Rais Magufuli awaapisha Wakuu wa Mikoa, Awaongelea Kasesela na aliyepigwa fimbo na Ndugai

Hongereni sana mliopata uteuzi, mkachape kazi kwa mwendo kasi na ufanisi mungu awabariki wote
 
Unaguna nini? kigeu geu cha hawa kimekuchefua?

13233029_1590768097881921_7440964151336377693_n-jpg.360620
Hatari sana hii. Wataandamana.
 
Amewataka wakamtangulize Mungu wao katika kazi zao.
Amewataka wakasimamie suala la Uadilifu, haki na ukweli.
Amewaagiza wasiwe wabaguzi katika kazi zao. Wakawahudumie wananchi wote bila kujali imani zao za dini, itikadi ya vyama, makabila na jinsia.
Amewaagiza kwenda kukemea rushwa, kutokula rushwa na kusimamia kwa ukamilifu mapato ya serikali.
Ameagiza wakasimamie kwa ukamilifu Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa sababu ndiyo wananchi waliipigia kura kwa wingi.

VIDEO:

10..jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam
1111.jpg

Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wateule wakila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam
88.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakuu wapya wa Wilaya mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya watatu wa Mkoa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu kutoka kushoto, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakwanza kushoto.​
 
Leo Tarehe 29 Rais Magufuli anawapisha wakuu wa mikoa na wilaya asubuhi hii live from Azam two na TBC1.

Rais Magufuli: Ningeweza nikataja majina yote mliopo hapa mpaka yule aliyepigwa fimbo na mtani wangu, karibu kila jina nalifahamu na sifa yake.

Hivi hilo sio kosa la jinai? Zamani wakati tupo hai, ukifanya jinai hustahili kuwa kiongozi.
 
]
Rais Magufuli:[/B] Nyinyi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mna mamlaka hata ya kuweka watu mahabusu, ila msiende kuonea watu.
.

Kwanini anapenda sana kukumbushia hapo? Ina maana kati mamlaka yote waliyonayo hao wateule hili ndiyo jambo tarajiwa sana?
 
.....aisee huyo ndugu aliyepewa ukuu wa wilaya bahati mbaya kwa jina la mwingine kukosewa!, yaani keshapewa pongezi na ndugu,jamaa na marafiki halafu mnafanya mambo gani tena aisee!!, siku nyingine kuweni makini bana.. tena makini sana!
 
Hivi si ninasikia kuwa ajira mpya zimesitishwa serikalini au hizi za wakuu wa wilaya na mikoa ni nini?
 
Unaguna nini? kigeu geu cha hawa kimekuchefua?

13233029_1590768097881921_7440964151336377693_n-jpg.360620
MKUU UTAKOSANA NA WATU,MM KILA NIKICHANGIA NIKIWAKOSOA TU NAMBIWA NATAKA UKUU WA MKOA YETU MACHO DR SLAA KAIBUKA TENA ANASEMA MBINU YA VYAMA VYA UPINZANI YA KUKIMBIA BUNGE NA KUSUSIA VIKAO VYA BUNGE HAITAVISAIDIA KAMA HAVIWEZI KUIBUA HOJA NZITO.NAPITA TU NITAREJEA BAADAYE
 
Katika mamlaka waliyokuwa nayo yote aliloliona la muhimu kulitaja ni la kuweka watu ndani! Kweli huyu ni dikteta.

Leo Tarehe 29 Rais Magufuli anawapisha wakuu wa mikoa na wilaya asubuhi hii live from Azam two na TBC1.

Rais Magufuli:
Gondwe ninajua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu.

Rais Magufuli:
Mchakato wa kuwapata Ma-DC haukuwa rahisi, ilibidi tutizame historia ya kila mmoja wao.

Rais Magufuli:
Kuna mabadiliko madogo tuliyoyafanya kutokana na jina lilikosewa, kwa hiyo aliyestahili tumeshamuweka.

Rais Magufuli:
Ningeweza nikataja majina yote mliopo hapa mpaka yule aliyepigwa fimbo na mtani wangu, karibu kila jina nalifahamu na sifa yake.

Rais Magufuli: Mna mamlaka makubwa ya kumuweka mtu Mahabusu ila msiende tu kuonea watu.

Rais Magufuli:
Mnaweza kufikiri tumewachagua sisi lakini inawezekana Mungu ametutumia sisi kuwachagua ninyi.

Rais Magufuli:
Nilikuwa namuona DC wa Iringa anabeba watoto wakamsema sana, na mimi nikasema abaki hapa hapa

Rais Magufuli:
Nilitegemea sana baada ya kuwateua, nilitegemea labda mngekuja robo tu, ninawashukuru sana kwa kuja.

Rais Magufuli:
Watanzania wengi tumezoea kulalamika, tunapenda tu kupewa, hatutaki kufanya kazi.

Rais Magufuli:
Ni matumaini yangu hamtaniangusha, hata sura zenu zinaonyesha ni wachapa kazi, nendeni mkachape kazi.

Rais Magufuli:
Nyinyi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mna mamlaka hata ya kuweka watu mahabusu, ila msiende kuonea watu.

Rais Magufuli: Mkasimamie yale tuliyowaahidi sisi wana CCM, mkayatekeleze kwa nguvu zote

Rais Magufuli:
Watanzania wengi wana changamoto nyingi, nina imani hamtaiangusha serikali hii.

Rais Magufuli:
Nataka niseme ukweli, wale ma-DC tuliowaacha hawakufikia vigezo

Mchakato wa kuwapata ma-DC ulikuwa mgumu, ilibidi tuangalie historia ya kila mmoja, tuliangalia mambo mengi sana.

Rais Magufuli anazungumza kwenye sherehe za kuwaapisha kiapo cha uadilifu wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapya.
 
Back
Top Bottom