Rais Magufuli, muapishe upya Waziri wako. Kuna siku mahakama itabatilisha maamuzi yake

Mkuu uyo ni wazir wa mwezi mmoja. Bunge linafungwa soon na baraza linavunjwa kisheria. Unless afanye ubabe avunje bunge bila kuvunja baraza.

Sent using Jamii Forums mobile app

Siyo kwamba mawaziri wanaendelea na nyazifa zao mpaka Siku ya uchaguzi mkuu? Nafahamu kuna kipindi Wizara inakuwa chini ya Katibu mkuu,ila sifahamu ni kipi kati ya hivi;
1) Kuanzia tarehe iliyotangazwa kuanzakampeni za uchaguzi mkuu, au
2) Kipindi cha mpito yaani baada yamatokeo ya uchaguzi kutangazwa ,na Rais mteule kuapishwa hadi atakapounda Baraza jipya la Mawaziri?
 
Wakuu embu tusikilizane,

Kwanza napenda kuwashukuru wachangiaji wote. Nadhani tunalitendea haki Jukwaa, ukiondoa mburura wachache.

Kuhusu mada husika, nitasema hivi. Kwanza sikuleta kifungu chochote cha sheria kwa sababu nilikuwa najua fika kuwa inawezekana kweli hakuna kifungu kinachosema ‘specifically’ mahali ambako kiapo kinatakiwa kufanyika.

Lakini, na hapa ndiyo maoni yangu yalipojikita, ni kuwa kiapo kisipofanyika katika utaratibu na mazingira yanayolinda sura, heshima na maadili ya kiongozi wa umma, yana athari za kupunguza au kuathiri uhalali wa kiongozi yule anayeapishwa na kama mapungufu haya yakijirudia, ina athari katika heshima ambayo jamii inawapa viongozi na watumishi wengine wa umma.

Kuna mtu amepost ibara inayogusia suala la kiapo. Ukiangalia, ile ibara haiongelei suala la mavazi anayotakiwa kuvaa anayepokea kiapo, haizungumzii kushika msahafu, haisemi umma utangaziwe pale kiongozi mteuliwa anapopewa kiapo, na ni wazi haisemi ni mahali gani kiapo kifanyike.

Kwa maana hiyo, kwa kuwa sheria haisemi hivyo kwa madai ya baadhi ya watu humu, ni kwamba ni sahihi kiongozi kwenda kupokea kiapo amevaa jezi ya Simba, kaptura na sandozi? Ni sahihi kutumia Bible App ya kwenye simu na kunyanyua simu janja badala ya msahafu wenyewe? Ni sahihi kiongozi kuapishwa bila umma kuambiwa?

Namalizia tu kusema, kuapishwa kiongozi ni kama ‘kumsimika’ na toka historia katika jamii zote, ni jambo linalotakiwa kufanyika kwa weledi na umakini. Naamini lile lililojitokeza litarekebishwa kwa njia moja ama nyingine na halitajirudia tena. Tulinde hadhi ya viongozi na watumishi wa umma. Msingi na uhalali wa serikali unategemea sana hilo.
 
Labda nyakati za vita. Na hapa hatuongelei angani au kwenye handaki, tunaongelea BAR!

Na hizo habari za ‘muzungu’ zinaingiaje?

Kumbuka siku zile corona ilikuwa imekaa vibaya mno. Cha muhimu sio sehemu ya kuapia bali mamlaka ya anayeapisha.
 
Back
Top Bottom