Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Usichokijua ni sawa na usiku wa kiza!

Fedha za wahisani zipo katika mafungu mawili: Kuna budget support funds ambazo huingizwa katika bajeti ya serikali ambazo Waziri wa fedha huzisoma bungeni na kuna fedha ambazo nchi wahisani hupitishia katika mashirika yao ya maendeleo kama DFID, GIZ, JICA nk na pia zipo za mashirika ya kimataifa kama UNICEF, IAEA, UNDP, WFP, WWF, NGOs za kimataifa nk ambazo hazipitii hazina ya serikali!

Fedha hizi ambazo hazipitii hazina ndizo unaona zinatumika hadi sasa katika warsha mbali mbali zinazofanywa katika mahoteli! Serikali haihoji fedha hizi na wala haina sababu ya kuzihoji matumizi yake! Na hata posho zake wakati fulani hutofautiana na posho za serikali!
Pia miradi yao ya maendeleo haimo katika mipango ya serikali ingawa serikali inaweza kuwa na taarifa ya utekelezaji wake kwa sababu ina malengo maalumu.

Fedha za wahisani zinazoingizwa katika bajeti ya serikali (budget support) hizi zinafuata taratibu za fedha serikali kama kawaida na wahisani hufuatilia matumizi yake!
Ufafanuzi Mzuri saana huu!
 
Habari wanajamii matumaini yangu ni kuwa mnaendelea salama na jukumu la kujaribu kutetea taifa letu kutoka katika janga la umasikini,
Mwezi huu tarehe 5, Mheshimiwa magufuli ametimiza mwaka mmoja Pale nyumba ya Ikulu magogoni,
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kajitahidi kufanya kazi kwa kadri ya uwezo wake, watu na watanzania kwa ujumla wamejikita katika kuangalia mafanikio tu bila kuangalia ni sehem gan kavuruga kidogo kwa kipindi cha mwaka mmoja,
Chini nithainisha maeneo aliyokosea kama mkuu wa Nchi,
1. KUDHANI NA KUTEGEMEA KUWA KUKOSEKANA KWA HELA KWA WANANCHI MFUKONI NDIKO KUTAWAFANYA TU WAFANYE KAZI KWA BIDII BADALA YA KUWAPA MBINU NA MAZINGIRA MAZURI YA KAZI,
Mara kadhaa watu wanasema hakuna hela na hakuna kweli tusijifanye hatuoni swala ili, linaumiza sana linasababisha kushuka kwa ajira, uwekezaji, na saa nyingine kunasababisha kukosa huduma nyingine muhimu ambazo zinapatikana kutokana na pesa,
2. KUONEKANA SERIKALI YA MTU MMOJA, YAAN ONE MAN SHOW, ndani ya mwaka mmoja yeye mkuu wa kaya kafanya kazi kuzidi waziri yeyote yule, na hakuna kinachofanyika kuwaandaa hao mawaziri kuwa, na hakuna mkakati wa kufanya mfumo wote uendane kama kasi yake.
3. AMEJENGA DHANA YA KUOGOPWA HATA KUKOSOLEWA,
Mawaziri, wabunge hasa wa CCM kutoa bashe , wakurugenzi, wachumi, mahakimu na wengine wengi wako kimya sana kwa bahadhi ya mambo ambayo yanapaswa kutolewa ufafanuzi, hivyo watu wanaogopa mnoo, ili ninamshauri mkuu ajenge jamii rafiki kuliko kumuogopa maana watazaliwa wanafiki wengi wa kumdanganya sana kwa mambo mbali mbali na baadae kuleta madhara makubwa katika nchi yetu, na hii ni hatari sana

4.KUKOSEKANA UAMINISHAJI WA WANANCHI JUU YA KIASI KINACHOKUSANYWA , wananchi hawafurahii tu kusema tumeongeza makusanyo ya kodi kutoka 800 billion mpaka 1.3 trill, wakati serikali haina hela hata za kuajiri haina, za kushughulikia majanga haina, za kusafirisha watumishi haina, je hapo ni kweli zinakusanywa kweli au ni kwenye makaratasi tu,?

5. AJIRA KWA VIJANA
Ajira ndo ulikuwa wimbo mkubwa sana kwenye kampeni, lakin mpaka sasa utaambiwa tumeajiri mahakimu 100, yaan katika janga lililopo utasema umeajiri watu 100 na unajinasibu kuwa umeajiri,

6. KUKOSA VIPAUMBELE KATIKA MATUMIZI YA HELA ZA NCHI
Hela nyingi zilizotumika kununua ndege direct ati kisa tutambe eti hatujakopa saa nyingine nahisi haikuwa sahihi, hizo ilibidi zikajenge zahanati, zinunue mashine za T-scan za kutosha na kuwapatia watoto pesa za kusoma, lakin ndege ndo ikawa kipaumbele,

7. KUTANGAZA WATUMISHI HEWA NA KUISHIA KUWA VICHWA VYA HABARI KWENYE MAGAZETI, Hawa hawakuchukuliwa hatua zinazostahili, wametangazwa tu basi hakuna kingine kilichoendelea,

hayo ndo mapungufu ya serikali kwa mwaka mmoja naombeni kwa unyenyekevu tuongeze au kukosoa bila kuvunja sheria za nchi yakawa mengine
 
Habari wanajamii matumaini yangu ni kuwa mnaendelea salama na jukumu la kujaribu kutetea taifa letu kutoka katika janga la umasikini,
Mwezi huu tarehe 5, Mheshimiwa magufuli ametimiza mwaka mmoja Pale nyumba ya Ikulu magogoni,
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, kajitahidi kufanya kazi kwa kadri ya uwezo wake, watu na watanzania kwa ujumla wamejikita katika kuangalia mafanikio tu bila kuangalia ni sehem gan kavuruga kidogo kwa kipindi cha mwaka mmoja,
Chini nithainisha maeneo aliyokosea kama mkuu wa Nchi,
1. KUDHANI NA KUTEGEMEA KUWA KUKOSEKANA KWA HELA KWA WANANCHI MFUKONI NDIKO KUTOFANYA TU WAFANYE KAZI KWA BIDII BADALA YA KUWAPA MBINU NA MAZINGIRA MAZURI YA KAZI,
Mara kadhaa watu wanasema hakuna hela na hakuna kweli tusijifanye hatuoni swala ili, linaumiza sana linasababisha kushuka kwa ajira, uwekezaji, na saa nyingine kunasababisha kukosa huduma nyingine muhimu ambazo zinapatikana kutokana na pesa,
2. KUONEKANA SERIKALI YA MTU MMOJA, YAAN ONE MAN SHOW, ndani ya mwaka mmoja yeye mkuu wa kaya kafanya kazi kuzidi waziri yeyote yule, na hakuna kinachofanyika kuwaandaa hao mawaziri kuwa, na hakuna mkakati wa kufanya mfumo wote uendane kama kasi yake.
3. AMEJENGA DHANA YA KUOGOPWA HATA KUKOSOLEWA,
Mawaziri, wabunge hasa wa CCM kutoa bashe , wakurugenzi, wachumi, mahakimu na wengine wengi wako kimya sana kwa bahadhi ya mambo ambayo yanapaswa kutolewa ufafanuzi, hivyo watu wanaogopa mnoo, ili ninamshauri mkuu ajenge jamii rafiki kuliko kumuogopa maana watazaliwa wanafiki wengi wa kumdanganya sana kwa mambo mbali mbali na baadae kuleta madhara makubwa katika nchi yetu, na hii ni hatari sana

4.KUKOSEKANA UAMINISHAJI WA WANANCHI JUU YA KIASI KINACHOKUSANYWA , wananchi hawafurahii tu kusema tumeongeza makusanyo ya kodi kutoka 800 billion mpaka 1.3 trill, wakati serikali haina hela hata za kuajiri haina, za kushughulikia majanga haina, za kusafirisha watumishi haina, je hapo ni kweli zinakusanywa kweli au ni kwenye makaratasi tu,?

5. AJIRA KWA VIJANA
Ajira ndo ulikuwa wimbo mkubwa sana kwenye kampeni, lakin mpaka sasa utaambiwa tumeajiri mahakimu 100, yaan katika janga lililopo utasema umeajiri watu 100 na unajinasibu kuwa umeajiri,

6. KUKOSA VIPAUMBELE KATIKA MATUMIZI YA HELA ZA NCHI
Hela nyingi zilizotumika kununua ndege direct ati kisa tutambe eti hatujakopa saa nyingine nahisi haikuwa sahihi, hizo ilibidi zikajenge zahanati, zinunue mashine za T-scan za kutosha na kuwapatia watoto pesa za kusoma, lakin ndege ndo ikawa kipaumbele,

7. KUTANGAZA WATUMISHI HEWA NA KUISHIA KUWA VICHWA VYA HABARI KWENYE MAGAZETI, Hawa hawakuchukuliwa hatua zinazostahili, wametangazwa tu basi hakuna kingine kilichoendelea,

hayo ndo mapungufu ya serikali kwa mwaka mmoja naombeni kwa unyenyekevu tuongeze au kukosoa bila kuvunja sheria za nchi yakawa mengine
Kuwa dhulumu watu wa Tabora pesa zao walizo pewa ili wajenge waondoke ktk mahema
 
Daima serikali haijengi viwanda wala kufanya biashara ila huandaa mazingira mazuri kwa wananchi wake na kwa wawekezaji na pia kuweka vivutio kwa wawekezaji kuwekeza katika nchi husika.hayo yote hayafanywi hapa,badala yake yanafanywa mambo ambayo huzorotesha na kuwafukuza wawekezaji na wafanya biashara wa kila ngazi.huwezi kupandisha kodi kwa sifa ili ukusanye hela nyingi na kusifiwa huku hamna hele inayoingia ndani ya nchi kupitia uwekezaji.katika hili serikali imekosea sana na tukiendelea hivi nchi ya viwanda na uchumi wa kati tuisahau..tuchukulie mfano mdogo tuu wa landing charges ambayo tanzania inaongoza kwa kuwa na high landing charges more than even its neighbours..hii imefanya nauli kuongezeka maradufu na aviation industry kudumaa huku nchi kama kenya yenye landing charges ndogo ikiendelea kupaa kwa aviation industries.wakati huohuo kuna kodi kubwa katika aviation mpaka kufanya makampuni mengine kuwa na malimbikizo ya kodi wanayoshindwa kulipa on time kisa gharama za uendeshaji ni kubwa mno.
Ukitaka kuangalia effects of raising tax kwa makampuni na wafanyabiashara angalia marekani ambapo makampuni makubwa ya nchi ile kama apple walikimbia nchi na kwenda kuweka base zao barani asia hivyo product hutoka asia na kuuzwa tena US na kampuni ya ndani ya nçhi na hii imefanya gharama za bidhaa hizi kuwa kubwa ukilinganisha na hapo mwanzo zilipokuwà zinatengenezwa nchini humo.hii imemfanya trump kuiwela katika ilani yake kama kipengele cha kwanza cha kupunguza kodi ili makampuni yaweze kurudi na kuzalisha nchini mwao na kkuongeza ajira kama ilivyokuwa mwanzo..
Lakini nchi nyingine zenye maendeleo ya viwanda na biashara zinapopunguza kodi ili kujenga mazingira rafiki kwa wafanya biashara na makampuni sisi ndo kwanza tuko bize sio tuu kuongeza kodi kwa makampuni na sekta mbalimbali bali hadi kwa wananchi mpaka kwenye mishahara yao.hii ndio sababu kubwa ya mzunguko wa hela kuwa mdogo na hela kuadimika mtaani just because mazingira sio rafiki.kama hatutabadilika hapa tusitegemee kubadilika hata ndani ya miaka 10
 
leo ni siku mpya

SHKAMOO MH MAGUFULI
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZNAIA
NA MWENYEKITI WA AFRICA MASHARIKI.

Mh Magufuli
naandika waraka huu kichwa kikiwa kimeshika moto, yaani nawaza bila majibu hapa.

Mh Magufuli
Kumbuka ulipoingia madarakani ulitiahidi maisha mazuri, na kuifanya tanzania nchi ya maziwa na asali.

Mh Magufuli
sasa ni mwaka mmoja umepita, mambo yameanza kugeuka kinyume nyume, ni kweli umeanzisha mahakama ya mafisadi (HONGERA) umesimamia uwajibikaji serikali (HONGERA) umeweza kuimarisha makusanyo ya kodi (INGAWA NINA MASHAKA JUU YA HILI LAKINI HONGERA)

Mh Magufuli.
kuna jambo ambalo bado linanitatiza hapa.
GESI NI MALI ASILI YETU, TUNAICHIMBA TANZANIA KULEE MTWARA, lakini inakuwaje hawa majamaa wa Tanesco wanataka kuongeza bei ya umeme.
Je wanajua kwa kuongezeka kwa umeme kila kitu kitapanda bei? ama wale wachina waliojenga bomba wameongeza kodi ya bomba?

Mh Magufuli.
Miezi yako michache ya mwanzo uliahidi sukari itakuwa 1800, kulikoni tena mkuu mbona huku bado ni 2500 tena wanaiuza hadharani kabisa?

Mh Magufuli
Yale basi ya mwendo kasi mmiliki wake ni nani, mbona yamekuwa kero kwa wananchi?

Mh Magufuli
la mwisho kwa leo ni hili la bodi ya mikopo.

HIVI BODI ILIVYOTUKOPESHA PAMOJA NA MWANAO, ilitegemea tulipeje hiyo mikopo. JE WANATAARIFA KUWA TANGU UMEINGIA HAKUNA AJIRA MPYA, AMA KUPANDISHA VYEO WATUMISHI?

je hao bodi wanategemea tulipe kutoka kwenye kipato gani? Mh, Kule mjini kumejaa wahindi, waarabu, wakenya na wachina kufanya kazi ambazo sisi tulipaswa kuzifanya ni tuweze kuchangia deni la bodi, Je unamkakati gani katika kuwafukura watu hao.

Mh Magufuli
Bodi yetu ya Mikopo isitake kuligeuza hili swala ni swala la kiuhalifu, wakumbuke kuwa Mikopo kwa Wanafunzi ni sera ya nchi katika kuinua kiwango cha elimu ili waweze kuboresha utendaji katika nchi.

NAISHAURI BODI KABLA YA KUJA KUDAI, KWANZA WANGETUELEZA HAO WANAFAIKA WA MIKOPO WALIMALIZA CHUO GANI, NA SASA HIVI WAPO KATIKA ENEO GANI LA AJIRA

Mh Magufuli naamini wewe ni mchapa kazi, na utaweza kulisongesha hili gurudumu, ULICHAGULIWA KWA KURA NYINGI ingawa mimi sikukupigia kura HIVYO NAAMINI UTAWATENDEA HAKI WATANZANIA WOTE, MASIKINI NA WALE MATAJIRI.

nakutakia asubuhi njema Mkuu Wangu

na Nakuombea Mungu Wangu Akutangulie katika kila amuzi dhidi ya Watanzania.
 
Kuna muda hata mimi nilikuwa mmoja wa watu wanaowalaumu wale waliokuwa wakitaka kujua muheshimiwa Rais kafanya nini kwaajili ya kututoa kule tulikokua.

(NCHI ILIYOOZA)tulikuwa tukiwaambia yani mnataka kuona mabadiliko na maendeleo ndani ya miezi hii miwili tangu achaguliwe?ikaja yani maendeleo yapatikane ndani ya miezi mitatu tu tangu aapishwe?sasa mwaka umekatika ni mengi yametokea na yamesemwa,matamko lukuki ndani ya mwaka mmoja na miezi sasa je? kuna nafuu yoyote?au tusubiri tena mwaka mwingine uishe ndio tuanze kuona mwanga wa tunakoelekea kama taifa?vipaumbele na matamko ndio yanatupa picha kama tunaenda kwenye njia au tumetoka tumeingia machakani?
kwa maoni yangu mimi naona bado sana,sioni mwanga wowote sijui nyie.
weka maoni yako yatusaidie sisi wengine ambao tunaanza kukata tamaa.
 
Naona Ana jitahidi tatizo mawaziri
tatizo sio maaziri tu,tatizo ni viongozi wengi wa serikali hii wengi wanasubiri mwongozo kutoka kwake,yani akisema hakuna msaada wa kujengewa nyumba wahanga kesho utasikia mkuu wa wilaya nae kakazia jambo hilohilo,akisema hakuna chakula cha msaada utasikia wakuu wa mikoa nao wanakazia humohumo lakini hakuna anaetokea kutoa maamuzi hayo kabla mkuu mwenyewe hajasema.
 
Mhaa! Unaweza kusema kuna giza lakini mimi hatagiza silioni nini mwanga waswahili wanasema dalili ya mvua ni mawingu lakini hata dalili ya uwepo wa hayo mawingu haupo matamko mengi uwongo umegeuzwa ukweli tuendako ni kubaya zaidi ila mi nampa miaka 3 moja ushakatika
 
Back
Top Bottom