Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Rais Magufuli: Mwaka mmoja madarakani

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,357
Reaction score
144,996
Mnamo tarehe 5 mwezi huu wa Novemba, mheshimiwa rais wetu mtukufu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atatimiza mwaka mmoja tokea ashike madaraka ya uongozi wa nchi yetu pendwa, Tanzania.

Katika huu mwaka, kuna mengi ambayo serikali yake imeyafanya. Mengi hayo ni pamoja na mazuri na mabaya.

Sasa, ndani ya huu mwaka wewe mwana JF una maoni gani juu ya utawala wa huyu mtukufu rais wetu?

Kama ni mtihani, utampa alama gani? A, B, C, D, E [kwa effort], au F?

Kafanikiwa yepi na kashindwa kwenye yepi?

Yepi ni mengi? Mafanikio ni mengi au kushindwa ndo kumekuwa kwingi zaidi?

Binafsi nampa alama ya E.

Nampa alama hiyo kwa jitihada zake ambazo amezionyesha katika kutaka kulirudisha taifa ndani ya mstari hususan kwenye mambo ya uadilifu, upigaji vita rushwa/ufisadi, na kadhalika.

Siwezi kumpa alama nyingine zaidi ya hiyo kwa sababu taifa lilikuwa limefikia pabaya mno kiasi kwamba hata angekuwa nani, ndani ya mwaka mmoja tu hawezi kurekebisha yote yaliyokuwa yameharibika [chini ya uongozi wa CCM].

Nadhani ni mtu mwenye nia nzuri na iliyo ya dhati kabisa katika kutaka kwake kulirudisha taifa kwenye mstari unaofaa.

Ila ndo hivyo tena. Sina hakika sana na njia, hekima, na busara zake anazozitumia katika kulifanikisha lengo hilo.

Leo anaweza kufanya jambo fulani ambalo ni zuri na la kuungwa mkono lakini kesho yake anakuja kufungua mdomo wake na kutoa kauli ambayo mtu inakuacha ukitikisa na kukuna kichwa chako na hata kubaki mdomo wazi.

Mwisho wa siku mtu unabaki kuduwaa tu na usijue hata umweke wapi, kwenye kundi gani!

Nyote mnakaribishwa kutoa tathmini zenu za huu mwaka mmoja wa utawala wa rais Magufuli.
 
Watanzania Wote kwa umoja wetu tunampa B
Kwa sababu mwalimu mzuri hampi wanafunzi wake 100% lasivyo mtakuwa mmetunganae mtihani
Na sisi wananchi kuna wengine hawakumpa kura Lakini anawakuna na wanampenda kimya kimya....!!
 
Kama mwanafunzi kweli kapata 100% kwa nini mwalimu ambanie?
 
Binafsi naamini tumepata mzalendo ambaye hata akikosea jambo ni ktk harakati za ustawi wa taifa letu. Changamoto kubwa aliyonayo nje ya kuleta maendeleo ambayo watanzania wanatarajia kwake ni kushughulika na wanasiasa wa chama tawala na upinzani ambào wamejengwa kwenye misingi ya ovyo na siasa za kimaslahi. Namshauri asikilize wataalamu ambao wako very well vetted ili nchi iwe kwenye direction sahihi na awe makini na ushauri wa wanasiasa WOTE!
 
Watanzania Wote kwa umoja wetu tunampa B
Kwa sababu mwalimu mzuri hampi wanafunzi wake 100% lasivyo mtakuwa mmetunganae mtihani
Na sisi wananchi kuna wengine hawakumpa kura Lakini anawakuna na wanampenda kimya kimya....!!
Usilazimishe watanzania wote kumpenda.halafu kumbuka hakuna Elimu bure.unalipa kodi.unanunua daftr kalm na mengine mengi hivo jipange tena
 
Huyu nampa Supplementary(Sup) akishindwa ku sapua anakuwa disqualified 2020
Kama hujatunga nae mtihani hawezi patia kila kitu lazima atakosa Hata kuandika,. <%&@
Ndo magufuri kafanya vizuri Lakini kasahau kuwapa wanafunzi WA diploma mikopo Kwani wao hawastahili
Yaani Haya ni makosa madogo madogo Lakini yanampunguzia maksi....!!
 
Hapa nimekumbuka ile script ya mtihani ambayo Ndalichako aliyoionyesha ya mwanafunzi aliyechora Zombie kisha akaandika "Zombi hajavaa viatu"
 
Kama hujatunga nae mtihani hawezi patia kila kitu lazima atakosa Hata kuandika,. <%&@
Ndo magufuri kafanya vizuri Lakini kasahau kuwapa wanafunzi WA diploma mikopo Kwani wao hawastahili
Yaani Haya ni makosa madogo madogo Lakini yanampunguzia maksi....!!
So unashauri arudie mtihani mana kaishia njiani halafu booklet limeisha?
 
Huyu ana F tu, ingekuwa ndo mwanafunzi wa kipindi hiki chuo angeishia kuhesabu tu maghorofa yake!
 
Back
Top Bottom