Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Gambo sikumfukuza Ukuu wa Mkoa bali aliniomba akagombee Ubunge baada ya kuona Arusha inakwama

Ukwaju ebu pitia pande hii please....
Mkuu mm hili Jukwaa siliwezi, kwani kule kwetu bado?
hiyo 28 ifike maana baada ya uchaguzi kuna maisha, hata 2025 tunaiombea tuwe hai
1603464425060.png

1603464197806.png
 
1. Elimu iongezeke, hususan elimu ya uraia kwa watu wengi zaidi. Mtaji wa CCM ni ujinga wa Watanzania wengi.

2.Watu waache utamaduni wa "hewala, hewala". Hata ukiwa na elimu, ukiwa mwoga hutaweza kuuondoa mfumo dhalimu.

3.Wanaotaka mabadiliko wamaanishe hilo kwa kweli. Wao wenyewe waanze kuishi kwa utamaduni wa kidemokrasia na kupenda mawazo mbadala. Siyo mtu analalamikia udhalimu wa CCM isivyo na demokrasia, wakati nyumbani yeye baba akishasema jambo halina mjadala. Au chama cha upinzani anakiendesha kama familia yake binafsi.

4. Vyama vya upinzani viache kuwa vyama vya msimu wa uchaguzi.Nimeshangaa sana upinzani umekubali kunyamazishwa na Magufuli miaka yote hii.Hususan katazo la kufanya mikutano ya hadhara ambalo liko kinyume na katiba. Kama wapinzani wameshindwa kupinga hili, nawaona bado sana hawajajizatiti kuiondoa CCM.

5. Tuandae watoto na vijana wanaokua sasa kukua katika utamaduni wa kuukata ujinga bila tahayari.Kwa sasa naona kama na wao tayari wanaondolewa kutoka kwenye "kizazi cha kuhoji" na kupelekwa kwenye "kizazi cha hewala hewala".

6. Vyama vya upinzani vijizatiti zaidi kimataifa kuchukua uzoefu sehemu nyingine na kutengeneza urafiki na network kubwa za kimataifa zitakazosaidia kuleta maendeleo chanya bila kuleta hofu ya siasa zetu kutawaliwa na watu wa nje. Kuna mitandao inayojulikana na kuheshimika kama vile Amnesty International, The Committee To Protect Journalists, Human Rights Watch etc inafanya kazi kubwa na nzuri kumulika serikali dhalimu, lakini sioni kama wapinzani wetu wanazitumia hizi taasisi vizuri.

7. Vyama vya upinzani bado sana havijatumia mitandao ya kijamii kujitangaza. Presence ya chama kama CHADEMA Youtube, Twitter, au hata JF ni ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa chama. Mitandao inasaidia sana kupasha habari watu wengi kwa wakati mfupi sana. Upinzani bado unacheza kwenye hili.

8.Vyama vya upinzani vinatakiwa kuonesha mifano ya shughuli za kiuchumi. Sio kupiga siasa za midomo tu.Yako wapi mashamba ya vyama vya upinzani? Yako wapi maduka yao? Iko wapi miradi ya kusaidia ajira kwa vijana? Wapinzani wakianzisha vitu hivi, humo humo kwenye miradi kuna nafasi ya kuongeza wanachama na kutanua wigo wa kueneza sera kwa wananchi, tena kwa kuonesha mifano, si maneno tu.Waswahili wanasema "Maneno matupu hayavunji mfupa". Waingereza wanasema "Action speaks louder than words".

9. Wapinzani wanatakiwa kuwashawishi watumishi wa umma, hususan vyombo vya dola, kwamba wao hawana ugomvi nao, wanataka kuitoa serikali ya CCM tu. Vyombo vya dola vinatakiwa kufanya kazi pamoja na wapinzani, si kudhibiti wapinzani. Vikidhibiti wapinzani ushahidi uchukuliwe na washitakiwe.

10.Vuyama vya upinzani vijizatiti zaidi kupanga mkakati wa kisheria kuhakikisha haviibiwi kura. Hii ni pamoja na mabadiliko ya katiba, kuongeza teknolojia, kuongeza waangalizi wanaoheshimika kutoka nje, na kuongeza kujitambua miongoni mwa wananchi.

Kuna mengi sana, ila kwa leo niishie hapa.
Shukrani mkuu
 
Sasa Rais amesema hakumfukuza na yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuajiri na kutengua. Sasa wewe unabisha nini sasa?
Kwahiyo akisema ndiyo ichukuliwe ndio ukweli?Mbona mwanzo alisema amemuondoa pamoja na wenzake kwasababu alichowatuma hawakwenda kukifanya wakakalia malumbano?Au mpaka uwekewe clip hapa akiyasema hayo?
Msiwe wapumbav kiasi hicho!
 
Yes, it is clear kwamba hakumfukuza - Gambo aliomba ili ashiriki uchaguzi wa kura za maoni - wanaAtown tumchague Mrisho Gambo akamsaidie JPM kupaisha nchi yetu
Duuh,wewe hata JPM akija akakuambia jinsia yako siyo hiyo uliyonayo utamwamini!!
Mtoto mjinga ni mzigo kwa mama yake!
 
Rais Magufuli amesema kuna watu wanadai anamchukia Mrisho Gambo na kwamba alimfukuza kazi ya mkuu wa mkoa wa Arusha lakini hiyo siyo kweli.

Gambo alinifata akaniomba agombee ubunge ili aiokoe Arusha ambayo inaonekana kukwama, amesema Dr Magufuli.
Ningekuwa namchukia ningempitisha kugombea ubunge? ameuliza.

Nileteeni Mrisho Gambo kwa ajili ya maendeleo ya Arusha amesisitiza Dkt. Magufuli.







Maendeleo hayana vyama!
Ni wajinga pekee wanaosikia ukweli,wanaona ukweli lakini Bado wanaamini uongo...shame on him asee Ni uchafu ndani ya takataka
 
Kwahiyo akisema ndiyo ichukuliwe ndio ukweli?Mbona mwanzo alisema amemuondoa pamoja na wenzake kwasababu alichowatuma hawakwenda kukifanya wakakalia malumbano?Au mpaka uwekewe clip hapa akiyasema hayo?
Msiwe wapumbav kiasi hicho!
Tukuamini wewe au Rais aliyesema au? Nenda zako na uelewa wako!
 
Asee sio huko niaje ni wakuzid arfu Yani Jana mnaambiwa 1+1=2,kesho 1+1=3 tumieni bhasi hta akili ya kuvukia road nyie mataga acheni kuburuzwa asee
Hapo umeonyesha uelewa wako wa hesabu na siasa ni zero kabisa!!
 
Back
Top Bottom