwepo wake katika cabinet kwa miaka 20 ulikuwa na benefit gani?

Nauliza haya kwasababu kuna utamaduni wa kucheza mduara halafu tunajifariji tunasonga mbele
Suala la umeme, tuliambiwa tutauza nje, yaani ziada.
Kuna gesi na stigler zote zilikuwa katika pipeline
Katika hali ya kushangaza tunaagiza kutoka Ethiiopia kana kwamba ni jambo geni kabisa

Tunawezaje kusonga mbele ikiwa hatufanyi review and appraisal ya projects zetu?
 
MkamaP kuna jambo nikuulize. Je, ulishawahi kuona mikataba ya madini?

Mikataba ya Tanzania ni siri(classified doc), sijawahi kuiona. Ila nafikiri mimi hatuwezi endelea kwa kutegemea maliasili bila kuwa na plan B yenye tija zaidi.

Madini yanakuwa na tija kama ukichimba tuseme cobalt ukatengeneza, smart phone mwenyewe ama ukachimba helium ukatengeneza bomu ama grid ya umeme mwenyewe.
 
Huu uzi mkubwa una mambo mengi lkn hujagusia sheria

Anachokifanya JPM je anafuata sheria na mkataba unasemaje?

Umeshaambiwa mchanga wa dhababu utakosaje dhahabu?

Mi naona zaidi huu uzi umeficha udhaifu wa utendaji wa jpm na unamkweza kwa sifa za kijinga c ni yale yale ya kunyosha nchi bila kufuata katiba
 
Mkuu, sheria hatujui inasema je kwa sababu hatujui kilichomo kwenye mikataba hiyo. Sie hapa tunajadili mstakabali wa Tanzania, sidhani kama tupo hapa kuangalia mapugufu ya mtu ama uhodari wake, hayo hayatatusaidia sana ktk kulisukuma gurudumu la Tanzania. Mie nafikiri tuangalie ktk ule muono wa big picture ya kwamba kwa vile mikataba walishaingia na Rais kaunda tume basi majibu watayopata wakae kwa meza ya mduara wayamalize mezani kama cha kurekebisha kimo wakubaliane mezani.
 
"The most potent weapon of the oppressor is the mind of the oppressed"...Steven Biko. Mtu anayeamini kwamba wazungu hawawezekaniki tayari ni mtumwaa wa fikra
 
Mikataba ya Tanzania ni siri(classified doc), sijawahi kuiona. Ila nafikiri mimi hatuwezi endelea kwa kutegemea maliasili bila kuwa na plan B yenye tija zaidi.

Madini yanakuwa na tija kama ukichimba tuseme cobalt ukatengeneza, smart phone mwenyewe ama ukachimba helium ukatengeneza bomu ama grid ya umeme mwenyewe.
Well said, na hapa ndipo point yangu ilipo, kwamba, hatufanyi mambo 'well defined'

Leo inaundwaje kamati ya kuchunguza mchanga ikiwa tumefanya hivyo kwa miaka 10!
Je, tulikuwa na sera ya madini? Na je tulivuna vipi hayo madini wakati kamati ikiwa haipo?

Yote yanakuja katika suala moja, mikataba imekuwa siri na hatujui ilifanyikaje na kwanini
Kuunda kamati ni 'pain killer' baada ya muda suala la mchanga litapita kutakuja tatizo jingine

Je, tunajua tunamilikisha vipi maeneo?
Wasipopeleka mchanga wakapeleka dhahabu kwa madege tutaunda kamati ya kufuatilia airport?
 
"The most potent weapon of the oppressor is the mind of the oppressed"...Steven Biko. Mtu anayeamini kwamba wazungu hawawezekaniki tayari ni mtumwaa wa fikra

Hatusemi kwamba mzungu hawezekaniki ni potentials tu alichonacho, nafikir acheni hating syndrome. Wewe kama ni mwananchi wa kawaida nenda mbele ya rais wako um confront kwa lolote uone naongea nini. kwa kutambua nguvu alizonazo rais wako na uka avoid confrontation naye haina maana wewe ni mtumwa wa fikra za rais. Come on dude, please give me a break.
 
Well said, na hapa ndipo point yangu ilipo, kwamba, hatufanyi mambo 'well defined'

Leo inaundwaje kamati ya kuchunguza mchanga ikiwa tumefanya hivyo kwa miaka 10!
Je, tulikuwa na sera ya madini? Na je tulivuna vipi hayo madini wakati kamati ikiwa haipo?

Yote yanakuja katika suala moja, mikataba imekuwa siri na hatujui ilifanyikaje na kwanini
Kuunda kamati ni 'pain killer' baada ya muda suala la mchanga litapita kutakuja tatizo jingine

Je, tunajua tunamilikisha vipi maeneo?
Wasipopeleka mchanga wakapeleka dhahabu kwa madege tutaunda kamati ya kufuatilia airport?

Ndiyo hapo hapo nafikiri approach yetu bado haijakaa sawa sawa, ni ngumu sana ku simulate scenarios as per regard. Ni kitu very complicated, ndiyo maana mie naona chochote kitakachokuwa basi wamalize kwenye meza ya mduara. Na kama akitaka labda kwa baadae mikataba inayofuata iwe inawekwa public. Unajua ukiweka tempalate ya mkaba bungeni waka debate kuna sehemu tu watakuonesha matobo hata kama bunge halina makali.
 
Ndiyo hapo hapo nafikiri approach yetu bado haijakaa sawa sawa, ni ngumu sana ku stimulate scenarios as per regard. Ni kitu very complicated, ndiyo maana mie naona chochote kitakachokuwa basi wamalize kwenye meza ya mduara. Na kama akitaka labda kwa baadae mikataba inayofuata iwe inawekwa public. Unajua ukiweka tempalate ya mkaba bungeni waka debate kuna sehemu tu watakuonesha matobo hata kama bunge halina makali.
Ni bora kwasababu wanaoandika mikataba hiyo ya siri wana interest zao
Mtu anaaahidiwa dola milioni 1 kwa kuondoa kipengele, kwa wtz inawezekana

Unakumbuka ile kesi ya Bank ambapo majaji walituhumiwa kupewa milioni 40?
Wakawemo viongozi wa dini wamekatiwa?

Inapokuwa siri kama ule mkataba uliondikwa na Karmaggg kule kwa mama ntilie London unategemea kitu gani hapo

Ikiwekwa wazi hata wasomi mmoja anaweza kuona tobo mahali pakazibwa mapema
Kwasasa tunafanya kazi kwa kutumia 'kamati' ndiyo maana sioni kama ni suluhisho

Halafu walikuwepo, waliyona miaka nenda rudi, leo wanatufanya tuamini ni geni kabisa
 
Mh Rais Magufuli, ktk mambo mengi upo sahihi na kama ni makosa basi ni ya kibinadamu. Ila nafikiri kuna kitu ambacho wenda hujakipatia sawa sawa ama bado hujapata habari kwa usahihi wake.

Mosi, lazima tukubaliane na ukweli kabisa kwamba kutokana na mazingira halisi ya ulaya hawawezi kuishi kwa amani wasiponyonya kwa nguvu nchi za afrika na Karebean na uarabuni. Na hivyo, hakuna fair trade ktk vitu ambavyo wanavyovihitaji kuendesha maisha yao na kizazi chao, na ya kwamba ni lazima wachukue vitu kwa bure ama bei inayokaribia na hapo.

Cha mhimu kujiuliza je tuna nguvu za kuwasimamisha kivita ama ktk ku control financial system? Sasa tukipata majibu inabidi kuchukua tahadhari sahihi hasa tunapo deal na yalipo masilahi yao. Siyo kwamba naandika haya kwa sababu tunawaogopa ila hali halisi yenyewe inanisukuma kuandika haya. Wazungu wao wanasema "wako radhi kufanya kazi na shetani palipo na masilahi yao".

IMF, UN, World bank, mahakama za dunia na vyombo vya habari ni mali za wazungu. Na wazungu ni wamoja sana kupita kipimo. Hivyo ukizuia mali za wazungu, tuseme dhahabu, umezuia mali ya IMF ama World bank.Na hivyo hawa (IMF, World bank, UN, court zote)hawatakuja kufurahia hata kidogo, watakufanyia hujuma na kukwamisha karibu ktk kila kitu.

Maoni yangu, we have to know our place. Ya kwamba tu deal na mafisadi wetu, hawa mafisadi wa dunia jaribu ku negotiate nao objectively na wakati huohuo tukiangalia maeneo mengine yatoyotunyanyua ktk maendeleo. Kukwaruzana nao hasa ktk madini, wanaweza turudisha ktk nyakati za ujima. Hawa jamaa kwa hujuma wame qualify kwa kiwango cha juu sana.

Ushauri, kaa nao mezani mkubaliane nao amicably the way forward. Hiyo kamati uliounda hata wakikuta dhahabu wazungu wanaiba, na imejaa kwenye macontena, naamini kwenye vyombo vyao hawataandika wala kuonesha kwamba wazungu wanaiba africa. Wao watachokifanya ni ku potray wewe, wao wanavyotaka uonekane ktk jamii ya dunia. Again, chochote kamati uliyoiunda itakachokuta kwenye makontena kaa nao ukubaliane kwa mazungumzo mezani.
Magu hajui analofanya, hajui kuna kitu kinaitwa ukoloni mambo leo.Vile vile haelewi kua taasisi za kifedha za dunia kama IMF,WORLD BANK, CENTRAL BANK OF AMERIKA nk ni taasisi binafsi.Hajui kua kwa nini Saadam Hussein,Hugo Chaves , Muammar Ghaddaf nk walitolewa madarakani bila kupendwa.Hajui kama matajiri wa ulaya na marekani ndio wanaoshikilia dunia, wanakontrol marais na kila kitu,Anafikiri yeye na Bashite wanaweza kudhibiti wazungu!
 
Ni bora kwasababu wanaoandika mikataba hiyo ya siri wana interest zao
Mtu anaaahidiwa dola milioni 1 kwa kuondoa kipengele, kwa wtz inawezekana

Unakumbuka ile kesi ya Bank ambapo majaji walituhumiwa kupewa milioni 40?
Wakawemo viongozi wa dini wamekatiwa?

Inapokuwa siri kama ule mkataba uliondikwa na Karmaggg kule kwa mama ntilie London unategemea kitu gani hapo

Ikiwekwa wazi hata wasomi mmoja anaweza kuona tobo mahali pakazibwa mapema
Kwasasa tunafanya kazi kwa kutumia 'kamati' ndiyo maana sioni kama ni suluhisho

Halafu walikuwepo, waliyona miaka nenda rudi, leo wanatufanya tuamini ni geni kabisa

Nakubaliana na wewe sana, pia pa kuanzia hapo if any, from now on, mikataba iwe inapelekwa bungeni na inapitishwa na bunge na kurekebishwa kidogo. Maana hii tuliyokwisha ingia tumeshaingia tu negotiate tu mezani otherwise, itakuwa kama kumtuma mbwa akamkamate chui.
 
Back
Top Bottom