Rais Magufuli mwombe Radhi Kikwete

Rais Magufuli mwombe Radhi Kikwete

Kufanya tathmini ya mhe.Jakaya na Raisi wa sasa kwa kipindi hiki naona ni mapema sana.
Sawa nakubali tathmini ya muda mfupi lakini kumbukeni ni awamu yake ya kwanza nayeye anafalsafa zake za kiutawala hivyo lazima mabiliko makubwa kama haya tuyashuhudie.
Nadhani akimalixa awamu yake hii ya miaka mitano hapo tutaweza kutoa tathmini ya ujumla.
 
Je hiyo mikopo iliyokopwa na jk alilipwa kwa wenye nayo?
Mkuu hata kikwete ana mapungufu yake na kwenye hilo aliteleza kwa sababu walikuwa hawarudishi mikopo.

Sasa hivi watu wanarudisha mikopo kwenye huu utawala wa JPM je kurudi huko kunaleta unafuu gani katika maisha ya mtanzania?
 
Wakati jpm akiingia madarakani alisema kuwa nchi ilikuwa imeoza kila sehemu akasema kuwa viongozi wabovu waliopita ndio wametufikisha hapa tulipo

Mzee wangJk hahakuwahiukutufikishawenye hali hii tutuliyopoasa
~Hali ya ukosefu wa ajira
~wanafunzi kukosa mikopo
~Pesa haipatikani
~wafanyakazi hawapandishwi madaraja
~Serikali kutoajiri mwaka na nusu sasa
~Biashara na viwanda vinakufa

Jpm mzee wangu chonde chonde mwombe samahani jk kwa kumsingizia kuwa yeye ndio aliotufikisha hapa

Wewe ndie uliyetufikisha hapa kwa mda mfupi tu.


Kwani mambo hayo hapo juu ndio yanamfanya JK asiwe kiongozi mbovu?
 
...Hizi siasa tu! yeye alikuwa sehemu ya Serikali iliyopita: Kwenye wizara zake ndo kulikuwa na madudu kuliko ...
Wakati jpm akiingia madarakani alisema kuwa nchi ilikuwa imeoza kila sehemu akasema kuwa viongozi wabovu waliopita ndio wametufikisha hapa tulipo

Mzee wangJk hahakuwahiukutufikishawenye hali hii tutuliyopoasa
~Hali ya ukosefu wa ajira
~wanafunzi kukosa mikopo
~Pesa haipatikani
~wafanyakazi hawapandishwi madaraja
~Serikali kutoajiri mwaka na nusu sasa
~Biashara na viwanda vinakufa

Jpm mzee wangu chonde chonde mwombe samahani jk kwa kumsingizia kuwa yeye ndio aliotufikisha hapa

Wewe ndie uliyetufikisha hapa kwa mda mfupi tu.
 
Watetea mafisadi chadema, mjue kabisa Magufuli siyo saizi yenu..

Kulialia kwenu kwenye mitandao ya kijamii hakuwezi kubadili jiwe kuwa barafu.

Chadema, chama la hovyo kuwahi kutokea duniani
 
dalili zinaonyesha sio kwamba yatatokea, yameshatokea. au hali halisi haujaiona, upo nje ya nchi nini? na kwa upande wangu, kwani sasaivi nimehamia nchi gani na hali hii ngumu? si nipo hapahapa bongo? tunachoombea Mungu tu 2020 ifike haraka ili tufanye maamuzi ya mubadala kwa amani tu.
Kwani 2015 ulifanya maamuzi gani na 2020 utafanya maamuzi gani?
 
kuna tofauti kubwa sana kati ya hawa watu wawili, mmoja dikteta mwingine mwana demokrasia, watu hawa hawalinganishwi kwa mambo mengi, na mwafaa alilijua hili mapema akazuia uhuru wa habari, akavibana vyombo vya habari, mihimiri ya bunge, mahakama na vyombo vya haki vikabinywa, akazuia uhuru wa kujieleza, akazuia kukosolewa na akataka asifiwe tu(udikteta). Jk alikua mvumilivu sana aliruhusu watu kujieleza, vyombo vya habari vilikuawa huru, haki za binadamu walikuwa huru, kwa upande mwingine tuliona mkwere kaharibu sana kwakua aliruhusu uhuru huu, hatukuwahi kuona akifunga watu kwa kumkosoa,aliitwa mpaka dhaifu ila kwa ukomavu wa kisiasa alikaa kimya, nakumbuka kauli yake siku moja alisema"jamani unajua raisi ana mamlaka makubwa sana, nikiamua nimwambie mwema kamata hao kina lissu atawakamata" ukimlinganisha na mwafaa...hana uvumilivu kabisa angeruhusu uhuru huo mpaka leo angekua kwenye hari ngumu sana, upepo wa Lowassa asingeuweza kabisa, ... sasa hivi ukiangalia nchi inavyoendeshwa ni one man show...vyombo vya habari haviko huru tena vimebaki kusifia tu...habari ni magufuli atumbua, mkuu wa wilaya aweka mtu rumande..hata ikitokea upinzani wakaitisha press conference tv na magazeti hawatairusha kama ilivo, watakata kata habari wanayodhani itamuudhi mwafaa haitarushwa,mifano tumeiona maiti za watu saba,kupotea Ben,maafa kagera, vyobo vya habari havikutoa uzito kabisa na vilivyoandika ni jujuu tu ili wasimuudhi mwafaa, juzi nilimusikia mama wa haki za binadamu akilalamika wakiomba tv kufanya vipindi vya kuikosoa serikali tv zinakataa... watu wakikosoa wanafungwa na mbaya zaidi hakuna utawala wa sheria tena dhamana mpaka mwafaa atoe ruhusa, tumeona mifano mbunge anakamatwa na katikati ya kesi alipotaka kupewa dhamana hakimu akapigiwa simu na baada ya simu ile maamuzi ya hakimu yalibadilika...baada ya hapo tunayaona yanayoendelea...sehemu pekee iliyokuwa imebaki kuikosoa serikali ni mitandao ya kijamii ..na yenyewe tunaona kina Melo wanayofanyiwa, kwa ufupi tumegeuka taifa la watu waoga, mawaziri waoga, wabunge waoga, wakurugenzi waoga, wanachi waoga, anaogopwa mwafaa, wataalam wetu wamekua waoga hawatumii tena taaluma zao, mtu mmoja ndo mtafiti,Dr,mchumi,hakimu,etc... mwafaa akasema jk we mvumilivu mimi siwezi kuvumilia...raisi hana uvumilivu wa kukosolewa mmmh.. Mungu apishe mbali tusizinguane na nchi yoyote atatupeleka vitani huyu
 
Urais ni taasisi!
Zaidi ya 90% ya watendaji na mawaziri wa JK ndio wale wale wa JPM na wote wanaitikia tune ile ile kwa vicheko!
Nawahurumia mnaoendelea kuamini kuwa JK alikuwa bora kana kwamba mlisimuliwa bila kumuona wenyewe. Pia mnasahau kuwa JPM ni ccm naye na keshahakikisha 'ulinzi' wa waliotengeneza majipu ...subiri kidogo, more recent wanasema kesi za mahakama ya ufisadi hazipo na lugumi haina kosa lolote ililofanya wala kanuni iliyokiukwa!
 
Hata hivyo naye alikuwa ni sehemu ya uoza huo kwani kama anavyosema yeye mwenyewe amekuwa serikalini kwa miaka 20 hivyo hawezi kujitenga na uovu anaousema.
Hapo sasa ......... miaka 20 alikuwa anangalia tu mambo yanavyokwenda kombo bila kusema kitu!!

Ina maana asingepata Urais 2015 bado angendelea kuangalia tu mambo yaendelee kuharibika mpaka hapo atakapopata nafasi ya kurekebisha!!?
 
Hamna lokote...Kikwete alifanya yake kwa kadiri uwezo wake na alivyoshauriwa watu waliishi kwa uhuru ktk nchi yao leo watu kimya kimya mateso bila chuki.
 
Hapo sasa ......... miaka 20 alikuwa anangalia tu mambo yanavyokwenda kombo bila kusema kitu!!

Ina maana asingepata Urais 2015 bado angendelea kuangalia tu mambo yaendelee kuharibika mpaka hapo atakapopata nafasi ya kurekebisha!!?
Jamani mulishaambiwa na wanaowajua Magufuli na Kikwete ni Kusi na kasi, munawalinganishaje?
 
Nilimdharau alipoamua kusema makaburi ya zamani hachimbuliwi hatoweza kuyafukia.. Na atawalinda wahalifu waliomuweka,wengine anawatumbua tu wakati wowote. Tokea siku hiyo nikamuona ni mtumishi Wa shetan am sure Mungu kesha mlaani.
 
2020 kuna mtu anaweza kuja kushindwa kujieleza amefanya nini miaka 5. ameumiza mioyo ya watz vya kutosha huyu mtu.
 
Nilimdharau alipoamua kusema makaburi ya zamani hachimbuliwi hatoweza kuyafukia.. Na atawalinda wahalifu waliomuweka,wengine anawatumbua tu wakati wowote. Tokea siku hiyo nikamuona ni mtumishi Wa shetan am sure Mungu kesha mlaani.
tatizo ni ujeuri. kiburi ni kitu kibaya sana, Nebukadreza wa Babeli alishushwa chini na Mungu hadi akala manyasi kama ng'ombe kwasababu ya ujeiru. wewe ukijiona mjeuri kamfanyie mkeo na familia yako, sio kila mtu unayemwona hapa nchini unaweza kumfanyia ujeuri, na kama mazoezi ya ukatili kamfanyie mkeo na watoto wako. ndio tatizo la watz.
 
unakumbuka mwaka juzi shule zlifungwa kwa kukosa chakula? unakumbuka migomo ya wanafunzi katika vyuo vya udom na udsm....hata wakati wa JK....tulipata shida saaaaaaaana ya mkopo
Lakini mwisho tukapata sasa hapa mwisho watu wamekosa
 
Back
Top Bottom