Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Ameweza kiasi fulani kukemea vikali ufisadi kwa vitendo. Nampa "C". Mengine yote "F". Kwenye uchumi nampa negative "F" kabisa. Hakuna nchi inayoendeshwa kibepari inaendelea bila biashara; yeye badala ya kuwavutia wafanyabiashara anawavunja moyo kupitia sera mbaya ya kodi na masimango mengi. Uongozi bora hajui; anajua kutisha. Teuzi zake ni kielelezo cha kushindwa kwake kama kiongozi. Anaua demokrasia kwa kasi na anaonekana kuamini kutoka moyoni kwamba bila udikteta hakuna maendeleo. Inasikitisha. Hapendi kukosolewa na hawezi kuongea kwa mpangilio akaeleweka na kuheshimika kwa kauli zake kama Kiongozi. Akijirekebisha haya machache niliyomkosoa ana nafasi ya kuiletea Tanzania maendeleo maana bado ana muda mrefu mbeleni.
 
Mimi bado nampa Muda kwenye Alama gani nampa, Mwaka Mmoja hautoshi kumpima, atleast Miaka 2 na kuendelea.
Alichofanikiwa Kubwa, kurudisha Nidhamu ya Utawala na Kazi, Kabana Mianya ya MaDili.
Alichoshindwa ni U CCM, bado ana elemet za U CCM, Lugumi, Escrow ... Hajagusa either kwa kuogopa au Maji kumzidi kimo.
Alichoniuzi, ni kumuita Mfalme wa Morocco "Mtukufu" na yule Boss wa Mabohora.
Mtukufu ni Mungu pekee.
Ila Ngosha nazidi kumwombea, maana nae ni Mwanadamu. Akaze Buti.


Mnamo tarehe 5 mwezi huu wa Novemba, mheshimiwa rais wetu mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atatimiza mwaka mmoja tokea ashike madaraka ya uongozi wa nchi yetu pendwa, Tanzania.

Katika huu mwaka, kuna mengi ambayo serikali yake imeyafanya. Mengi hayo ni pamoja na mazuri na mabaya.

Sasa, ndani ya huu mwaka wewe mwana JF una maoni gani juu ya utawala wa huyu mtukufu rais wetu?

Kama ni mtihani, utampa alama gani? A, B, C, D, E [kwa effort], au F?

Kafanikiwa yepi na kashindwa kwenye yepi?

Yepi ni mengi? Mafanikio ni mengi au kushindwa ndo kumekuwa kwingi zaidi?

Binafsi nampa alama ya E.

Nampa alama hiyo kwa jitihada zake ambazo amezionyesha katika kutaka kulirudisha taifa ndani ya mstari hususan kwenye mambo ya uadilifu, upigaji vita rushwa/ufisadi, na kadhalika.

Siwezi kumpa alama nyingine zaidi ya hiyo kwa sababu taifa lilikuwa limefikia pabaya mno kiasi kwamba hata angekuwa nani, ndani ya mwaka mmoja tu hawezi kurekebisha yote yaliyokuwa yameharibika [chini ya uongozi wa CCM].

Nadhani ni mtu mwenye nia nzuri na iliyo ya dhati kabisa katika kutaka kwake kulirudisha taifa kwenye mstari unaofaa.

Ila ndo hivyo tena. Sina hakika sana na njia, hekima, na busara zake anazozitumia katika kulifanikisha lengo hilo.

Leo anaweza kufanya jambo fulani ambalo ni zuri na la kuungwa mkono lakini kesho yake anakuja kufungua mdomo wake na kutoa kauli ambayo mtu inakuacha ukitikisa na kukuna kichwa chako na hata kubaki mdomo wazi.

Mwisho wa siku mtu unabaki kuduwaa tu na usijue hata umweke wapi, kwenye kundi gani!

Nyote mnakaribishwa kutoa tathmini zenu za huu mwaka mmoja wa utawala wa rais Magufuli.
 
He deserves D.

Kuna mahali niliona maelezo ya haya madaraja.

A: Mtu ana uelewa mkubwa wa mambo na uwezo mkubwa wa uchambuzi. Hahitaji msaada/uelekezi katika masuala mengi.

B: Mtu ana uelewa mkubwa wa mambo na uwezo wa kutosha wa kufanya uchambuzi.

C: Mtu ana uelewa wa mambo ya msingi na anaweza kufanya uchambuzi wa msingi

D: Mtu ana uelewa mdogo na anahitaji msaada mkubwa katika kufanya uchambuzi

E: Mtu anahitaji usaidizi katika maeneo karibu yote

F: Crippled
 
Maoni ya Profesa yanaweza kutusaidia kutoa alama :

Prof. Issa Shivji : Tathmini na uchambuzi wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ina

  • Mtazamo wa uchumi
  • Siasa na Demokrasia ni ambao tunaweza kuuita ''Mfumo wa Utawala''
  • Mtazamo wa mahusiano ya Tanzania na nchi za nje kikanda, bara la Afrika na Kilimwengu pamoja na mikataba ya kimataifa kama EPA n.k
  • Tusifanye mazoea ya kuvunja Katiba
  • Rushwa na ufisadi
  • Ukwepaji kodi
  • Uchumi wa kitaifa (unaangalia ndani uzalishaji wa viwanda) VS Uchumi wa Kikoloni ( Unaangalia nje kuuza mali ghafi nje)
  • Uzalishaji (Kilimo + Viwanda) unafuatwa na biashara na siyo biashara kufuatwa na uzalishaji
  • Uwekezaji toka nje tusiletewe viwanda vichafu na mazingira duni ya kibinadamu kwa wafanyakazi
  • Rais hajazungumzia kwa msisitizo Kilimo na Ufugaji ktk kipindi hiki cha mwaka mmoja
  • miundo mbinu ifuate lengo la usafiri wa barabara toka vijijini (uzalishaji) kuunganishwa na mfumo wa reli na usafiri wa maji ili kuwawezesha wazalishaji wadogo walio wengi vijijini kunufaika kiuchumi
  • Mfumo wa utawala ngazi Mkoa uwe kazi yao kuu ni kuratibu badala ya ''kutawala''
  • Ni makosa kudhani demokrasia inaishia ngazi ya kitaifa
  • Siasa ni ushawishi na siyo ''kuamrisha'' , mijadala ni muhimu kuliko kutoa amri au matamko
  • Halisi siyo shwari Zanzibar na kusababisha nchi za nje kuuingilia siasa zetu za ndani
  • Udikteta
  • Bunge
  • Siasa za nje msimamo haupo : Afrika kupinga ukoloni , nchi ya Afrika Kukalia nchi nyingine ya Kiafrika, Ubaguzi wa rangi. Msimamo kimataifa Ubeberu . Ukoloni Mamboleo , Kutofungamana na Nchi za Kibabe

Source: Issa Shivji
 
Pongezi nyingi kwa Rais wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kutimiza mwaka mmoja wa uongozi wake wenye mafakio makubwa sana.

Hakika watanzania wengi tunajivunia uongozi wako, na tambua bado unakazi kubwa ya kutuongoza kwa miaka minne iliyobaki, naomba usipunguze kasi yako ya utendaji ili kufikisha Tanzania yenye Amani,Utulivu na Maendeleo.
Hapa Kazi Tu
Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele
#UMOJANIUSHINDI
[HASHTAG]#MwakaMmojaJPM[/HASHTAG]
JESHI5.jpg
 
Hakika nampenda sana Rais Magufuli. Anafanya mambo kwa manufaa ya Watanzania
 
Ha ha ha, jamaa amesema maendeleo yaliyopatikana ni Utulivu na Amani!
 
Bado maendeleo hayajaanza kuonekana sema angalao inatia matumaini
 
Hakika nampenda sana Rais Magufuli. Anafanya mambo kwa manufaa ya Watanzania

Ngoja nikusaidie mkuu. Baadhi ya mambo aliyofanikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja ni:
1. Kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kutoka bil 800 hadi tril 1.2;
2. Kuongezeka kwa nidhamu ya maumizi ya fedha za umma
3. Kuwashughulikia watumishi wazembe na wasiozingatia kanuni za utumishi.
4. Kubainisha na kuwaondoa watumishi hewa katika payroll ya serikali
5. Kuzuia safari na shughuli za serikali zisizokuwa na tija ikiwemo safari za nje ya nchi

Nisaidie kuongeza mengine katika list hiyo ili tufikishe angalau 10, kisha uonyeshe mafanikio hayo yameleta impacts gani kwa wananchi. Mimi binafsi nimeishiwa.
 
Kiukweli Kabisa, Rais JPM amefanya mambo fulani mazuri ya msingi. Kwa ujumla katika huu mwaka mmoja, amefanikiwa KUANZA kujenga misingi ya uchumi endelevu. Ni tatizo tu la watu wanaomshauri. Kipaumbele cha kwanza kabisa kwa Rais kisingekuwa "Nchi yenye viwanda". Hicho kiko mbali sana. Utaanzaje na kipaumbele hicho wakati huko Karagwe watu wanalala na njaa? kuna nchi gani ambayo imeanza kuwa ya viwanda katika dunia hili huku ikiwa na matatizo madogo kama kujitosheleza kwa chakula? Je ni kweli wote tunasoma historia ya nchi zilizofanikiwa na kuelewa vizuri mambo haya? JPM kuna vitu amepewa na baadhi ya mburura wa chama XX kuuza kama Sera lakini hazitekelezeki. He has an oppotunity to capitalize on things that are doable. Ajenge taasisi imara na mifumo ya usimamizi wa fedha za umma. Tayari ameshapata mafanikio makubwa hapa. Pili, aweke mifumo imara na endelevu ya ukusanyaji wa kodi. Hapa hajanikiwa sana, kwa sababu ameendelea zaidi kuwasikiliza wale Mburura, huku akiacha mawazo mengi mazuri ya watu ambao yeye hawaamini na kuwasikiliza. Akifanikiwa katika maeneo hayo juu, ndipo aanze kuimarisha, kufufua na kuanzisha viwanda vidogo vidogo. Safari ya Tanzania ya viwanda lazima ianzie hapo.....To be honest, Tanzania ya viwanda haitapatikana wakati wa utawala wake wa miaka 10. If i am a liar, keep this post and let's meet in 2021, God wishes....
 
Kama sehemu ya kuimarisha mifumo ya taasisi na uwajibikaji, aanze kuhakikisha taasisi za umma zinafanya kazi zake, na awabane waonyeshe matokeo (si michakato) ya kazi hizo. Kwa mfano, vitengo vya ujenzi wa barabara, lazima vionekane barabarani vikifanya kazi za kuziba mashimo bararani na kurekebisha miundombinu. Vitengo vya usafi na mipango miji, lazima vionekane vikisimamia uzoaji taka, na kusimamia ujenzi, nk.
Pia katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza, ashughulikie zaidi kero ndogo ndogo ambao zinawapa shida wananchi wengi. Nyingi ya hizi ziko ndani ya uwezo wa serikali kwa sasa. Kwa mf, suala la msongamano wa magari katika jiji la Dar linawagusa watu wengi sana, na lina athari kiuchumi kwa nchi yetu. Anapaswa kuonyesha tofauti kati ya kuongea sera na kuondoa tatizo kabisa.

Kwa upande wa hali ya kisiasa. Hapa anapaswa kufanya kazi zaidi. Anapaswa kuonyesha yeye ni Rais wa Watanzania wote. Kuna elements fulani sasa hazijakaa vizuri. Ajitahidi sana kutoonyesha hasira wala chuki kwa watu fulani, yeye abaki kuwa bold kwenye issues. Namna nyingine ya kupambana na wapinzani wako wa kisiasa, ni kuonyesha kwa umma kwamba you are treating everyone equal. Nitatoa mfano: Badala ya kuzuia vyama vya siasa kufanya mikutano au maandamano, unawaacha wafanye hivyo (kwa sababu vipo kisheria), na unaruhusu vyombo vya dola kuhakikisha vinatoa ulinzi unaohitajika. Ikitokea vyama hivyo vimesababisha dosari fulani, wewe unarudi kwa wananchi kusema.."Mmeona..."? Watu wenye common sense watakuelewa na kukuunga mkono kwa wingi..

Muache kusema tunakosoa tu hatutoi ushauri...
 
Jana usiku baada ya Taarifa ya Habari Kituo cha ITV kiliandaa Kipindi Maalum Mwaka mmoja wa Utawala wa Magufu. Sasa kilipofika kipindi cha kuwahoji Raia mmoja mmoja toka sehemu mbali mbali za Nchi, wengi wao majibu yalifanana. Yaani walimshukuru Magufuli kuwabana Watumishi wa Umma na kusema sasa kuna nidhamu na heshima ipo pia walikuwa wanachezea fedha ya Serikali pia Mafisa. Pia walioneshwa kufurahia na huu utaratibu kwa kubana Matumizi kuwa ni Mzuri. Sasa kilichonisikitisha ni kuwa, anaongea vizuri hayo mwanzo kama preamble sasa baadaye anaanza kulalamika tena kuwa Magufuli alegeze kidogo maana pesa mtaani ngumu na haipatikani. Lakujiulizia Kulikuwa na haja gani ya kumsifia katka kubana matumizi wakati unasema hali ngumu tena pesa hakuna?

Unajua layman wengi wameaminishwa kuwa mchawi wao alikuwa ni mtumishi wa Umma ndiye alikuwa mfujaji wa pesa na fisadi wakati siyo kweli, mbaya wao ni CCM na Watu wake, yatosha kusema hivyo. Swala la Kujiuliza je huo Mzunguko wa pesa mnaousema haupo ni nani amabaye alikuwa anauundeleza?

Kwa ufupi ni kuwa Serikali ndiyo mwenye matumizi makubwa katka nchi yoyote na hayo matumizi yake ndiyo yansababisha aidha kuwe na Mzunguko Mzuri wa Pesa kwa Raia ama lah kutegemea na kiwango gani kinaenda kwa hao wananchi. Na haya matumizi asilimia kubwa ni kupitia kwa huyu huyu mnayemchukia mtumishi wa Umma. Sisemi waibe, hapana ila Sitahiki zao wapewe, Watumishi wengi wa Umma mishahara yao ni midogo mno japo najua mnaamini wanapata mamilioni kitu ambacho si kweli.

Hii Serikali ikimuwezesha Vizuri huyu Mtumishi wake, Mtumishi ndiye anaenda kutumia hii pesa kwa manunuzi mbalimbali na kufanya shughuli zingine za maendeleo na ndiyo hupelekea pesa kumfikia hata yule wa Nanjilinji.

Njia zingine za kuongeza Mzunguko wa pesa kwa wananchi ni pamoja Serikali kufanya miradi ya maendeleo ampapo pesa inaingia pia kwa wananchi kupitia manunuzi na Ujira wa waliopo kwenye sekta hiyo.

Wananchi wa Kawaida naomba tubadilike, tuache kuwaona Watumishi wa Umma kama ndiyo Wabaya wenu kama mnavyoaminishwa. Mbaya wenu wa uchumi ni huyo huyo mnayemsifia.

NB: Wengi wao wa waliohojiwa ni Mama Ntilie, Wauza Magenge, Wengine waliwamakata tu Barabarani na inaonesha Uelewa wao kitaalam katka mambo ya Uchumi ni mdogo saana.
 
Mkuu umenena vyema hasa kuhusu watumishi na mapato yao. Lakini sasa niulize kitu kimoja: Je, mishahara ya watumishi imepunguzwa au watumishi hawapati mishahara? Nasema hivyo kwa sababu kama mishahara haijapunguzwa na wanapata mishahara yao kama zamani imekuwaje matumizi yapungue na hivyo kusababisha pesa kukosekana mitaani?
 
Mkuu umenena vyema hasa kuhusu watumishi na mapato yao. Lakini sasa niulize kitu kimoja: je mishahara ya watumishi imepunguzwa au watumishi hawapati mishahara? Nasema hivyo kwa sababu kama mishahara haijapunguzwa na wanapata mishahara yao kama zamani imekuwaje matumizi yapungue na hivyo kusababisha pesa kukosekana mitaani?
Hakuna ongezeko la mshahara na hali maisha yanapanda gharama kila uchwao.
 
Back
Top Bottom