Rais Magufuli anahitaji maombi yako

Rais Magufuli anahitaji maombi yako

vita ya uganda na tanzania na vita anayopigana magufuli/nyerere junior ni vita mbili tofauti na ndio maana magufuli anahitaji maombi ili apate ulinzi wa mungu.
Magufuli anapigana vita na adui wa ndani,wengine anaweza akawa anacheka nao na asijue kuwa ni adui na ndio maana anahitaji kuombewa.

Vita zote ni mbaya ila kupigana na unaowajua na usiowajua kuwa ni adui ni hatari zaidi.

Hee leo hii mnasema urais ni ukakamavu,makubwa haya,si nyie mlikua mkisema ikulu hakuna kubeba zege?,tena mkasema hata lowassa akiwa kwenye machela mtamchagua??!!.sasa huyo lowasa angeingia ikulu na vile alivyokua akitetemeka huo ukakamavu angeutoa wapi?najiuliza tu,magufuli alisimama na kuhutubia kwa saa karibia mbili,haya lowasa angewezea wapi na yeye dk 10 tu zilikua mtihani??!!.

Unasema urais ni ukakamavu wkt mnataka kumpeleka lowasa ikulu hamkuliona hilo?

Sio kila vita inapiganwa kwa bunduki na mabomu,vita nyingine silaha inayohitajika ni maombi.

​wangesema hotuba ipo katika mtandao nendeni mka download
 
kuna mambo ambayo magu akiyafanya tu naanza kubeba gun za kiasili kumlinda hku nikikesha kumuombea kwa sasa naona ni rasha rasha tu mvua kamil bdo
 
hata mwalimu nyerere alikuwa na maadui humu ndani, baada ya kufa ndo wapinzani wake wakamkubali ingawa wengine mpk leo hawamkubli.
sishangai kwa maneno yako ingawa una uhuru wa kusema na kutoa maoni lkn hapa mkuu hukuangalia maslahi ya taifa.
kama raia wa mataifa mengine wanamkubali magu sisi humu tunamkataa inatuthibitishia ile kauli ya nabii hakubaliki kwao. au ngombe haoni faida ya mkia wake mpk ukatike.
any way all in all mi nilidhani baada ya maombi yale threads zilizofuata zote zingesema AMINA.

kama umeanza kuwa na akili tunaweza kuongea. Sasa kama unataka sisi raia wa Tanzania tumkubali Magufuli, wewe na wenzako mlikuwa mnaleta thread kwa minajili gani? Mkwa nini mlete thread kuhusu utendaji wa Magufuli kama ulitarajia wote tuusifie. Basi wewe mwenyewe huna imani na huyo Magufuli.

Kama unaamini kuwa wote tunatakiwa kumsifia basi hukuwa na sababu za kuleta thread maana moyo wako ungetulia ukijua tunamuona ni safi na fit.

Ukitaka kumsifia magufuli halafu usipingwe nenda pale Lumumba ofisi ya CCM. Pale hata ukisema Magufuli ndiye binadamu bora tangu kuumbwa ulimwengu hakuna atakayekupinga na atakayethubutu kukupinga atakiona cha mtema kuni.

Kamsifie hivyohivyo kwenye ofisi za CCM utabebwa kwa shangwe na ndani ya mwaka utapata jumba la ghrofa pale Mbezi Beach.

Lakini huku kwa sisi ambao tunajitegemea tunadunda maisha kivyuet, tunaendesha kampuni zetu, tutakuchambua kinagaubaga.

Karibu.
 
Unaonesha kumjua sana nyerere mpaka kufikia kumkosea heshima rais wetu! Una umri gani wewe? Si busara kuongea maneno hayo...

Huwezi kumlinganisha nyerere na magufuri hiyo ni kufuru
 
Anaemfananisha Nyerere na Magufuri ana matatizo kichwani
 
Kwa dhamira aliyonayo Rais Magufuli kwa wananchi na taifa la Tanzania nina uhakika Mwenyezi Mungu atamlinda kama alivyomfikisha kwenye nafasi ya Urais.

Taifa letu lilikuwa limefikia hali mbaya sana kiasi ambacho chochote cha haramu kilikuwa cha halali na cha halali kilikuwa cha haramu, bila kumpata kiongozi shupavu na jasiri kama Rais Magufuli Tanzania ilikuwa inaelekea pabaya sana.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona vyama vya upinzani kuanza kupinga mabadiliko aliyoyaleta na anaendelea kuyaleta hapa Tanzania, kauli mbiu za vyama vya upinzani ilikuwa ni mabadiliko na kwasasa Rais Magufuli anatekeleza kauli mbiu hiyo bila kujali itikadi ya Chama chake cha CCM.

Naomba wanasiasa bila kujali itikadi ya vyama vyao wamuunge mkono huyu ndugu yetu Rais Magufuli kwa faida ya watoto wetu na vizazi vyetu.

Katika bara la Afrika ni nadra sana kumpata kiongozi aina ya Rais Magufuli sasa tusipotezee baraka hii Mwenyezi Mungu aliyetupa, na ninawashauri viongozi waliokuwa wamekuwa na mazoea ya ufisadi the honeymoon is over wabadilike kwa faida ya nchi hii.
 


Kwa dhamira aliyonayo Rais Magufuli kwa wananchi na taifa la Tanzania nina uhakika Mwenyezi Mungu atamlinda kama alivyomfikisha kwenye nafasi ya Urais.
Taifa letu lilikuwa limefikia hali mbaya sana kiasi ambacho chochote cha haramu kilikuwa cha halali na cha halali kilikuwa cha haramu, bila kumpata kiongozi shupavu na jasiri kama Rais Magufuli Tanzania ilikuwa inaelekea pabaya sana. Ni jambo la kusikitisha sana kuona vyama vya upinzani kuanza kupinga mabadiliko aliyoyaleta na anaendelea kuyaleta hapa Tanzania, kauli mbiu za vyama vya upinzani ilikuwa ni mabadiliko na kwasasa Rais Magufuli anatekeleza kauli mbiu hiyo bila kujali itikadi ya Chama cha CCM. Naomba wanasiasa bila kujali itikadi ya vyama vyao wamuunge mkono huyu ndugu yetu Rais Magufuli kwa faida ya watoto wetu na vizazi vyetu.
Katika bara la Afrika ni nadra sana kumpata kiongozi aina ya Rais Magufuli sasa tusipotezee baraka hii Mwenyezi Mungu aliyetupa, na ninawashauri viongozi waliokuwa wamekuwa na mazoea ya ufisadi the honeymoon is over wabadilike kwa faida ya nchi hii.
 
UPINZANI AMBAO HAUJIAMINI HATUUTAKI TANZANIA...

UPINZANI AMBAO HAUELEWEKI UNASIMAMIA AGENDA GANI NI WA KUPUUZWA...HAUWEZI KUTUVUSHA.


UPINZANI AMBAO UNATETEA MAFISADI NA WAVIVU HUKU UKIMUITA DIKITETA ANAYECHUKULIA HATUA MAFISADI UNAPASWA KUTOUNGWA MKONO NA WANAOLITAKIA MEMA TAIFA LETU.
 
Hata Kikwete mlitulaghai kuwa alikuwa chaguo la Mungu na kusifia kila alichofanya na sasa mnatulaghai kuwa alifikisha nchi pabaya. Leo hii mnatulaghai Magufuli analindwa na Mungu huku anatumia katiba ile ile aliyoitumia Kikwete na pia amekataa katakata kurudisha katiba ya Warioba, sana sana amempoza Warioba kwa kumpa Kippi Warioba ukuu wa wilaya. Mungu hawezi kumlinda mtu ambaye hatendi haki, Mungu atamlinda Magufuli kama akitenda haki na kuachia uhuru wa siasa na kutoa maoni. Ni ajabu sheria ya mitandao imeundwa kwa ajili ya Magufuli peke yake, akitukanwa mitandaoni aliyetukana anakamatwa haraka na kamera juu, mimi na wewe tukitukanwa hata tukienda kushtaki polisi tunaambiwa tutoe hela. Mungu hawezi kumlinda mtu kama huyu
 
Usipoiheshimu Katiba Uliyoapa kuilinda na kuitetea kwa jina la Mwenyezi Mungu. Baraka za Mungu utazisikia kwa jirani.
 
Kwa dhamira aliyonayo Rais Magufuli kwa wananchi na taifa la Tanzania nina uhakika Mwenyezi Mungu atamlinda kama alivyomfikisha kwenye nafasi ya Urais.
Taifa letu lilikuwa limefikia hali mbaya sana kiasi ambacho chochote cha haramu kilikuwa cha halali na cha halali kilikuwa cha haramu, bila kumpata kiongozi shupavu na jasiri kama Rais Magufuli Tanzania ilikuwa inaelekea pabaya sana. Ni jambo la kusikitisha sana kuona vyama vya upinzani kuanza kupinga mabadiliko aliyoyaleta na anaendelea kuyaleta hapa Tanzania, kauli mbiu za vyama vya upinzani ilikuwa ni mabadiliko na kwasasa Rais Magufuli anatekeleza kauli mbiu hiyo bila kujali itikadi ya Chama chake cha CCM. Naomba wanasiasa bila kujali itikadi ya vyama vyao wamuunge mkono huyu ndugu yetu Rais Magufuli kwa faida ya watoto wetu na vizazi vyetu.
Katika bara la Afrika ni nadra sana kumpata kiongozi aina ya Rais Magufuli sasa tusipotezee baraka hii Mwenyezi Mungu aliyetupa, na ninawashauri viongozi waliokuwa wamekuwa na mazoea ya ufisadi the honeymoon is over wabadilike kwa faida ya nchi hii.
Daaaa wewe jamaa umejiunga jf leo hii kisa kutuletea uzi kama huu?
 
Back
Top Bottom