Rais Magufuli: Ndege ndio heshima ya nchi

Rais Magufuli: Ndege ndio heshima ya nchi

Hapa nilichoka kabisa ...Ndege ndio heshima ya nchi ?

Aliye elewa anisaidie mimi bado nalitafakari hili

Natamani ningezaliwa usukumani labda ndio ningemuelewa

Kesho utasikia Mkolomije mmoja anasema manguo yao ya Kung'aa na marangi rangi ndio heshima ya Wasukuma
Mku nimelewa hivi ni muhimu ionekane angani kuonyesha ile ni ndege ya watanzania haijalishi unajiendesha kwa faida au hasara
 
Mkuu hapana. Hata hizi zetu zinahitajika. Tena kama unaisimamia vizuri ina faida nyingi sana. Tusiangalie tu kwenye shirika kuleta faida. Tuangalie kwenye usafirishaji wa mizigo, dawa na vitu muhimu ndani ya nchi na kwa haraka.
Tusiangalie hasara tu.

Zina faida nyingi kama alivyotaja mkuu hapa juu.
Wanasiasa wakati wa kampeni,viongozi wa dini,hata taasisi za wanafunzi wa vyuo vikuu watazifaidi sana.
 
Basic needs zenyewe ni issue halafu eti ndege ni heshima ya nchi
Kweli mkuu, huwa napata aibu sana nikipata wageni kutoka nje wanapoona:-
1. Jinsi dar kulivyo na shida ya maji safi
2. Usafiri wa jiji usivyokuwa wa kistaarabu, abiria kuminyana na kurundikwa kama si binadamu.
 
Sema siku nyingine muangalie wanasheria waadilifu wa kuwatuma kwenye kesi za kimataifa, hao akina Chenge kazi yao ilikuwa kuuza mechi tu na kulitia hasara taifa, ona sasa hasara tunayopata kwenye hiyo ndege
 
Heshima ya nchi ni ndege wakati zinaingiza hasara ya bilioni 223.1 ndani ya miaka miwili tu!?
Woooooyooooo!!! 😱😱😱
Zimeingizaje hiyo hasara aisee.., hebu tupe habari kamili basi
 
Heshima ya nchi kwanza kabisa ni UTAWALA BORA unaozingatia haki na sheria (katiba) ambazo wananchi wote wamekubaliana ziwaongeze. Hayo mengine yanafuata baadaye. Hata ukinunua ndege mpya mia moja lakini huku unakandamiza haki za msingi za binadamu, hiyo heshima ya nchi utakuwa unaiona wewe kichwani mwako tu - inakuwa ya KUFIKIRIKA!
 
Rais Magufuli: Tanzania tulikuwa hatuna ndege. Ndege ndio heshima ya nchi!!


> Tumeingia madarakani nikasema lazima tuwe na ndege. Wakasema pesa atapata wapi? Nikasema pesa ziko kwa Mafisadi na watazitema hata ikibidi kwa kutapika

ngoja kwanze nilale,punde nitarejea[emoji41][emoji41][emoji41]
Tatizo la huyu bwana ni mvivu wa kufikiri na kujifunza kama ndege ni heshima ya Nchi ajiulize hizi Pangaboi zilizotangulia kwa nini zimesababisha hasara ya mabilioni? Hivi anafahamu huwa zinaenda hata mwanza na abiria 20? Hivi heshima ya Nchi ni kupata hasara? Huyu bwana lazima ana hitilafu kichwani
 
Rais Magufuli: Tanzania tulikuwa hatuna ndege. Ndege ndio heshima ya nchi!!


> Tumeingia madarakani nikasema lazima tuwe na ndege. Wakasema pesa atapata wapi? Nikasema pesa ziko kwa Mafisadi na watazitema hata ikibidi kwa kutapika

ngoja kwanze nilale,punde nitarejea[emoji41][emoji41][emoji41]
tupo kutafuta heshima zaidi.

wananchi wanyonge subirini kwanza hadi heshima ijae pipa!!
 
Usishangae tu, eleza umuhim wake ili wajifunze toka kwako
Mkuu unajua/umewahi kusikia nchi inayoitwa Ethiopia yenye shirika la ndege liitwalo Ethiopian? Unajua ni nchi maskini sana na wananchi wake hawana uwezo wa kupanda ndege lakini shirika linawasaidia sana uchumi wa nchi kwa faida linalopata? Kama wao wameweza kwanini sisi tusiamini tunaweza?
 
Mkuu tulishaimba sana hili. Ndio maana kuna madili maana serikali ndio mfanyabiashara mkuu na mwenye kutunga miongozo na sheria.
Tanzania tusahau maendeleo katika hilo. Hebu angalia umeme,maji vyote ni serikali. Hata usafiri?
Maji akiachiwa kampuni binafsi aendeshe utaweza kulipa bill?? Au utalia lia tena na serikali!
 
Inatengeneza hasara nayo ni heshima ya nchi

Ova
 
Back
Top Bottom