Uchaguzi 2020 Rais Magufuli: Gambo sikumfukuza Ukuu wa Mkoa bali aliniomba akagombee Ubunge baada ya kuona Arusha inakwama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Rais Magufuli amesema kuna watu wanadai anamchukia Mrisho Gambo na kwamba alimfukuza kazi ya mkuu wa mkoa wa Arusha lakini hiyo siyo kweli.

Gambo alinifata akaniomba agombee ubunge ili aiokoe Arusha ambayo inaonekana kukwama, amesema Dr Magufuli.
Ningekuwa namchukia ningempitisha kugombea ubunge? ameuliza.

Nileteeni Mrisho Gambo kwa ajili ya maendeleo ya Arusha amesisitiza Dkt. Magufuli.







Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi mbunge na mkuu wa mkoa nani ana nafasi nzuri ya kuleta au kushawishi maendeleo? Mbunge ana kazi gani? Hivi kweli wabunge hawa watakumbuka kuisimamia serikali au watakuwa vikaragosi vya serikali. Mola atunusuru bungeni kuwe na mchanganyiko mzuri wa wabunge ama sivyo itakuwa shida tupu.
 
Kwa hiyo Magufuli ndiye mjumbe mkuu wa kupitisha na kukata watu?

Na kama kumpitisha mtu ni kutomchukia, kutompitisha ni kumchukia?

Maana katika kujibu swali hili kazua swali jingine.

Wale ambao hajawapitisha kama kina Bashite na Adadi Rajabu, tena kwa Adadi Rajabu alikuwa incumbent, hao anawachukia?
 
Kwa hiyo anatuaminisha kuwa kauli zake zoote alizowahi toa ni uwongo? tuanze kujikumbusha moja baada ya nyingine:

1. Mimi ni Rais wa vyamaa vyoote na sibagui chama chochote- Kumbe uwongo
2. Mwanangu pia nae alipata Corona - Kumbe Uwongo
3. Nchi yetu ni tajirii, we are supposed to be a donor country - Uwongo Mtupu
4. Nimeguswa saana na shambulio alilofanyiwa Lissu - Uwongo mtupu
5.
 
Muongo sana huyu mzee halafu msahaulifu.
20201023_132450.jpg
20201023_132447.jpg
 
Kama Mrisho Gambo atanyimwa kura na watu wa Arusha anapaswa kumlaumu Magufuli.

Kama kuna mtu anadhani Magufuli amemfanyia kampeni Gambo ukweli ni kwamba amemuharibia na wananchi wataamini hawa wote wawili ni waongo na matapeli watupu.

Lema anakwenda kuwamaliza na clip za nyuma halafu atawawekea hii ya leo, kura zitakapopigwa mtakumbuka maandishi yangu.

Huyu mzee sijui ana matatizo gani huwa sielewi kabisa.
 
Back
Top Bottom