Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,762
- 26,051
Now now now now, ndugu yangu Phillipo.
Taratibu. Tatatibu. Taratibu.
Sarcasm prevents revolutions. Sisi wengine hatupendi kuchinjana, kwa hiyo tukiona kitu hakitufai tuna haki ya kuwa sarcastic. Its a small price to pay for bad leadership.
Tatizo kubwa ni kwamba you have too much respect for authority. That is dangerous. Hiyo ni sababu moja kwa nini hatuendelei.
Turudi kwa Magufuli na marufuku yake.
Tatizo linalojitokeza hapo ni kuhukumu kosa ambalo hata halijatokea.
Ni kama uende Manzese kwa Mfuga Mbwa halafu uwakamate watoto wote uwafunge jela kwa kusema nyie mkikua kidogo ntakuwa Panya Road na kutuletea matatizo, kwa hiyo bira tuwafungikie mbali ili msije kutuletea matatizo baadaye.
Mimi Magufuli na serikali yake wangewaadabisha wapinzani wanaosema ovyo - wapo wapinzani kama hao- on a case by case basis, baada ya kusema ovyo, with hard evidence and justification kwamba wamesema ovyo, hata nisingekuwa na tatizo.
Kwa sasa ameqeka mtego wa panya unaokamata waliokusudiwa na wasiokusudiwa.
Hata mtu mwenye heshima zake anayetaka kufanya mikutano ya vyama vya upinzani ya kukosoa serikali kwa njia sahihi na ambayo inalindwa ma katiba ya nchi yetu, hawezi kufanya hivyo.
Magufuli kaziba uhuru huu.
Kama si udikteta huu ni nini?
JPM speech is the catalyst for this debate- supposedly.
Mkuu Kiranga, tatizo ni kwamba mimi wewe na wana JF wengi tulipiga sana kelele hapa juu ya serikali ya awamu ya nne kuhusu yale yaliyokuwa yakifanywa pamoja na ufisadi.
Sasa kaja raisi ambae anatekeleza mengi ya yale tuliyokuwa tukiyapigia kelele, halafu wanajitokeza watu walewale walokuwa wakimpigia kelele JK sasa wanambeza raisi JPM, ni jambo la aibu sana na tunaonekana ni wajinga.
Na yeye kama binadamu hata ungekuwa ni wewe unapata shock kwanza na baadae inabidi aweke sera na mipaka ili aweze kudhibiti hiyo tabia maana si tu watu wanakosoa bali wanakebehi, kutukana na kurudisha nyuma jitihada zake na wanaonekana wazi wanafanya hivyo kwa makusudi.
Kwahiyo sisi observers wengine tunaweza kusema kwamba upinzani kwa sasa hauna cha kusema kuhusu yale ambayo yote yako covered na raisi JPM na wanapoanza kwenda mitandaoni ama kubeza kwenye majukwaa yao au kuhisi wanafanya sarcasm or caricature inakuwa wanaoenekana wana ajenda ingine.
Mimi niliwaheshimu sana wapinzani kabla ya kumkaribisha Edward Lowasa lakini nilikuwa mfuatiliaji wa itikadi ya Dr Slaa.
Mlipomkaribisha Lowasa kwenye UKAWA ndipo mlipoharibu kila kitu maana sasa anawatuma watu (allegedly) wamchafue raisi JPM ama mitandaoni au kwenye media.
Maana ya neno Catalyst:
A substance that increases the rate of a chemical reaction without itself undergoing any permanent chemical change.
President Magufuli was talking about cementing the relationship between Kenya and Tanzania and by doing so this relationship would emphasise on building strong bilateral and economic ties and this relationship is the catalyst.
Tukirudi kwenye hiyo clip kuna watu wamebeza takwimu zake za uchumi na sasa inaletwa hii ya neno Catalyst.
CCM wenyewe wanaweza kufananishwa na kazi ya Catalyst kwamba mabadiliko yote ya mpaka kumfanya Lowasa aondoke mle wao bado wamempata raisi ambae ndiye bora na wao wanadunda hata kwa kuugulia khasa wale walotia nia mapema asubuhi.
Wakuu sasa tuanze kusifia yale mazuri anayofanya raisi JPM na kama unafanya utani ieleweke ni utani kwa kutoa angalizo maana bila hivyo mtu unaonekana unakejeli na kubeza.