Rais Magufuli: Hata kama umekula hela si unyamaze!!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,238
103,910
"Mtu anasimama,anatoka mapovu,unaweza kujiuliza uzalendo wake uko wapi?,hata kama umekula hela si unyamaze".......John Pombe Magufuli, October 23, 2017

Swali
Ukitofautiana na rais sio mzalendo? Lakini kina Zitto wakati wanapambana na mikataba ya Buzwagi,Rais wakati huo alikuwa wapi. Tuseme alilipwa fedha na wawekezaji kunyamaza? Tuvumiliane tubishane kwa hoja na majibu ya nidhamu. Raia kuwaambia wengine wanatoa mapovu sio ustaarabu

Sasa kama ana ushahidi wa mtu kula pesa kwanini asimkamate badala ya kuropoka ropoka?

Because you can't take us out of our lovely country,you may choose to take the country out of us
 
"Mtu anasimama,anatoka mapovu,unaweza kujiuliza uzalendo wake uko wapi?,hata kama umekula hela si unyamaze".......John Pombe Magufuli, October 23, 2017

Swali
Ukitofautiana na Rais sio mzalendo?
Hoja ni kula pesa na kutupigia kelele...kwa data za uongo.

Kosoa kwa facts sio kupotosha umma kwa maslahi ya Tumbo lako.

Kumbuka huyu huyu kibaraka ndiye aliyetaka Rais kutangaza baa la njaa kwa data zake za kughushi.

Akiachwa ataendelea...ifike mahala siasa ya uongo uongo ife kabisa nchini.

SWALI KWA MLETA MADA....JE ZITTO ALIVYOITWA MSALITI NA MBOWE ILIMAANISHA MBOWE HAKOSOLEWI??
 
"Mtu anasimama,anatoka mapovu,unaweza kujiuliza uzalendo wake uko wapi?,hata kama umekula hela si unyamaze".......John Pombe Magufuli, October 23, 2017

Swali
Ukitofautiana na rais sio mzalendo?
Kwa kweli haya ni maajabu ya rais wetu wa sasa ukitofautiana naye tu unakuwa msaliti, sio mzalendo, umehongwa, duh safari hii tumepata rais untouchable.
 
Ndiyo, huo siyo uzalendo tena in uovu unaoweza kuhatarisha maisha yako. Yaani, wewe unaitwa msaliti na kama inavyokuwaga vitani (wanajeshi wanajua), ndivyo ilivyo kwenye vita vya kiuchumi. Huwezi kuwa msaliti halaf ukaachwa usavaivu tu. ....No, not to that extent!

Tumelikoroga wenyewe! Ni lazima tulinywe!
 
Watu wamekula hela (rushwa) na hawajafikishwa mahakamani.

Ana ushahidi wote wa wizi wa dhahabu lakini kakubali kuchukua chini ya 1% anachodai na anajisifu.

Tukihoji uhalali wa madai ya wizi au ripoti za kupika tunaitwa wasaliti.

Tumerudi enzi za Nyerere. Mwenye mawazo ya kizalendo ni mmoja tu.

Jinsi utakavyopaza sauti ya "Ndiyo Mzee" ndiyo utatunukiwa cheyo.

Kama anafanya kila kitu sawa asiogope kuhojiwa. Watu watatofautisha pumba na mchele.
 
"Mtu anasimama,anatoka mapovu,unaweza kujiuliza uzalendo wake uko wapi?,hata kama umekula hela si unyamaze".......John Pombe Magufuli, October 23, 2017

Swali
Ukitofautiana na rais sio mzalendo?
Yeye mbona kala mahela kibao na nyingine akahonga mahawara zake alipouza nyumba za serikali. Leo ndio anataka kutudanganya kuwa yeye ni mzalendo sana.
 
Hii nchi sasa inakwenda kubaya..

Lazima nchi yote tuimbe na kumsifu Mkulu kwa kila afanyalo!

Yeyote anayekwenda kinyume, atabatizwa majina ya msaliti, siyo mzalendo na umenunuliwa na hao wezi wetu!
 
Hoja ni kula pesa na kutupigia kelele...kwa data za uongo.

Kosoa kwa facts sio kupotosha umma kwa maslahi ya Tumbo lako.

Kumbuka huyu huyu kibaraka ndiye aliyetaka Rais kutangaza baa la njaa kwa data zake za kughushi.

Akiachwa ataendelea...ifike mahala siasa ya uongo uongo ife kabisa nchini
Kipindi kile alichokuwa anasema Nchi inanyemelewa na njaa ilikuwa kweli mfano mdogo ni sisi mkoa wa Mbeya hatujawahi kununua debe la mahindi tshs20000/= mpaka25000/= lakini mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu hali ilikuwa hivyo
 
Ina maana wote tunaopingana naye tumekula pesa, Msekwa amekula ngapi, Wassira amekula ngapi hata Kikwete naye kahongwa, this is too much sasa.
Niwekee ukosoaji wa Msekwa,Wassira,au Kikwete tuone kama kuna ukosoaji au upotoshaji wa data....usiniletee udaku wa Mange please.

Niwekee Taarifa zinazoonesha hao uliowataja kumkosoa Magufuli.

Jifunzeni kuandika kweli tupu
 
Magufuli ulipokuwa unapiga makofi kupongeza na kugonga meza kwa ushabiki wakati mkipitisha kuunga mkono kule bungeni, huu ushenzi unao"jifanya " kuuchukia leo, jee ULIKUWA UMERAMBISHWA pesa na BWANA yupi?
Magufuli huna jipya
Well said, yaani watu wanapitisha wenyewe vifungu na sera mbovu.wakija kuona inawabana wakiwa nje wanaanza kupiga kelele, na wasiwasi na huyu mtu huenda alikuwa analala akisikia meza zinagongwa nae anafuata upepo
 
Sasa kama ana ushahidi wa mtu kula pesa kwanini asimkamate badala ya kuropoka ropoka? Kwenye boti uozo na pangaboi yeye kala pesa kiasi gani?
Akikamatwa mtasema ananyanyasa wapinzani!!vigeu geu sana ninyi
 
Niwekee ukosoaji wa Msekwa,Wassira,au Kikwete tuone kama kuna ukosoaji au upotoshaji wa data....usiniletee udaku wa Mange please.

Niwekee Taarifa zinazoonesha hao uliowataja kumkosoa Magufuli.

Jifunzeni kuandika kweli tupu
Upinzani sio uadui, Kikwete.
 
Back
Top Bottom