Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala

Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
292
500
Habari zenu mabibi na mababu!

Kwanza kabisa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kila mtu anapoambiwa au kusikia kuongezewa muda wa kutawala Rais magufuli anashikwa na ghadhabu na kutamani ata kumpiga mtu ngumi kutokana na ugumu wa maisha uliopo.

Sio watumishi wa Serikali, sio wafanyabiashara, machinga, wastaafu, wanachuo, wahitimu wa chuo, mama ntilie, wachuuzi, n.k wote hawa hawataki kusikia ata kidogo msamiati wa Rais magufuli kuongezewa muda wa kutawala, wamemchoka vibaya mnoo kiasi kwamba mpaka wanajuta kwanini walimpa uraisi na bila kupepesa macho wanatamani ata kesho tu Amalize muda wake wa kutawala waangalie ustaarabu wa raisi ajae.

Na wale wanaoshupalia kuwa aongezewe ni wabunge ambao wapo bungeni wakiona hawana cha kupoteza kwamba akitawala milele basi wao wakijipendekeza watakuwa kwenye maisha salama, lakini viongozi ambao wamemwagwa hawapo ata bungeni ukiwafata uwaambie JPM aongezewe Muda usipokuwa makini wanaweza kukupiga makofi mfano mfate lugola alafu mwambie JPM tumpe milele bhana kama hatokutukana, kwahyo wale wanaoshupalia ni wale ambao wananufaika nae tu ila mzee baba hakuna anaempenda watu washamchoka.

^^^^^^^^^^
Mambo ambayo akiyafanya Rais magufuli Watanzania wenyewe bila kushurutishwa watamlilia na kuandamana barabarani kuomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala ata milele.

1. Kuongeza nyongeza ya mishahara na kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma. (hawa watu wametaabika na wana hali mbaya sana kwa muda wa miaka 6 sasa mpka barabarani wanajiongelesha wenyewe kwa stress, Magu akitaka apate mapambio ya kuongezewa muda wa kutawala basi hawa watu awapandishe mishahara kwa asilimia kubwa % na kuwalipa madeni yao wataongoza kumsifu na kumshinikiza).

2. Kuajiri vijana waliopo mtaani. (siku hizi wahitimu wa vyuo wamejaa mtaani kama njugu vile hawana kazi yoyote ile, sio walimu, sio manesi, madokta, bwana mifugo n.k, hili kundi ni kubwa mnoo na linaongoza kumchukia magufuli vibaya mno adi kutamani Mungu angempenda zaidi mana mtaani wanataabika hatari, vijana hawa hawana ata familia lakini wanaongoza kuwa na msongo wa mawazo).

3. Wastaafu kulipwa pesheni zao. (hapa wazee wengi wanasononeka na kushikwa na hasira mtu amemaliza kutumikia taifa lakini haki yake mwenyewe anazungushwa mpaka anakata tamaa, mzee kastaafu ila ana miaka mitano bado hajapewa pesa zake hayo mapenz yakutaka rais aongezewe muda wa kutawala atayatolea wapi!! Hawa ni wengi mnoo wengine mpaka wanakufa wamekosa stahiki zao.)

4. Wafanyabiashara kupunguziwa kodi za hovyo zinazowapekea kufunga biashara zao.

5. Wakulima wa korosho kulipwa pesa zao. (hawa watu sio tu kuwa wana hasira na huyu bali wana kisasi kikali san na ukitaka kujua machungu yao uwakute wanaongea kikabila, kiasi kwamba wanamuombea majaliwa angalau aje kuwa Raisi ili apunguze machungu ya watu wake wa kusini.)

6. Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kupunguziwa riba.

7. Wakulima kutafutiwa masoko ya uhakika na kupunguziwa gharama za pembejeo.

8. Kuzuia mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali. Mf. Mafuta, sukar, cement.

9. Mikopo himilivu kwa vijana na wanawake.

10. Bima bora za afya kwa Watanzania.

11. Kuhamasisha Matajiri duniani kuwekeza viwanda mbalimbali Tanzania.

Mh Raisi akiyafanya hayo bila chuki wala roho mbaya Watanzania wenyewe wataamua na kumshinikiza kwa maandamano atawale ata milele hadi afie ikulu.

~Gai da Seboga
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,034
2,000
Hakuna mwekezaji atakuja kwa sera zake za kukurupuka ...analowaza ndio sheria nani atapoteza muda kuja huku ? Hawezi kuongeza mishahara hana wigo mzuri kodi wengi wanafunga biashara....wakandarasi wanadai sana SGR ni wimbo tu markez wanafanya kwa speed ndogo sana ....hela hakuna Bwawa kule amelipa 1.25 T kati ya 7 T ....
 
Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
4,991
2,000
Hayo ni hewa.

Tunataka katiba mpya.

Na hata km akiitimiza madaraka hatoongezwa mtu hapa hii nchi sio ya Mugabe.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
6,692
2,000
Habari zenu mabibi na mababu!

Kwanza kabisa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kila mtu anapoambiwa au kusikia kuongezewa muda wa kutawala Rais magufuli anashikwa na ghadhabu na kutamani ata kumpiga mtu ngumi kutokana na ugumu wa maisha uliopo...
Alishindwa kujenga ukuta hivyo hawezi kamwe kuja kujenga ukuta. Binafsi hata anipandishe daraja mara 20! Bado haitakuja itokee nikamkubali.

Muda wake ukiisha aondoke zake. Wengi tumemchoka kupitiliza.
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
4,215

Vipi kuacha kuwapiga risasi wakosoaji? Kuacha kubambika kesi za uhujumu uchumi kwa watu asiowapenda?
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,343
2,000
Habari zenu mabibi na mababu!

Kwanza kabisa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kila mtu anapoambiwa au kusikia kuongezewa muda wa kutawala Rais magufuli anashikwa na ghadhabu na kutamani ata kumpiga mtu ngumi kutokana na ugumu wa maisha uliopo...
Shallow thinking! Ukomo wa miaka kumi haukuwekwa kwa sababu za kijinga kama unavyodhani. Ukomo upo ili kuondoa loophole ya marais wenye tamaa no matter how good their perfoming! Ukisema huyu amefanya vizuri aongezewe muda kipindi kijacho atakuja fashisti na ukifika wakati wa kuondoka atadai na yeye amefanya vizuri sana hivyo anastahili kufia madarakani. Tuheshimu utaratibu wa miaka kumi kwani watanzania wenye uwezo wa kuongoza wako wengi sana.
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,376
2,000
Hakuna binadamu mmoja anaweza kufanya hayo...., Ni misingi ya nchi inayofuatwa ndio inaweza kuhakikisha hayo yanafanyika (System na sio Mtu)

Na kwa mtu ambaye hafuati system na anaweza kuamka na kubadilisha system hayo kamwe hayatafanyika.

ifike wakati nchi iendeshwe kwa misingi ya nini tunataka kufanya na wapi tunataka kwenda, kiongozi anayekuja ni kusimamia ile misingi na kufuata ni nini kinatakiwa kufanyika (hata kama akiwa robot ) sababu ni misingi kila mtu atakuwa anajua tunataka kufanya nini kama taifa na sio fulani anataka tufanye nini (na nini kifanyike kinakuwa kimeshapangwa long term) ; huwezi kutegemea mipango ya muda mrefu ifanywe na mtu ambaye anakaa muda mfupi..., atakachofanya ni vitu short term....
 
EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
5,525
2,000
Kuzingatia katiba ni jambo la msingi kuliko huo utopolo kufanya hayo kwa watanzania ni jukumu lake na kuteketeza katiba inasema nini ni jambo lingine.Watanzania sio wajinga,tumeelewana ndugu zangu
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
733
1,000
hayo mambo yote uliyoyataja yatakuja,na usifikiri yakuja au yanaota kama uyoga,huwezi na hamuwezi kukaa ndani ya nyumba iliyokuwa haijajengwa au nyumba chafu,ni lazima utengeneze mazingira yakiuhakika na sio ya kubahatisha,ni lazima hayo uliyoyataja yawepo katika mazingira rafiki yanayokubalika.

Yote yatakuja wenyewe na hapo ,yaani tunasema kwa sasa wacha magufuli atuweke juani na hayo unayoyasema yatakuja na tutayala kwenye kivuli,tatizo ni kama watu mliokuwa hamjazoea shida,na ni kweli hamjazoea shida ,mlikuwa mnaenda kazini saa mnazotaka,mnaajiri mpaka waliokufa kwa kuwa mlikua mna kiongozi au viongozi sijui tuwaite dhaifu au wale wanaoona haya na muhali ,kuwajibika na kukemea wanapoona maovu.

Tulieni nchi isafishwe na kama mnavyoona kila siku zinaposogea wanapatikana viongozi wazalendo wenye mwendo unaoendana na kuivuta Tanzania kwenye maendeleo ya hayo uliyoyataja.
 
Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
292
500
Alishindwa kujenga ukuta hivyo hawezi kamwe kuja kujenga ukuta. Binafsi hata anipandishe daraja mara 20! Bado haitakuja itokee nikamkubali.

Muda wake ukiisha aondoke zake. Wengi tumemchoka kupitiliza.
Binadamu n kiumbe cha kubadilika dkk sifuri tu, anaweza akatikisa namba, mkaja na mapambio na mkaandamana juu mei mosi
 
Gai da seboga

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
292
500
Shallow thinking! Ukomo wa miaka kumi haukuwekwa kwa sababu za kijinga kama unavyodhani. Ukomo upo ili kuondoa loophole ya marais wenye tamaa no matter how good their perfoming! Ukisema huyu amefanya vizuri aongezewe muda kipindi kijacho atakuja fashisti na ukifika wakati wa kuondoka atadai na yeye amefanya vizuri sana hivyo anastahili kufia madarakani. Tuheshimu utaratibu wa miaka kumi kwani watanzania wenye uwezo wa kuongoza wako wengi sana.
Kipi bora, aongezewe muda akiwa kayafanya hayo nlosema au aongezewe muda ikiwa wanachi bado tunatafuna nyasi!
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,794
2,000
Akiyafanya mema hayo wote wananchi wataishije kama MASHETANI? Huyu jamaa furaha yake ni kuona tumerudi hadi zama za kale za mawe.
Mtu anayetishia kufunga mitandao ya mawasiliano kwenye zama hizi za sayansi na teknolojia ni wa kumkwepa kama ukoma
 
MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,027
2,000
Habari zenu mabibi na mababu!

Kwanza kabisa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kila mtu anapoambiwa au kusikia kuongezewa muda wa kutawala Rais magufuli anashikwa na ghadhabu na kutamani ata kumpiga mtu ngumi kutokana na ugumu wa maisha uliopo.

Sio watumishi wa Serikali, sio wafanyabiashara, machinga, wastaafu, wanachuo, wahitimu wa chuo, mama ntilie, wachuuzi, n.k wote hawa hawataki kusikia ata kidogo msamiati wa Rais magufuli kuongezewa muda wa kutawala, wamemchoka vibaya mnoo kiasi kwamba mpaka wanajuta kwanini walimpa uraisi na bila kupepesa macho wanatamani ata kesho tu Amalize muda wake wa kutawala waangalie ustaarabu wa raisi ajae.

Na wale wanaoshupalia kuwa aongezewe ni wabunge ambao wapo bungeni wakiona hawana cha kupoteza kwamba akitawala milele basi wao wakijipendekeza watakuwa kwenye maisha salama, lakini viongozi ambao wamemwagwa hawapo ata bungeni ukiwafata uwaambie JPM aongezewe Muda usipokuwa makini wanaweza kukupiga makofi mfano mfate lugola alafu mwambie JPM tumpe milele bhana kama hatokutukana, kwahyo wale wanaoshupalia ni wale ambao wananufaika nae tu ila mzee baba hakuna anaempenda watu washamchoka.

^^^^^^^^^^
Mambo ambayo akiyafanya Rais magufuli Watanzania wenyewe bila kushurutishwa watamlilia na kuandamana barabarani kuomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala ata milele.

1. Kuongeza nyongeza ya mishahara na kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma. (hawa watu wametaabika na wana hali mbaya sana kwa muda wa miaka 6 sasa mpka barabarani wanajiongelesha wenyewe kwa stress, Magu akitaka apate mapambio ya kuongezewa muda wa kutawala basi hawa watu awapandishe mishahara kwa asilimia kubwa % na kuwalipa madeni yao wataongoza kumsifu na kumshinikiza).

2. Kuajiri vijana waliopo mtaani. (siku hizi wahitimu wa vyuo wamejaa mtaani kama njugu vile hawana kazi yoyote ile, sio walimu, sio manesi, madokta, bwana mifugo n.k, hili kundi ni kubwa mnoo na linaongoza kumchukia magufuli vibaya mno adi kutamani Mungu angempenda zaidi mana mtaani wanataabika hatari, vijana hawa hawana ata familia lakini wanaongoza kuwa na msongo wa mawazo).

3. Wastaafu kulipwa pesheni zao. (hapa wazee wengi wanasononeka na kushikwa na hasira mtu amemaliza kutumikia taifa lakini haki yake mwenyewe anazungushwa mpaka anakata tamaa, mzee kastaafu ila ana miaka mitano bado hajapewa pesa zake hayo mapenz yakutaka rais aongezewe muda wa kutawala atayatolea wapi!! Hawa ni wengi mnoo wengine mpaka wanakufa wamekosa stahiki zao.)

4. Wafanyabiashara kupunguziwa kodi za hovyo zinazowapekea kufunga biashara zao.

5. Wakulima wa korosho kulipwa pesa zao. (hawa watu sio tu kuwa wana hasira na huyu bali wana kisasi kikali san na ukitaka kujua machungu yao uwakute wanaongea kikabila, kiasi kwamba wanamuombea majaliwa angalau aje kuwa Raisi ili apunguze machungu ya watu wake wa kusini.)

6. Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kupunguziwa riba.

7. Wakulima kutafutiwa masoko ya uhakika na kupunguziwa gharama za pembejeo.

8. Kuzuia mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali. Mf. Mafuta, sukar, cement.

9. Mikopo himilivu kwa vijana na wanawake.

10. Bima bora za afya kwa Watanzania.

11. Kuhamasisha Matajiri duniani kuwekeza viwanda mbalimbali Tanzania.

Mh Raisi akiyafanya hayo bila chuki wala roho mbaya Watanzania wenyewe wataamua na kumshinikiza kwa maandamano atawale ata milele hadi afie ikulu.

~Gai da Seboga
Aondoke tu muda ukifika, tumenyanyasika sana hayo unayosema tunahitaji kwa Rais ajae sio huyu mwenye roho ya korosho.
 
permanides

JF-Expert Member
May 18, 2013
5,435

Hakuna hoja yenye mantiki hapo, JK alifanya yote hayo, mbona hatukumwongezea muda, huyu amalize miaka yake (Mungu akimjalia) asepe ili tuwe na rais mwingine na mwenye mawazo tofauti. Tena terms za miaka 5 ni ndefu sana, zinapaswa ziwe miaka 4.
 
Lumwago

Senior Member
Aug 20, 2020
142
250
Katika yote umesahau kitu muhimu Sana. Uhuru wa Demokrasia. Watu wakiwa na Uhuru wa kusema hayo yote watayadai bila uwoga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom