Uchaguzi 2020 Gambo auweka rehani Ubunge Arusha mjini kwa wazee

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema anawasubiri wazee wampe ridhaa kugombea Ubunge Arusha Mjini

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa hana Mpango wa kugombea Ubunge, tofauti na ambavyo imekuwa ikidhaniwa na baadhi ya Watu wakiwemo Wanasiasa wa Mkoa wa Arusha.

Gambo amesema kazi ya kuleta maendeleo anayoifanya katika Mkoa wa Arusha, ni katika Utekelezaji wa kawaida wa majukumu aliyopewa na Mamlaka yake ya Uteuzi, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo amesema hatapuuza maombi ya Wazee, kama watamuomba kugombea Ubunge.

pic%2Bgambo.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arusha ilishakuwa na maendeleo tangu zamani, sasa ni uboreshaji tu. Sasa asiji fanye yeye ndiye anaeleta maendeleo muda huu. Pia kuwa mkuu wa mkoa sio sifa ya kuwa mbunge, kwani ubunge na ukuu wa mkoa ni vitu viwili tofauti.
Ubunge ni uongozi na ukuu wa mkoa ni utawala.
 
Sasa hivyo si ndio njia yao ya kusema anataka kugombea, labda kama unayeandika ni mgeni wa siasa.
 
Magufuli alisha watahadharisha, kuhusu tamaa ya vyeo, una nafasi hii unataka kugombea na ile, alishasema ukikosa imekula kwako
 
Ni mtanzania. Ana haki ya kugombea popote. Apime kama anakubalika. La sivyo atakosa vyote.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema anawasubiri wazee wampe ridhaa kugombea Ubunge Arusha Mjini

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa hana Mpango wa kugombea Ubunge, tofauti na ambavyo imekuwa ikidhaniwa na baadhi ya Watu wakiwemo Wanasiasa wa Mkoa wa Arusha.

Gambo amesema kazi ya kuleta maendeleo anayoifanya katika Mkoa wa Arusha, ni katika Utekelezaji wa kawaida wa majukumu aliyopewa na Mamlaka yake ya Uteuzi, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo amesema hatapuuza maombi ya Wazee, kama watamuomba kugombea Ubunge.

View attachment 1325060

Sent using Jamii Forums mobile app
Maendeleo gani ataleta mbona Tanzania ina kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Monaban alishindwa yeye ataweza.au anadhani kwa kuwa aliteuliwa na rais basi na wanaArusha watamkubali.Halafu gambo ni vema anveendelea na ukuu wa mkoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema anawasubiri wazee wampe ridhaa kugombea Ubunge Arusha Mjini

Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa hana Mpango wa kugombea Ubunge, tofauti na ambavyo imekuwa ikidhaniwa na baadhi ya Watu wakiwemo Wanasiasa wa Mkoa wa Arusha.

Gambo amesema kazi ya kuleta maendeleo anayoifanya katika Mkoa wa Arusha, ni katika Utekelezaji wa kawaida wa majukumu aliyopewa na Mamlaka yake ya Uteuzi, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo amesema hatapuuza maombi ya Wazee, kama watamuomba kugombea Ubunge.

View attachment 1325060

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee Mangula msikilize huyo, anataka uongee.

Tume ya Uchaguzi mmesikia?

Takukuru kamateni rungu lenu, kuna mtu anafanya yake huko.
 
Back
Top Bottom