Rais Magufuli awaapisha Wakuu wa Mikoa, Awaongelea Kasesela na aliyepigwa fimbo na Ndugai

Sahihisho, Rais anawaapisha wakuu wa Mikoa tu na Wakuu wa Wilaya wataapishwa na wakuu wao wa Mikoa
"Nataka niseme ukweli, wale ma-DC tuliowaacha hawakufikia VIGEZO." - JPM

Mkuu kubali tu kuwa hukuwa na VIGEZO. Endelea kuuza t-shirt Lumumba & kumtukana Lowasa. Ndivyo unavyoviweza.
 
Kumbe JPM ni mwana jf mwenzetu maana jana kuna uzi uliletwa kuhusu huyo jamaa aliyepigwa na Ndugai kuteuliwa kuwa DS wa Meatu.
 
Leo Tarehe 29 Rais Magufuli anawapisha wakuu wa mikoa na wilaya asubuhi hii live from Azam two na TBC1.

Rais Magufuli:
Gondwe ninajua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu.

Rais Magufuli:
Mchakato wa kuwapata Ma-DC haukuwa rahisi, ilibidi tutizame historia ya kila mmoja wao.

Rais Magufuli:
Kuna mabadiliko madogo tuliyoyafanya kutokana na jina lilikosewa, kwa hiyo aliyestahili tumeshamuweka.

Rais Magufuli:
Ningeweza nikataja majina yote mliopo hapa mpaka yule aliyepigwa fimbo na mtani wangu, karibu kila jina nalifahamu na sifa yake.

Rais Magufuli:
Mna mamlaka makubwa ya kumuweka mtu Mahabusu ila msiende tu kuonea watu.

Rais Magufuli:
Mnaweza kufikiri tumewachagua sisi lakini inawezekana Mungu ametutumia sisi kuwachagua ninyi.

Rais Magufuli:
Nilikuwa namuona DC wa Iringa anabeba watoto wakamsema sana, na mimi nikasema abaki hapa hapa

Rais Magufuli:
Nilitegemea sana baada ya kuwateua, nilitegemea labda mngekuja robo tu, ninawashukuru sana kwa kuja.

Rais Magufuli:
Watanzania wengi tumezoea kulalamika, tunapenda tu kupewa, hatutaki kufanya kazi.

Rais Magufuli:
Ni matumaini yangu hamtaniangusha, hata sura zenu zinaonyesha ni wachapa kazi, nendeni mkachape kazi.

Rais Magufuli:
Nyinyi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mna mamlaka hata ya kuweka watu mahabusu, ila msiende kuonea watu.

Rais Magufuli: Mkasimamie yale tuliyowaahidi sisi wana CCM, mkayatekeleze kwa nguvu zote

Rais Magufuli:
Watanzania wengi wana changamoto nyingi, nina imani hamtaiangusha serikali hii.

Rais Magufuli:
Nataka niseme ukweli, wale ma-DC tuliowaacha hawakufikia vigezo

Mchakato wa kuwapata ma-DC ulikuwa mgumu, ilibidi tuangalie historia ya kila mmoja, tuliangalia mambo mengi sana.

Rais Magufuli anazungumza kwenye sherehe za kuwaapisha kiapo cha uadilifu wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapya.

Mbona wamo wengi tu wenye Historia Chafu
 
Hivi wakuu wa mikoa na wilaya kazi zao huwa ni nini?
Hawa ni makada wa fisiem na hakuna lingine..

Mosi : hawana kasma katika bajeti kuu ya serikali
Pili: hawana uamuzi wa jambo lolote katika maeneo yao katika maswala yanayohusu maendeleo
Tatu: hawana nguvu ķisheria katika jambo lolote, kwa hiyo maelekezo yao yanaweza kupuuzwa na hakuna madhara kisheria na wala hawana namna ya ku enforce chochote wanachokipanga kikifanya

Swali: Hivi kwa akili ya kawaida ni sahihi kulipa vyeo ambavyo havina tija kama hivyo?

Wananchi tunataka katiba yetu.. ili tukomeshe ujuha wa fisiem.. tumechokaaa
 
JPM kamaliza kazi imebaki kwa wapiga debe. Hawa hawalali kutwa kutafuta mabaya na uzushi wa kila rangi. Asante sana mh. rais.
 
Mkuu, na kunguru waoga nao wengi sana pia! wanapenda kusifia tu kwa kila kitu hata kama ni kibaya. Wewe unasimama upande gani?
 
Hata
Leo Tarehe 29 Rais Magufuli anawapisha wakuu wa mikoa na wilaya asubuhi hii live from Azam two na TBC1.

Rais Magufuli:
Gondwe ninajua unatangaza,sasa utakwenda kutangaza maendeleo unakokwenda,ufanye kama unatangaza tangaza tu.

Rais Magufuli:
Mchakato wa kuwapata Ma-DC haukuwa rahisi, ilibidi tutizame historia ya kila mmoja wao.

Rais Magufuli:
Kuna mabadiliko madogo tuliyoyafanya kutokana na jina lilikosewa, kwa hiyo aliyestahili tumeshamuweka.

Rais Magufuli:
Ningeweza nikataja majina yote mliopo hapa mpaka yule aliyepigwa fimbo na mtani wangu, karibu kila jina nalifahamu na sifa yake.

Rais Magufuli:
Mna mamlaka makubwa ya kumuweka mtu Mahabusu ila msiende tu kuonea watu.

Rais Magufuli:
Mnaweza kufikiri tumewachagua sisi lakini inawezekana Mungu ametutumia sisi kuwachagua ninyi.

Rais Magufuli:
Nilikuwa namuona DC wa Iringa anabeba watoto wakamsema sana, na mimi nikasema abaki hapa hapa

Rais Magufuli:
Nilitegemea sana baada ya kuwateua, nilitegemea labda mngekuja robo tu, ninawashukuru sana kwa kuja.

Rais Magufuli:
Watanzania wengi tumezoea kulalamika, tunapenda tu kupewa, hatutaki kufanya kazi.

Rais Magufuli:
Ni matumaini yangu hamtaniangusha, hata sura zenu zinaonyesha ni wachapa kazi, nendeni mkachape kazi.

Rais Magufuli:
Nyinyi wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mna mamlaka hata ya kuweka watu mahabusu, ila msiende kuonea watu.

Rais Magufuli: Mkasimamie yale tuliyowaahidi sisi wana CCM, mkayatekeleze kwa nguvu zote

Rais Magufuli:
Watanzania wengi wana changamoto nyingi, nina imani hamtaiangusha serikali hii.

Rais Magufuli:
Nataka niseme ukweli, wale ma-DC tuliowaacha hawakufikia vigezo

Mchakato wa kuwapata ma-DC ulikuwa mgumu, ilibidi tuangalie historia ya kila mmoja, tuliangalia mambo mengi sana.

Rais Magufuli anazungumza kwenye sherehe za kuwaapisha kiapo cha uadilifu wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wapya.
Hata mrisho gumbo amekidhi vigezo pamoja na mwanae?
 
Back
Top Bottom