Hivi Wakuu wa Mikoa Wabunge na mfumo rasmi wa serikali umeshindwa kabisa kutatua matatizo ya wananchi mpaka aje Makonda mwenezi. Kuna kasoro

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,461
1,445
Mimi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kinachoendelea kuhusu ziara za Makonda mikoani, na zoezi la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kimsingi hali inafikirisha sana, na hapa Mwanasheria Mkuu wa serikali ameliona hili. Tuna wakuu wa Wilaya,wakuu wa mikoa , wabunge Takukuru nk wote kweli wameshindwa kutatua kero mpaka Makonda aje huko. Hii ni aibu kwa serikali. kiukweli wana mwangusha Rais kiaina.Mwenezi hawezi kumaliza kero zote zaidi ni asilimia 0.1 %ya kero zilizopo kwenye jamii.Njia nzuri ni kila mtendaji aliyeteuliwa na Rais atimize wajibu wake au mifumo rasmi itumike.vinginevyo watamchukia bure Makonda kuwa anawafitinisha lakini utaratibu anaotumia utachokwa na yeye mwenyewe atachoka tu na hapo wananchi watazidi kuichukia serikali yao. utataribu huu ni temporary tu kisiasa.
 
Hizo kero zinaundwa tu wakati Makonda anakaribia kufika, kwa maana nyingine ni maigizo amini usiamini, na akiondoka kila kitu ubaki hapohapo.
 
Mimi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kinachoendelea kuhusu ziara za Makonda mikoani, na zoezi la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kimsingi hali inafikirisha sana, na hapa Mwanasheria Mkuu wa serikali ameliona hili. Tuna wakuu wa Wilaya,wakuu wa mikoa , wabunge Takukuru nk wote kweli wameshindwa kutatua kero mpaka Makonda aje huko. Hii ni aibu kwa serikali. kiukweli wana mwangusha Rais kiaina.Mwenezi hawezi kumaliza kero zote zaidi ni asilimia 0.1 %ya kero zilizopo kwenye jamii.Njia nzuri ni kila mtendaji aliyeteuliwa na Rais atimize wajibu wake au mifumo rasmi itumike.vinginevyo watamchukia bure Makonda kuwa anawafitinisha lakini utaratibu anaotumia utachokwa na yeye mwenyewe atachoka tu na hapo wananchi watazidi kuichukia serikali yao. utataribu huu ni temporary tu kisiasa.
They create PROBLEM in one hand,..and solve with another hand,..that is government.
 
Kwani Makonda mwenyewe anatatua matatizo ya wananchi?

Ni scripts za drama na comedy ziimeandaliwa mzee baba. Hivi unadhani hao mawaziri anaowapigoa simu anawashitukiza?

Kalagha baho!!
 
Back
Top Bottom