Rais Magufuli kakomesha upinzani

Rais Magufuli kakomesha upinzani

Hili bandiko limeandikwa vibaya
Kwanza ni kosa kudhani Magufuli hana kashfa kisiasa, kijamii na kiuchumi kashfa anazo nyingi tu. Tukiziorodhesha hapa dunia itapasuka.

Magufuli anafanya siasa peke yake! Siku wapinzani wakitoka wakaanza kufanya siasa atashangaa! Mamilioni ya watanzania vijana kwa wazee, wake kwa waume watakavyo furika kwenye mikutano ya UKAWA. SUBIRI UONE SIKU IKIFIKA!

Una msifu Magufuli? Kwa lipi hasa? Kwa kuua uchumi? Leo hii zaidi ya biashara 10,000 zimefungwa . Hii ni kwa mujibu wa TRA. Unamsifu magufuli kwa kuupendelea mkoa wake na hasa Chato? Ukitoa likizo, amesha kwenda chato kwa sababu mbalimbali mara Sita! Lakini mpaka leo hii Nyanda za juu kusini hajawahi kufika.

Unasifu Magufuli kwa kutamani kuwafilisi matajiri? Kumwacha Bashite ajinufaishe binafsi kwa kuwatisha wafanya biashara? Unamsifu kwa kuvunja KATIBA?
 
Vision ya magufuli ni ipi???naomba nisaidiwe hapo..because kama vision yake ni kujenga nchi ya viwanda then political atmosphere anayocreate isnt conducive for that....ulaya walikuwa industrilised baada ya agricultural revolution..surplus kutoka kwenye kilimo ikaleta mapinduzi ya viwanda....that was starting point yao....sasa huku kwetu kilimo katapanya...wawekezaji anawachukia...hw will he acomplish industrialisation...
 
Watanzania tunapolia kwa adha tulizosababishiwa na ccm tusiwaweké pembeni akina mkapa, mwinyi, kingunge, lowasa na sumaye na wengine nisiyo wajua. Nakili rais wa sasa kwa upande mmoja Ametupatia ugumu wa maisha tofauti na matarajio yetu, lakini kwa kujaribu kuisafisha nchi nampongeza sana kwani anachokifanya ndicho wapinzani walikuwa wanakipigia debe japo nadmshangaa tena kuona wanakipinga tena. Watanzania kinachotumaliza ni unafiki na njaa zetu.
 
Binafsi JPM namkubali kwa mengi kasoro hili la kutumia nguvu kubwa kuua UPINZANI.
 
Peoples kuweni Na akili japo kidogo basi, upinzani Ni fikra, Mbowe, Maalim Seif, Zitto nk Ni viongozi wa makundi yenye fikra zinazofanana ambayo makundi hayo yamejipa majina Kama CHADEMA, cuf, act-wazalendo nk, hata hivyo vyama vikifa leo, fikra za upinzani zitabaki hai kwa wananchi kusubiri muunganiko wenye jina jingine la kisiasa, kimsingi upinzani Ni kitu cha asili katika jamii yoyote, kinachotokea Ni kwamba upinzani hufifia au kuimarika kutegemeana Na ufanisi wa chama kinachotawala. Lakini kwa sasa ukitaka kujua ukweli afya ya upinzani ikoje, mwambie uncle Magu aruhusu mikutano, utakachokiona linganinisha Na zamani halafu ulete matokeo hapa.
Umetoa ufafanuzi mzuri sana!Pokea like ya manual!!
 
Boss Martin George Nachukia Watu Wanaoeneza Uongo. Umeandika Uongo. Ukweli Ruzuku ipo kwa Mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi.

Ni kweli Nchi inaongozwa na CCM na Serikali aka Jamhuri yake ila Si kweli Ruzuku ni ya CCM, au ni ya Serikali ya CCM. Maana CCM nayo inapata Ruzuku kwa Mujibu wa Sheria na Katiba.

Ni kweli Ruzuku inaweza kufutwa na Mh. Rais anaweza kuifuta, ni just kupeleka Mswada Bungeni na Wabunge wakapitisha Mswada huo, na Rais akau sign kuwa Sheria.

Ila Swali, Je CCM nao watakubali kukosa Ruzuku? Maana ni kama kukata mti ulioukalia.

My Take: Nia iwe kuelimishana na kufundishana na kukosoana vizuri.
Mkuu Kikarara 78 kama umeisoma sheria ya vyama vingi vya siasa utagundua kwamba kamwe huwezi kuitenganisha CCM ambacho ni chama dola na serikali. Ndomana Lowasa alipojiunga Chadema ili agombee urais aliwaeleza wazi kwamba Chadema kama chama kipambane kujipatia wabunge wengi lakini yeye kama Lowasa wamwachie jukumu la kupigania urais. Lowasa anajua wazi kwa Katiba na Sheria zilizopo ni ndoto wapinzani kushika dola, rejea hata Zanzibar ambao sheria zetu zinafanana sana, ndio maana akajaribu kukaa katikati ya CCM na chadema lakini bado haikumsaidia. Kuhusu ruzuku CCM hawahitaji Sheria wala Katiba kupata fedha kutoka serikalini kama hulielewi hata hilo basi wewe si mwanasiasa na unaweza kujiuliza kwanini CCM na chadema hawapeleki audited financial statements kwa msajili na CAG?!!!! Karibu.
 
Boss Martin George ulichoandika mwanzo na ulichoandika sasa hivi, ni vitu viwili tofauti. Kasome upya ulichoandika mwanzo Boss.

Mkuu Kikarara 78 kama umeisoma sheria ya vyama vingi vya siasa utagundua kwamba kamwe huwezi kuitenganisha CCM ambacho ni chama dola na serikali. Ndomana Lowasa alipojiunga Chadema ili agombee urais aliwaeleza wazi kwamba Chadema kama chama kipambane kujipatia wabunge wengi lakini yeye kama Lowasa wamwachie jukumu la kupigania urais. Lowasa anajua wazi kwa Katiba na Sheria zilizopo ni ndoto wapinzani kushika dola, rejea hata Zanzibar ambao sheria zetu zinafanana sana, ndio maana akajaribu kukaa katikati ya CCM na chadema lakini bado haikumsaidia. Kuhusu ruzuku CCM hawahitaji Sheria wala Katiba kupata fedha kutoka serikalini kama hulielewi hata hilo basi wewe si mwanasiasa na unaweza kujiuliza kwanini CCM na chadema hawapeleki audited financial statements kwa msajili na CAG?!!!! Karibu.
 
Ni kwa miaka mingi siasa za vyama vingi nchini zimeshuhudia upinzani wa hali ya juu baina ya CCM na chama kikuu cha upinzani kwa wakati husika. Lakini mara zote sababu kuu ya msuguano na udhaifu kwa chama tawala ukiwa ni kulaumiwa kushindwa kusimamia rasilimali za umma na kuwa na sera legelege zinazofumbia macho wabadhirifu.

Kwa zaidi ya miaka 30 sijui kama yupo anayeweza kuelezea jambo kubwa lililofanywa na vyama vya upinzani nje ya kupiga kelele dhidi ya ubadhirifu wa viongozi wa umma!

Kwa upande wa Zanzibar angalau chama cha CUF kwa kuwa kiliwahi kuwepo madarakani wao Kuna vijimambo vichache walivitenda!

Nguvu ya siasa za upinzani sio za kitaasisi, ni watu wachache ambao hawajawahi jubadilika for ages, hapa nawazungumzia kina Lowasa, Lissu, Zito, Slaa, Mbowe etc ambao Kweli wapo very strong wakiwa mmoja mmoja Lakini si kama taasisi.

Now, mkuu wa Nchi wa sasa Dr. J.P. Magufuli, yeye kwanza hafanyi makosa ya kucheka na wabadhirifu, sio legelege na wala haonekani kwenye kashfa za kijinga.

Upande mwingine kama role model, yeye anawashinda kimsimamo wanasiasa Wengi na hivyo kuiba agenda almost zote za upinzani na kuwaacha hawana cha kufanya.

Sasa watu waliokuwa wanamtaka kiongozj jemedari, mkali na jeuri asiyeogopa wawekezaji wahuni na mzalendo, Leo wamegeuka na kuitaka demokrasia, mtu akiiba akaulizwe kama anataka kuhojiwa ili tusijepoteza wawekezaji!

Alichofanya Magufuli ni kukomesha upinzani wa kichama na sasa kuwekea upinzani wa kimaslahi baina ya wabadhirifu na wanaokula Mali za umma vs wale walio waadilifu!
Ni kweli, waadilifu wenyewe ndio akina Bashite, Lugumi na the like. kalaghabaho!
 
Tatizo la upinzani hawajapata mtu kichaa anayeweza kuanzisha zali la "najitoa muhanga, liwalo na liwe".

Hata Tundu Lissu hajafika level hiyo.

Akipatikana mtu wa hivyo, akajipanga vizuri, aka raise level ya figisu iwe juu kabisa, huku chini watu wataona figisu ndogo ndogo poa tu.

Sasa hivi ukiacha upinzani, kuna CCM kibao hawampendi Magufuli. Kuna watu kibao wametumbuliwa summarily.Kuna watumishi wa serikali kibao hawapendi alivyopiga stop kupandishwa vyeo.Kuna watumishi kibao hawapendi harassment ya ujinga wa kuhakiki vyeti mara mia mia.

Upinzani hauja tap kwa hao.

Sijasikia effort ya maana kwenye hili. Upinzani ni kama unategemea Magufuli a implode tu.

Tatizo ni kwamba, hata Magufuli aki implode, watu wataona ni showmanship yake tu na hiyo ni baruti ya tafrija zake.
Tatizo lako mkuu wewe haupo hapa Bongo, unafurahia amani iliyotengenezwa na wenzio raia wa hiyo nchi. Huku bongo tunaona tukifuata huo ushauri wako kikinuka tutakosa hata nafasi ya kutafuta mkate, kutakuwa na dhiki kuu na wengine hawana pa kukimbilia. Mapungufu ya Magufuli yanavumilika kuliko adha au mateso yatokanayo na uvunjivu wa amani. Viongozi wa upinzani hakika ni wanafiki kama vile walivyo viongozi wengi serikalini lakini wapinzani wanaona hata biashara zao zitazidi kuharibiwa kama vurugu za mapigano ya ndani yataanza.
 
Tunaandaa clips za ahadi zenu mlizotoa uchaguzi uliopita. Nyie pigeni porojo kama vile na nyie ni chama cha upinzani, mtajionea wenyewe 2020.
 
Lakini tatizo la nchi hii halijawahi kuwa vyama vya upinzani. Stop that nonses already. Vyama vya upinzani havikuwepo mwaka 1970, 1975 wala 1980 na Tanzania ilikuwa nchi maskini hivi hivi kama ilivyo leo na hata zaidi. Be intelligent. Semeni ukweli uwaweke huru.. Ni nani hasa adui namba moja maendeleo ya nchi hii???? Mnamjua sana. Anaanza na herufi C.
 
Back
Top Bottom