Rais Magufuli: Ndege ndio heshima ya nchi

Rais Magufuli: Ndege ndio heshima ya nchi

Hizi panya ndio za kutapikia maneno yale! Nchi imekula hasara hii
 
Vizazi vijavyo vitamkumbuka kwa haya anayoyafanya.
Wakati wa kujenga lazima maumivu yatokee.
 
Sasa kama hizo ndege zina faida na zinasaidia sana uchumi wake, hiyo nchi inaendeleaje kuwa masikini sana!? Au ni mimi sielewi? Mbona tunaona vijana wa kiethiopia kila siku wakikamatwa hapa nchini wakiwa njiani kwenda SA kutafuta maisha? Hebu leteni utetezi utakaoingia akilini jamani kwani na sisi ni watu wazima wenzenu.
Mkuu usiache nicheke. Unategemea uchumi wa nchi uendeshwe kwa ndege tu? Haiwezekani. Mimi nimesema (na eewe mwenyewe umesema kwa maneno) kuwa ''zinasaidia sana uchumi wa nchi''. Kusaidia siyo Kutosheleza! Hata sisi Bongo utalii unasaidia sana uchumi wetu lakini hauondowi shida zenu! Misaada ya nchi wahisani inasaidia sana sana uchumi wetu lakini haitoshelezi! Tuache kujitoa ufahamu kwa vitu ambavyo viko wazi!
 
Lkn sio Mapanga boy.
Ushamba wa kabila fulani saiv umekuwa ushamba wa Taifa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Embu punguza siasa. Kaaome website ya bombardier kuhusu specification ya hii ndege alaf ndio uje uite mbovu.
America wanazo,brazili wanazo,rwanda wanatumia, kenya airways wanazo,ethiopia airways wanazo.
Kama ni mpya hazina shida, shida ni kama ni mitumba kama hizi zetu zinavyohisiwa kuwa.
 
IMG_20180403_150047_0.jpeg
 
Kuna watu wabishi humu jf hadi raha kufuatilia comment zao
 
Kuna ndege kweli zinaleta heshima kwa nchi.lakini hizi panga boi?mzee asituone wajinga.tena asiongee huo --------tena.
 
vinchi kama vya kwetu reli sawa, siyo ndege. Zilzopo zinatema hasara tupu. Aviation industry ni ngumu sana kwa vinchi kama vyetu
Mkuu hata kwa nchi za ulaya na Amerika biashara hii haimilikiwi na Serikali kwa asilia mia kuanzia KLM, Air France, Brussel Air n.k. Wamebaki waarabu tu na wanatoa ruzuku kwelikweli. Kwa serikali zetu si biashara ya kutegemea kukuza uchumi wa nchi hata siku moja. Nchi hii 75% ya watu ni wahemeaji tu, kitakacholeta maendeleo (economic development) ni kilimo. Tatizo wanasiasa wa nchi zetu wanatudanganya na takwimu (Economic growth).
 
Mkuu hapana. Hata hizi zetu zinahitajika. Tena kama unaisimamia vizuri ina faida nyingi sana. Tusiangalie tu kwenye shirika kuleta faida. Tuangalie kwenye usafirishaji wa mizigo, dawa na vitu muhimu ndani ya nchi na kwa haraka.
Mkuu hii biashara haina faida kubwa kama hiyo hasa kwa nchi kama zetu. Kenya airways (KQ) pamoja na kutawala soko la East Afrika ikiwa peke yake bado walichemsha walikuja kuokolewa wakielekea kuzama, huku Air France-KLM wakinunua hisa 26%. Tena inakuwa ngumu zaidi unaponunua ndege kwa cash mpaka ziki break even si leo. Narudia serikali iwekeze seriously kwenye kilimo hakika kitawasaidia waTZ wengi sana.
 
..yeye mwenyewe hana hulka ya kupanda ndege..anafanyaje promotion?...BTW...hii mentality yake ya heshima kuja kwa kuwepo ndege ni ya kishamba sana....ndio maana yuko radhi kununua ndege moja kwa gharama ya ndege tatu...tena akitamba kwa cash money...hizi mentality ni ya kishamba sanaa....haionyeshi mtu mwenye logic kwenye maamuzi...hata kama anashauriwa vibaya...Hana logical thinking....
 
Back
Top Bottom