Rais Magufuli: Ndege ndio heshima ya nchi

Rais Magufuli: Ndege ndio heshima ya nchi

Hapa nilichoka kabisa ...Ndege ndio heshima ya nchi ?

Aliye elewa anisaidie mimi bado nalitafakari hili

Natamani ningezaliwa usukumani labda ndio ningemuelewa

Kesho utasikia Mkolomije mmoja anasema manguo yao ya Kung'aa na marangi rangi ndio heshima ya Wasukuma
Hahahah
 
Heshima ya nchi ni ndege wakati zinaingiza hasara ya bilioni 223.1 ndani ya miaka miwili tu!?
Woooooyooooo!!! 😱😱😱
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
vinchi kama vya kwetu reli sawa, siyo ndege. Zilzopo zinatema hasara tupu. Aviation industry ni ngumu sana kwa vinchi kama vyetu
Unataka wote tuwe tunatumia basi hata kama tunaharaka.
 
Hahahahhhhhhhhh nacheka kihutu ajisemea Mange
Ndege ndio heshima ya nchi how?????
Mzee hayo ni mascrapper umeuziwa zitakuwa juu ya mawe
Ungejaribu kupata ushauri kwa nchi jirani ambao ndege zao zinaenda Europe, America etc
 
eg...

Kenya

[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Kuendesha mashirika ya ndege kisiasa ni chanzo kikubwa sana cha mashirika hayo kushindwa kujiendesha kwa faida na kufa.

Heshima ya nchi haijengwi kwa kuwa na ndege zenye thamani, inajengwa kwa kuthamini utu.

Utu na vipaumbele vya kutuingizia Pesa yab uhakika. Tumejiuliza kwanini viwanda vilikufa?
je ATC ya enzi ya Nyerere ilikuwaje?, TRC ya enzi ya Nyerere ilikuwaje?
Je hatukuingia ubia na South African Airways ? Nini kilitokea?.

Ni kipi tumebadili sasa na kwamba tunaweza kuendesha AirTanzania Kibishara? .
 
Sikiliza dhalimu heshima ya nchi inakuja pale aliyekabidhiwa kuongoza nchi hiyo anauheshimu utawala wa sheria, anaheshimu katiba ya nchi, anaheshimu Bunge, mahakama, sheria na taratibu zote za nchi. Anaheshimu vyombo vya habari, vyama vyote vya siasa, si mbaguzi, anaheshimu haki ya raia na uhuru wao kujadili na kukosoa mambo mbali mbali ndani ya nchi yao. Hivi ndiyo namna ambavyo nchi inajipatia heshima yake na si ndege kama unavyotaka kutuaminisha Watanzania ndege ambazo Watanzania watakaozipanda hawafiki hata 10% ya Watanzania wote na huku zikiliingizia Taifa hasara kubwa sana.

Rais Magufuli: Tanzania tulikuwa hatuna ndege. Ndege ndio heshima ya nchi![emoji38][emoji38][emoji38]

> Tumeingia madarakani nikasema lazima tuwe na ndege. Wakasema pesa atapata wapi? Nikasema pesa ziko kwa Mafisadi na watazitema hata ikibidi kwa kutapika

ngoja kwanze nilale,punde nitarejea[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Hapa nilichoka kabisa ...Ndege ndio heshima ya nchi ?

Aliye elewa anisaidie mimi bado nalitafakari hili

Natamani ningezaliwa usukumani labda ndio ningemuelewa

Kesho utasikia Mkolomije mmoja anasema manguo yao ya Kung'aa na marangi rangi ndio heshima ya Wasukuma

Hivi huwa mnashirikisha akili kabla ya kukomenti?
 
Kuendesha mashirika ya ndege kisiasa ni chanzo kikubwa sana cha mashirika hayo kushindwa kujiendesha kwa faida na kufa.

Heshima ya nchi haijengwi kwa kuwa na ndege zenye thamani, inajengwa kwa kuthamini utu.
Kiranga naona kauli hii imekutoa chimbo
 
Kiranga naona kauli hii imekutoa chimbo
Hapana, mbona nipo kitambo tu, ila upuuzi hautakiwi kuachiwa uendelee bila kukemewa.

Nilikuwa namsikiliza CEO mmoja wa Ethiopian Airlines anahojiwa na BBC. Kipindi fulani cha Business.

Akaulizwa, shirika la ndege la Ethiopia limekuwa na mafanikio sana, kitu ambacho hakikutegemewa sana kwa nchi ya Afrika, nini siri ya mafanikio yenu?

Akataja vitu kadhaa, lakini akasema, kikubwa kabisa, ni jinsi serikali yetu ilivyotuachia tujiendeshe kibiashara bila ya kuingilia maamuzi ya kibiashara na bila kutaka siasa iongoze shirika letu.

Hilo lilikuwa ni jambo kubwa sana katika kufanikisha Ethiopian Airlines ifanikiwe.

Huko kwetu tunaona shirika la ndege lilivyoendeshwa kisiasa na kupata hasara miaka mingi, na mpaka sasa rais anaingilia habari za shirika la ndege na kuliongoza kisiasa.

Kwa nini tunafikiri tutaepuka shirikakuendeshwa kwa hasara?
 
Back
Top Bottom