Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Tatizo wabongo tukipata elimu kidogo tu..tunakuwa wajuaji kupita kiasi..kila kitu tunataka kutumia elimu ya darasani...vingine unatakiwa usikilize wazoefu...hili ndo tatizo la awamu hii....economics mimi...agriculture mimi...transportation mimi..n.k
 
Bahati mbaya sikuhizi wenye PHD ndio wameula,wanaingizwa kwa wingi kwenye siasa mwisho wa siku wanasahau taaluma zao na kuona kumbe kwenye siasa ndio ulaji ulipo.hili nalo ni tatizo la msingi.
 
Wakuu leo nataka kujua ni kwa kiasi gani magufuli ametekeleza yale aliyoyaahidi kipindi cha uchaguzi .

Kwa upande wangu hakuna hata kimoja alichokiahidi na kukifanya

Mfano aliahidi Tanzania ya Viwanda lakini haipo

Aliahidi mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu haitasumbua lakini imekuwa kinyume chake kwa sababu mwaka jana waliopata mkopo walikuwa zaidi ya laki moja lakini mwaka huu waliopata mkopo walikuwa watu elfu 20 tu basi na hata baada ya ku appeal hakuna kilichobadilika watu wameappeal zaidi ya elf 50 lakini waliopata ni watu elfu.moja miatano na hamsini na Mohammed tu basi ,na pia hata hao waliobahatika kupata mkopo wengi wao pesa zinaasumbua kupewa kwa kuwa wengi wamepata nusu na wengine wamepata awamu moja tu basi

Pia kingine suala la ajira hili nalo limekuwa kizungumkuti sana kwa sababu yeye aliahidi neema kwa wafanyakazi ikiwemo kuongeza posho matokeo yake amepunguza posho pia amezuia ajira tangu aingie madarakani watu wamekuwa wakifukuzwa kila kukicha bila ya kuwa na mbadala wa watu wengine wa kwenda kujaza nafasi hizo

Pia amekuwa mtu wa kuwakata mishahara wafanyakazi wengi serikalini kwa kigezo cha kubana matumizi hali ya kuwa hao wafanyakazi hawajapunguziwa working hours pia hizo hela ambazo wamebana matumizi hazijulikani huwa zinaenda wapi kwa maana kila kukicha afadhari ya jana

Pia alitoa ahadi kuwa ikiwa mfanyakazi akiharibu sehemu moja hiyo itakuwa ntolee hatoweza kumpa tena nafasi sehemu nyingine mfano mtu akiharibu mwanza asitegemee atapewa tena nafasi dar es salaam lakini kumbe ilikuwa changa la macho kwa kuwa tunaona kila kukicha mtu anatumbuliwa sehemu A anaenda kupewa cheo sehemu B mfano mzuri mama Anna Malecela

Pia aliahidi kutoa milion 50 kila kijiji lakini pia hii nayo imekuwa ahadi hewa

Pia alitoa ahadi ya kuwapa laptop walimu wote Tz nzima lakini pia ni changa la macho

Pia bila kusahau alisema kuwa suala la umeme kukatika itakuwa historia lakini walaaa lilikuwa changa la macho umeme umekuwa ukisumbua sana mara 3 zaidi ya kipindi cha JK

Pia alitoa ahadi kuwa tukimchagua hakuna mwanafunzi atakaye kaa chini lakini mpaka leo wanafunzi wanakaa chini

Pia alitoa ahadi kuwa tukimchagua atahakikisha mambo ya kodi atapunguza kwa kiasi kikubwa na kufuta kabisa baadhi ya kodi lakini imekuwa kinyume chake kodi zimekuwa kubwa sana kuliko kawaida

Pia ali ahidi kuwa atajenga mahakama ya mafisadi ikiwemo kuzishughulikia zile kesi sugu na kuwafunga baadhi ya walanguzi wa uchumi lakini ndio kwaaanza amesema hawezi kufukua makaburi yaliyochimbwa

Pia aliahidi kusimamia uhuru wa habari na kulinda demokrasia lakini imekuwa kinyume chake kila kukicha watu wanakamatwa kwa sababu tu ya kuikosoa serikali pia amenyima uhuru wa habari kwa kufungia bunge lisiwe linarushwa live

Kwa kifupi sijaona alichokiahidi na kukitekeleza zaidi ya kupambana na upinzani hivyo basi nawataka wale makada nguli wa CCM waje walitolee ufafanuzi suala hili.
 
Mnamo tarehe 5 mwezi huu wa Novemba, mheshimiwa rais wetu mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atatimiza mwaka mmoja tokea ashike madaraka ya uongozi wa nchi yetu pendwa, Tanzania.

Katika huu mwaka, kuna mengi ambayo serikali yake imeyafanya. Mengi hayo ni pamoja na mazuri na mabaya.

Sasa, ndani ya huu mwaka wewe mwana JF una maoni gani juu ya utawala wa huyu mtukufu rais wetu?

Kama ni mtihani, utampa alama gani? A, B, C, D, E [kwa effort], au F?

Kafanikiwa yepi na kashindwa kwenye yepi?

Yepi ni mengi? Mafanikio ni mengi au kushindwa ndo kumekuwa kwingi zaidi?

Binafsi nampa alama ya E.

Nampa alama hiyo kwa jitihada zake ambazo amezionyesha katika kutaka kulirudisha taifa ndani ya mstari hususan kwenye mambo ya uadilifu, upigaji vita rushwa/ufisadi, na kadhalika.

Siwezi kumpa alama nyingine zaidi ya hiyo kwa sababu taifa lilikuwa limefikia pabaya mno kiasi kwamba hata angekuwa nani, ndani ya mwaka mmoja tu hawezi kurekebisha yote yaliyokuwa yameharibika [chini ya uongozi wa CCM].

Nadhani ni mtu mwenye nia nzuri na iliyo ya dhati kabisa katika kutaka kwake kulirudisha taifa kwenye mstari unaofaa.

Ila ndo hivyo tena. Sina hakika sana na njia, hekima, na busara zake anazozitumia katika kulifanikisha lengo hilo.

Leo anaweza kufanya jambo fulani ambalo ni zuri na la kuungwa mkono lakini kesho yake anakuja kufungua mdomo wake na kutoa kauli ambayo mtu inakuacha ukitikisa na kukuna kichwa chako na hata kubaki mdomo wazi.

Mwisho wa siku mtu unabaki kuduwaa tu na usijue hata umweke wapi, kwenye kundi gani!

Nyote mnakaribishwa kutoa tathmini zenu za huu mwaka mmoja wa utawala wa rais Magufuli.
Mihimili isiingiliane Benge,Mahakama.Serikali
 
Watanzania Wote kwa umoja wetu tunampa B
Kwa sababu mwalimu mzuri hampi wanafunzi wake 100% lasivyo mtakuwa mmetunganae mtihani
Na sisi wananchi kuna wengine hawakumpa kura Lakini anawakuna na wanampenda kimya kimya....!!
uc2pigie kula wengne tuna majib yetu moyon
 
Kuna haja ya kuendelea kuleta majibu au umeyapata mwenyewe kwa juhudi zako ?
 
Back
Top Bottom