Rais Magufuli, namuombea msamaha Paul Makonda. Msamehe

Rais Magufuli, namuombea msamaha Paul Makonda. Msamehe

Mocumentary

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
857
Reaction score
2,241
Mhe Rais wetu, na viongozi wote wa serikali yako, sisi kama vijana tunayemtazama. Paul Makonda kama chachu ya uongozi katika mioyo ya vijana, tunakuja mbele yako kwa unyeyekevu mkubwa kuomba msamaha wa yale yote aliyoyafanya kinyume na matakwa yako na serikali yako kwa ujumla.

Tunaamini yapo mapungufu mengi aliyonayo na yapo makosa mengi aliyoyafanya hata ambayo sisi tunaweza tusijue, ila tunakujua wewe Mh. Rais kama Baba mwenye upendo, mwenye huruma, kipenzi cha vijana wa taifa hili, mwenye moyo wa kusamehesaba mara sabini maana tumekushuhudia ukitusamehe vijana wa taifa hili. Tunakuomba sana baba msamehe Makonda mpe nafasi nyingine itakayokupendeza ili aendelee kuwatumikia watanzania.

Tunaamini bado anayo akili, utashi, ujasiri na upendo kwa nchi yake. Bado ana vitu vingi sana vya kuwafanyia wanyonge wa nchi hii. Bado tunaamini anayo nguvu ya kuendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo kwa 2020-2025 imesheheni mipango mingi na mizuri sana kwa kijana wa nchi hii.

Baba msamehe Makonda mpe nafasi katika serikali yako.Tunakuahidi kukupigia kura nyingi za kishindo, zitakazoonyesha shukrani yetu kwa kazi uliyoifanya kwa nchi hii.Kwa yeyote anayeweza kumfikia Mh. Rais, tunakuomba umwambie tunampenda, tunamuomba amsamehe Makonda, yatima, wajane, maskini, wanyonge na vijana wanchi hii tunamkumbuka na kumuombea msamaha.

Lakini pia tunamuomba Askofu Gwajima amsamehe na kumuondolea laana aliyoitamka madhabahuni kwake ya kumfuta katika siasa za nchi hii juu yake. Bado ni kijana mdogo anayehitaji kusamehewa na kufundishwa. Taifa hili bado linahitaji mchango wake.Mungu awabariki sana.Kwa niaba ya tunaomkumbuka Makonda.


domitiandomitian@gmail.com.
IMG_20200902_142104.jpg
IMG_20200902_142107.jpg



NOTE: MLETA MAADA HANA MASLAHI WALA HUUSIANO NA UJUMBE HUSIKA, HIVYO HASIUSISHWE MOJA KWA MOJA NA MADA, YEYE NI MLETA TAARIFA TUU.
 
Watu wengine wanakaririswa sana mi huyu jamaa binafsi sina chuki nae najua ni mchapa kazi labda ilikua ni mihemuko tu ya kuwatumikia wananchi binafsi naungana na ww muheshimiwa amsamehe tuu tunamuhitaji Mimi siwezi kumchukia mtu kwa mihemuko ya watu wachache kwanza kwa lipi Mie cjawah hata kukutana na makonda wala hajawah kuniumiza kwa namna yyt ile hakuna mkuu wa mkoa yyt wa dar alie mfikia makonda kwa kuchapa kazi
 
Ujumbe utakuwa umefikia mhusika Ila Sasa akaanze kilimo au biashara au ufungaji ili aweze kujikimu kimaisha. Ajira sio lazima awe mtumishi wa umma. Pia ataweza kuchangia taifa kwa kulipa Kodi .
 
Kafanya kosa gani kwani? Kuna adhabu gani aliyopewa kwani kwa hilo kosa?

Makonda hafai katika uongozi hapa nchini na kama Magufuli atamrudisha katika nafasi nyingine tena hapa itadhihilika kuwa kuna waganga wanaomdanganya kuwa hawezi kutawala bila Kuwa na Makonda!!

Amefanya mambo mengi ambayo yamemdhalilisha Jiwe likiwemo la kutaka kuingiza makontena kinyemela na kuwalazimisha wafanya biashara kumpa fedha kwa nguvu kwa kutumia cheo chake! In short Makonda is a criminal who should be shied away. Hizo mbinu za kuomba uteuzi kwa kutumia media ni za kitoto ambazo mtu yoyote mwenye busara hawezi kuzitumia.
 
KIKAO GANI KILIKUTUMA UKAOMBE MSAMAHA KWA NIABA YA MAKONDA? TANZANIA KUNA VIJANA WENGI WANAOWEZA KUFANYA MAKUBWA KWA TAIFA HILI. MH MAGUFULI ANAFANYA VIZURI SANA KULIKO WALIOMTANGULIA KWA SABABU AMEPEWA NAFASI. KAMA MAKONDA KASHINDWA KUTII KATAZO LA RAISI WETU WOTE, HAFAI HAFAI HAFAI.
 
Makonda njoo tujiajiri fursa ni nyingi huku mitaani kama ulivyokua unatwambia ukiwa ofisini!!
1) kilimo cha mbogamboga kitakufa
2)ufugaji wa kuku na bata na kanga na kware ni biashara mzuri sana acha kutegemea ajira za serikali
3) wewe ni mkristo tena mkatoliki ufugaji knguruwe unalipa sana karibu ndugu
4)kuna biashara ndogo ndogo ,wenzio tumehitimu vyuo vikuu mwaka wa tano sasa hatuna ajira njoo tuuze mkaa uswahilini unalipa sana
5)najua wewe deep freeza hukosi njoo tuuuze maji baridi huu ni msimu wa kiangazi mkuu!!
Fursa ni nyingi sana tunaomba uje uwe chachu achana na ajira serikali ina mambo ya msingi ya kufanya Rais amefanya mengi sana usimsumbue njoo tujiajiri bwana
Pia nimekuona ukihubiri injili zama huko huko mkuu sadaka hazina kodi
Pambana aisee nimeona umepata mapacha njoo ndugu hela ya pampasi uipatie huku kama sisi uliokua unatwambia tujiajiri tuache uzembe
Mwisho kabisa nakutakia kazi njema na pole sana kwa kutimuliwa pale jamhuri dodoma inaonekana wale maafisa kipenyo hawajui kua wewe ni NGOSHA????
 
"Yule mchato" aliamua kumuweka benchi ili akiguswa "yeye" asinuke... avundie huko huko bench
 
Mhe Rais wetu, na viongozi wote wa serikali yako, sisi kama vijana tunayemtazama Paul Makonda kama chachu ya uongozi katika mioyo ya vijana, tunakuja mbele yako. kwa unyeyekevu mkubwa kuomba msamaha wa yale yote aliyoyafanya kinyume na matakwa yako na serikali yako kwa ujumla...
Mkuu nenda kajiajiri, naamini mtaji unao wa kutosha
 
Back
Top Bottom