Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,601
Haitoshi kuogopa figisu ambazo hazijaanzishwa.Hahaha sawa mkuu. Ila naona kama vyama vya siasa vya upinzani nchi hii vinasakamwa kiasi kwamba haiwezekani kabisa kuanzisha kiwanda. Zitazuka figisu figisu na kodi za kupakazia na vikwazo na gharama na faini na hatimaye kila kitu kitashindikana. Tangu nchi hii kupata uhuru sijawahiona utawala unathubutu kuharibu shamba tena shamba la mfano wa kilimo cha kisasa kwa sababu za chuki za kisiasa kama ambavyo nimeshuhudia katika awamu hii, sembuse kiwanda.
Mimi ningeheshimu juhudi za wazi zitakazoanza, halafu serikli ilete figisu za wazi tuone.
Watanzania ni wavumilivu lakini kuna level fulani ya uvumilivu itashindwa kuvumilia.
Chama kianzishe kiwanda cha kuwapa ajira watu 500 halafu serikali ilete figisu.
Hiyo figisu tu inaweza kuwa mtaji wa kisiasa wa chama kuwa mobilize hao watu 500 kwenye vyombo vya habari kuonyesha serikali onevu inavyoua jitihada za kiuchumi za vyama kujenga viwanda nchini na kutoa ajira.
Vyama vinaweza kusema tunaitikia wito wa rais wa kuanzisha viwanda nchini, lakini tunakuwa frustrated na Draconian code.Ukiweka mambo wazi hivi wananchi wataona, hao watu 500 watasema kwenye familia zao na kwa jirani zao.
Siasa zitachukua sura ya uhalisia zaidi, kupita nadharia.
Hili halijafanyika bado.
Of course serikali ya sasa haitabiriki. Unaweza kufikiri itawabana wanasiasa, ukaona Magufuli kasema waachiwe wafanye biashara.
Ney wa Mitego alivyokamatwa na polisi waliojipendekeza kwa Magufuli, hakuna aliyetegemea Magufuli atamtetea na kumualika Ikulu.
Magufuli ni wa kumtest tu, si wa kumuogopa.
Ukiogopa umeshindwa hata kabla hujaanza. Ukitest unaweza kuzuiwa, unaweza pia usizuiwe.
Tatizo wapinzani wengi hawana uthubutu katika hili, ingawa sitaki ku sound kama naina minimize juhudi zao nyingi zenye uthubutu mwingi sana.