Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Najua hili suala la kumuapisha Waziri Mwigulu limejadiliwa kwa njia tofauti tofauti.
Ila naomba niliangalie kwa mtazamo wa baadae. Sina mfano wowote wa Waziri au mtumishi mkubwa wa Umma aliyepewa kiapo katika mazingira ya bar. Hata kwa mazingira tu ya kawaida, suala hili linaleta maswali ya kimaadili na kiuongozi.
Kama kuna maamuzi yoyote ya kisheria yatakayofanywa au kumshirikisha Waziri huyu, ambayo kimsingi ni yote amefanya toka ameapishwa hadi pale utakapotengua uteuzi wake au kuchukua ushauri wangu na kumuapisha upya, nachelea kusema kuwa uteuzi wake na maamuzi yote atakayofanya, au hata kushiriki tu kuyafanya, chini ya kiapo kile yanawezana kuwa ni batili.
Hakuna ubaya wa kurudia kiapo. Nakumbuka kulikuwa na hitilafu fulani katika kiapo cha Barack Obama, ikabidi arudie kiapo kile wakati mwingine kabla ya kuanza shughuli za Urais.
Kiapo siyo lazima kifanyike kukiwa na media na kutoa hotuba ila nadhani ni muhimu kukiwa na ushahidi kuwa kimefanyika kwa usahihi, hasa kwa viongozi wakubwa. Kiapo ni alama kubwa ya uhalali wa kiongozi wa umma.