Uchaguzi 2020 Rais Magufuli ndiyo anaibuka kuwa atawaongezea mishahara wafanyakazi. Tunamwambia kuwa hatudanganyiki ng'oo

Mzee meko hafai hata ukatibu kata! Hatutaki kuongozwa kama mifugo!
Hahaaaaaa............

Tunasubiria tu tukiwa na vichinjia vyetu mifukoni, ili ikifika tarehe 28, tukamilishe kazi ya kumrejesha Jiwe kijijini kwake Chato
 
Ndugu yangu kumbuka sheria ni msumeno inakata mbele na nyuma. Ukiwa mfanyakazi unalindwa na sheria sawa lakini ni lazima pia mfanyakazi ati sheria za kazi. Mfano uwajibikaji, kutokupokea rushwa, vyeti feki, wizi hizi zote zinamuondolea kinga. Nchi kabla Magufuri hajaingia madarakani wenyenchi yao ambao ni wapiga kura walikuwa na malalamiko Kila kona yanayohusu rushwa, kuzalauliwa na hao watumishi wa uma. Kucheleweshewa kwa makusudi kwajili ya urasim. Kwakifupi walikuwa watumishi wengi wezembe walirudisha nyuma uchumi wa nchi wakati huohuo wao wanaendelea kudai maslai haki. Au umejisaulisha ndugu yangu, nasema uongo ndugu yangu. Ilikuwa imefika wakati ukitaka kumuandikisha mtoto darasa la kwanza mwalimu anakuomba pesa la sivyo atakwambia nafasi zimejaa. Sasa jemedali wetu mtetezi wawanyonge JPM ameingia kaweka mambo sawa tunampa mitano mingine ili kazi iendelee.
Mimi sina haki ya kumchagulia mtu nani wa kumchagua haki yako. Kuhusu wafanyakazi kama ulivyosema sheria msumeno basi wenye haki wapewe na wenye makosa wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria hilo sipingi. Ila kwenye haki zao isiwe kama anafanya hisani ni kama akiwachukulia hatua isiwe kama yeye ni mbaya ni sheria tu. Rushwa mpaka leo kama ipo tukienda mimi na wewe kuomba passport tu siku moja mimi nikatoa pesa ya soda wewe usitoe basi mimi nitapa katika siku 4 wewe utasubiri mwezi, haya mambo yapo mpaka leo na passport nimetolea mfano tu. Hii kauli ya kumuita rais wa wanyonge inapotosha sana, na wasiokuwa wanyonge nani rais wao? mnyonge ni nani? unyonge ni pale hujui haki zako na unaenda kuomba ukijuwa haki zako huna haja ya kuwa mnyonge sasa viongozi wanafanya watu wote wanyonge waombe hata nyongeza japo ni haki yao.
 
mbona alikuwa hasemi!! ilani yenu imejaa miundombinu!!
Haa😂😁😀😅😄😄😄😄
Hakusema Siku Zote Leo Ndiyo Anasema
Mbona Hakwenda Kuyasema Haya Pemba, Mtwara, Lindi Ruvuma, Katavi, Rukwa
Ameshikwa Pabaya
 
We mfanyabiashara wa nchi gani au Ubelgiji? Unajambo gani hali yakuwa mimi mfanyabiashara wa hapa bongo mi5 kwa JPM kazi iendelee.
16/10/2020 joined

Utakuwa mpwa wa Meko uliyesahaulika mchinjilie mbali uyo Meko Hana faida ata kwenye ukoo

Shetani Hana rafiki
 
Wewe unachosema siyo campaign ya Mbeligiji? Achana na mambo ya kizushi
Teh teh teh.....kwanini umehitimisha ni kampeni ya Lissu na sio Lipumba? wapi nimemtaja Lissu?

Hizi ID za kampeni zimeibuka nyingi sana kweli..'kisu kimegusa mfupa' teh teh teh 🤣🤣
 
Haa
Hakusema Siku Zote Leo Ndiyo Anasema
Mbona Hakwenda Kuyasema Haya Pemba, Mtwara, Lindi Ruvuma, Katavi, Rukwa
Ameshikwa Pabaya
Washamba hawa! mwaka huu lazima watoke!! nahivi tambiko lao hilikutupumbaza Kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka yote!!
 
Washamba hawa! mwaka huu lazima watoke!! nahivi tambiko lao hilikutupumbaza Kama ambavyo wamekuwa wakifanya miaka yote!!
Wamejisahau, kwa kuwa tambiko lao la kila mwaka la kutukimbizia Mwenge wao wa kutumbulaza nchi nzima, hawajaukimbiza mwaka huu..........

Hawa jamaa wang'oke tu mwaka huu
 
Wewe acha unafiki unafikiri hutoba ya Jana alisoma akiwa chumbani kwako tu. JPM amejipambanua kwakusema ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Aidha jana ametoa sababu za wazi kabisa kwamba alikuwa amaimarisha uchumi akimanisha ukusanyaji wa kodi, kuziba mianya ya rushwa, wafanyakazi hewa, kuzibiti mafisadi, kuongeza nidhamu na uwajibikaji kazini. Sasa ameona mambo yapo kwenye right truck, uchumi umekua nidhani kazini na uwajibikaji umekua sasa mishahara itapanda kwa speed ya kimbunga. Sisi wananchi wajasilia mali tumemuelewa Sana. Tunajua miaka mitano tulikotoka hapa tulipo na tunako elekea. Usishi kwa mazoea utafilisika ndugu amka. #JPM mi5 tena kazi iendelee
Hili la mishahara hata mngeteteaje, ni cancer ambayo inaendelea kuwatafuna, mnajua maisha ya watumishi? Ila hamuwezi jua hasa nyie mlio kua karibu na keki ya taifa that's mkisikia neno jpm kupingwa chini mnachanganyikiwa,
Sawa alikua kwenye kukuza uchumi, na kulazimisha watu kufunga mikanda vipi yeye binfsi katika kipindi hichi alifunga mkanda na je kukuza uchumi ni Vita? Na je ni waziri ,au makatibu wakuu,wakurugenzi, n.k wamefunga mikanda tofauti na watumishi wa chini? Why wafaidi watu wachache alhali wote wanashiriki katika ujenzi wa taifa.
Achen kutetea Mambo haya
 
Nilimsikia Rais Magufuli, katika mkutano wake wa kampeni hapo Jana, huko Bagamoyo mkoani Pwani, akiwaahidi wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara yao wafanyakazi hao, iwapo watamchagua tena katika uchaguzi mkuu ujao!

Hivi si ndiyo huyu huyu Rais Magufuli amekuwa akigoma katakata kuongeza mishahara ya wafanyakazi, kila amapoonbwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutokana na kupanda kwa hali ya maisha kwa wafanyakazi hao, katika kila sherehe za Mei Mosi, kila mwaka tokea aiingie madarakani mwaka 2015, akidai kuwa hawezi kuongeza mishahara wafanyakazi, kwa kuwa katika kipindi hiki anajenga miundo mbinu mikubwa ya reli ya SGR na bwawa la umeme la Stieglers Gorge?

Wakati Rais Magufuli amekuwa akigoma katakata kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa sababu hizo zisizokuwa na mashiko hata kidogo, marais wenzake wote waliomtangulia walikuwa wakiwaongeza mishahara yao wafanyakazi, pamoja na marais hao pia walikuwa wakiendelea kujenga miundo mbalimbali hapa nchini

Hivi Rais Magufuli kutoa ahadi hiyo wakati huu wa kampeni, anatugeuza sisi wafanyakazi wa nchi hii ni wajinga mno na tunaoweza kudanganyika kirahisi hivyo?

Sisi wafanyakazi wa nchi hii, hatudanganyiki tena na Rais Magufuli na tuna jambo letu ambalo tutalitimiza ifikapo Oktoba 28 mwaka huu kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Sema wewe. Mimi na wafanyakazi wenzangu ninaowafahamu na tulio wengi tutampa kura yetu maana tunajua kinachofanyika katika nchi yetu. Hatupo kwa wakati huu kwa ajili ya matumbo yetu tu. Tunatambua maendeleo yaliyopo sasa ikilinganishwa ni awamu zilizopita zilizokuwa zinarundikia mapato ya taifa kwa manufaa ya matumbo yao tu.
 
Aache unafiki watumishi lazima tuchinjeee...alisema mei mosi ataongeza kabla ya kutoka madarakani sasa anakuja na ulaghai mwongomwongo
Huyu Mzee ni msahaulifu kupita kiasi,katika kampeni hizi hizi za uchaguzi mkuu aliwahi kusema mishahara haiwezi kuongezwa wakati nchi inapigana vita ya uchumi.Najiuliza aliposema nitaongeza mishahara kabla ya mwisho wa utawala wake alimaanisha mwaka gani?Anapangilia atakayoyafanya baada ya uchaguzi ambao haukuwa umefanyika(Beyond 2020 General Elections),ameshachaguliwa?
 
Hizo longolongo za CCM bara na tararira za CCM Zanzibar ndio zile zile za mwaka 2015,hivi CCM hawana kumbukumbu za kujua walichokizungumza kwenye uchaguzi wa 2015 ,wanarudi na ahadi zilezile ambazo zimewafanya waonekane waongo, sasa askari gani utamwambia nitakuzidishia mshahara.mwalimu gani ,mjeshi yupi,CCM msidanganye huu sio wakati wa kudanganyana kwa kuzirudia ahadi zenu ambazo ni ahadi hewa.

Kubalini mambo ya ishe upepo huu sio wa kurudi na kutudanganya kwa ahadi hewa angalau mnekuja na mengine mepya,hatupigi kura kuchagua chama au mtu tunapiga kura kuwaondoa waongo na waongo tulionao kwa sasa ni CCM.
 
Nilimsikia Rais Magufuli, katika mkutano wake wa kampeni hapo Jana, huko Bagamoyo mkoani Pwani, akiwaahidi wafanyakazi kuwa atawaongeza mishahara yao wafanyakazi hao, iwapo watamchagua tena katika uchaguzi mkuu ujao!

Hivi si ndiyo huyu huyu Rais Magufuli amekuwa akigoma katakata kuongeza mishahara ya wafanyakazi, kila amapoonbwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kutokana na kupanda kwa hali ya maisha kwa wafanyakazi hao, katika kila sherehe za Mei Mosi, kila mwaka tokea aiingie madarakani mwaka 2015, akidai kuwa hawezi kuongeza mishahara wafanyakazi, kwa kuwa katika kipindi hiki anajenga miundo mbinu mikubwa ya reli ya SGR na bwawa la umeme la Stieglers Gorge?

Wakati Rais Magufuli amekuwa akigoma katakata kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa sababu hizo zisizokuwa na mashiko hata kidogo, marais wenzake wote waliomtangulia walikuwa wakiwaongeza mishahara yao wafanyakazi, pamoja na marais hao pia walikuwa wakiendelea kujenga miundo mbalimbali hapa nchini

Hivi Rais Magufuli kutoa ahadi hiyo wakati huu wa kampeni, anatugeuza sisi wafanyakazi wa nchi hii ni wajinga mno na tunaoweza kudanganyika kirahisi hivyo?

Sisi wafanyakazi wa nchi hii, hatudanganyiki tena na Rais Magufuli na tuna jambo letu ambalo tutalitimiza ifikapo Oktoba 28 mwaka huu kwenye sanduku la kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Spana za Lissu na watanzania kwa ujumla zimemwingia vizuri. Hata hivyo kauli zake za sasa hazitamsaidia kitu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom