Rais Magufuli awaapisha Wakuu wa Mikoa, Awaongelea Kasesela na aliyepigwa fimbo na Ndugai

1467209680546.jpg
 
Saafi sana Rais kipenzi cha Watanzania.




Watanzania wapo karibu milioni 50,kumwita aliyechaguliwa na watu milioni 8 kuwa ni kipenzi cha Watanzania nayo yaweza kuwa "ishara ya msalaba" yenye kuashiria mwanzo wa Sala za "Ritania ya watakatifu".Endelea kumsifu na kumwabudu ana uwezo wa kutengua uteuzi wa yeyote akakupa nafasi wewe.
 
Watanzania wapo karibu milioni 50,kumwita aliyechaguliwa na watu milioni 8 kuwa ni kipenzi cha Watanzania nayo yaweza kuwa "ishara ya msalaba" yenye kuashiria mwanzo wa Sala za "Ritania ya watakatifu".Endelea kumsifu na kumwabudu ana uwezo wa kutengua uteuzi wa yeyote akakupa nafasi wewe.
Muda mwingine walau uwe unaanza kujihoji kabla ya kupost hata swali moja tu kuwa "hivi muda huu ni saa ngapi?"
Ni kweli Tanzania kwa sasa tunakaribia Million 50...LAKINI UKWELI UNAOSHINDWA KUUSEMA AIDHA KWA MAKUSUDI AU KWA NIA YA KUPOTOSHA NI KUWA KATI YA HAO NI MILKION 24 TU NDIO WENYE SIFA ZA KUPIGA KURA KWA MWAKA JANA (Sifa tofautitofaut labda umri nk)
Na katika hao million 24 waliopiga kura ni zaidi ya Million 23
HIVI KATIKA HILO PIA LINAHITAJI SIASA KWELI??? Au ulitaka na watoto wa miaka 10-17 na wenyewe wapige kura SIMPLY KUKUFURAHISHA WEWE KWA NAMBA ETI????
Ni vizuri sana kukosoa LAKIN NI VIZURI ZAID ANAYE KOSOA KWA HOJA ZENYE MASHIKO NA KWA LENGO LA KUSAIDIA SIYO ILI NA WW UONEKANE UMEPOST KITU JF
Hata ukiwa wa kusoma post za wengine bado UTAITWA MTANZANIA (Kama ni raia kweli)
 
Leo Tarehe 29 Rais Magufuli anawapisha wakuu wa mikoa na wilaya asubuhi hii live from Azam two na TBC1.

Rais Magufuli:
Gondwe ninajua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu.

Rais Magufuli:
Mchakato wa kuwapata Ma-DC haukuwa rahisi, ilibidi tutizame historia ya kila mmoja wao.

Rais Magufuli:
Kuna mabadiliko madogo tuliyoyafanya kutokana na jina lilikosewa, kwa hiyo aliyestahili tumeshamuweka.

Rais Magufuli:
Ningeweza nikataja majina yote mliopo hapa mpaka yule aliyepigwa fimbo na mtani wangu, karibu kila jina nalifahamu na sifa yake.

Rais Magufuli:
Mna mamlaka makubwa ya kumuweka mtu Mahabusu ila msiende tu kuonea watu.

Rais Magufuli:
Mnaweza kufikiri tumewachagua sisi lakini inawezekana Mungu ametutumia sisi kuwachagua ninyi.

Rais Magufuli:
Nilikuwa namuona DC wa Iringa anabeba watoto wakamsema sana, na mimi nikasema abaki hapa hapa

Rais Magufuli:
Nilitegemea sana baada ya kuwateua, nilitegemea labda mngekuja robo tu, ninawashukuru sana kwa kuja.

Rais Magufuli:
Watanzania wengi tumezoea kulalamika, tunapenda tu kupewa, hatutaki kufanya kazi.

Rais Magufuli:
Ni matumaini yangu hamtaniangusha, hata sura zenu zinaonyesha ni wachapa kazi, nendeni mkachape kazi.

Rais Magufuli:
Nyinyi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mna mamlaka hata ya kuweka watu mahabusu, ila msiende kuonea watu.

Rais Magufuli: Mkasimamie yale tuliyowaahidi sisi wana CCM, mkayatekeleze kwa nguvu zote

Rais Magufuli:
Watanzania wengi wana changamoto nyingi, nina imani hamtaiangusha serikali hii.

Rais Magufuli:
Nataka niseme ukweli, wale ma-DC tuliowaacha hawakufikia vigezo

Mchakato wa kuwapata ma-DC ulikuwa mgumu, ilibidi tuangalie historia ya kila mmoja, tuliangalia mambo mengi sana.

Rais Magufuli anazungumza kwenye sherehe za kuwaapisha kiapo cha uadilifu wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapya.
Kama rais anasema kuteua ma-DC haikuwa kazi rahisi halafu anamteua ABDALLAH NJWAYO kuwa DC. Nipoteza imani na JPM kaisa. CCM ni ile ile
 
Vyeo vya kupeana kikada,ukada ndio sifa kuu na wala si weledi!Ona baada ya polepole kupiga mayowe sana kumponda lowassa ndio akaonekana ni kada mtiifu!
 
Back
Top Bottom