Rais Magufuli kakomesha upinzani

Rais Magufuli kakomesha upinzani

2kimo

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,029
Reaction score
2,072
Ni kwa miaka mingi siasa za vyama vingi nchini zimeshuhudia upinzani wa hali ya juu baina ya CCM na chama kikuu cha upinzani kwa wakati husika. Lakini mara zote sababu kuu ya msuguano na udhaifu kwa chama tawala ukiwa ni kulaumiwa kushindwa kusimamia rasilimali za umma na kuwa na sera legelege zinazofumbia macho wabadhirifu.

Kwa zaidi ya miaka 30 sijui kama yupo anayeweza kuelezea jambo kubwa lililofanywa na vyama vya upinzani nje ya kupiga kelele dhidi ya ubadhirifu wa viongozi wa umma!

Kwa upande wa Zanzibar angalau chama cha CUF kwa kuwa kiliwahi kuwepo madarakani wao Kuna vijimambo vichache walivitenda!

Nguvu ya siasa za upinzani sio za kitaasisi, ni watu wachache ambao hawajawahi jubadilika for ages, hapa nawazungumzia kina Lowasa, Lissu, Zito, Slaa, Mbowe etc ambao Kweli wapo very strong wakiwa mmoja mmoja Lakini si kama taasisi.

Now, mkuu wa Nchi wa sasa Dr. J.P. Magufuli, yeye kwanza hafanyi makosa ya kucheka na wabadhirifu, sio legelege na wala haonekani kwenye kashfa za kijinga.

Upande mwingine kama role model, yeye anawashinda kimsimamo wanasiasa Wengi na hivyo kuiba agenda almost zote za upinzani na kuwaacha hawana cha kufanya.

Sasa watu waliokuwa wanamtaka kiongozj jemedari, mkali na jeuri asiyeogopa wawekezaji wahuni na mzalendo, Leo wamegeuka na kuitaka demokrasia, mtu akiiba akaulizwe kama anataka kuhojiwa ili tusijepoteza wawekezaji!

Alichofanya Magufuli ni kukomesha upinzani wa kichama na sasa kuwekea upinzani wa kimaslahi baina ya wabadhirifu na wanaokula Mali za umma vs wale walio waadilifu!
 
Huwezi kuwa na UPINZANI unaotegemea ruzuku ya serikali ya CCM kwa 100%. Hii kiinimacho Magufuli ataifutilia mbali fullstop!!
 
Not every human being fits the real definition of human being; and the number of real human beings today,if any,that number itself is not real.

Kwa nitaowakwaza kwa maneo yangu haya mtanisamehe ila mleta mada kanifanya niwaze yote haya.

Siasa za nchi mwenzenu huwa zinanifanye nifikiri sana.

Tumekuwa kama wanyama kisa siasa!!
 
Tanzania hakuna vyama vya siasa, kuna magenge ya kutafuta ulaji tu.

Si CCM wala upinzani.

Na Magufuli ni gubegube ambalo linafunga kamba vitoto mikono na kuvicharaza mpaka vitokwe damu.

Huwezi kulisifia kwamba limekomesha vitoto.

Hili jitu ni hayawani lisilona simile wala rehani.
 
Tanzania hakuna vyama vya siasa, kuna magenge ya kutafuta ulaji tu.

Si CCM wala upinzani.

Na Magufuli ni gubegube ambalo linafunga kamba vitoto mikono na kuvicharaza mpakavitokwe damu.

Huwezi kulisifia kwamba limekomesha vitoto.

Hilijitu ni hayawani lisilona simile wala rehani.

Duh!Unahasira
 
Hapana.

Akili kubwa ikipiga chafya tu, akili ndogo lazima ione hasira.

Tatizo tunaongozwa na waliofeli shule wakarudia kama mara mia hivi ndipo baada ya kufaulu wanajiona wanaakili kumbe hamna kitu.Wengine na mitihani wamekwiba kwa maana hata vyeti si vyao basi wanajiona wasomi,sasa ona wanavyotenda hata msomi wa chekechea hawezi kutenda hivyo.Anyway ndiyo Afrika
 
Upinzani uliojengwa kwa utapeli,uhalifu...usaliti na kutumika hauwezi kusurvive kipindi hiki cha Magufuli

Hii ndio raha ya demokrasia sasa, ccm mnakuja na vibwagizo vyenu na mnatamba mnavyotaka. Shida sasa ni pale wapinzani wanapomwaga mitazamo yao mara utasikia mmekosa nidhamu, mara wachochezi nk. Mmefikia mahali mnawapoteza watu wanaosema ukweli. Siasa raha yake utambe ukubali na wengine watambe.
 
Kwani upinzani ni maadui. .... kuna mengi ya kufanya. ....
 
Hii ndio raha ya demokrasia sasa, ccm mnakuja na vibwagizo vyenu na mnatamba mnavyotaka. Shida sasa ni pale wapinzani wanapomwaga mitazamo yao mara utasikia mmekosa nidhamu, mara wachochezi nk. Mmefikia mahali mnawapoteza watu wanaosema ukweli. Siasa raha yake utambe ukubali na wengine watambe.

Hao wamezoea kukwapua,hata huyo wa sasa nao ni wale wale,wanatafuta njia tu hakuna UZALENDO wala ubepari walaji wote tu
 
Back
Top Bottom