Viongozi wetu wamekuwa wakituasa tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu. Tatizo hawatuelezi tuwaombee wapate kitu gani. Mimi napendekeza tuwaombee kuwa na HEKIMA.
Biblia inatueleza kwamba Mwenyezi Mungu alimpatia Mfalme Suleimani fursa ya kuomba chochote. Mfalme Suleimani aliomba apatiwe HEKIMA. Ombi la Suleiman lilimpendeza Mwenyezi Mungu na Suleiman akapatiwa HEKIMA na kuongezewa kila kitu ikiwa ni pamoja na Amani na Utajiri.
HEKIMA ninayowaombea ni ile itokayo juu kwa Mwenyezi Mungu. Mtume Yakobo anaelezea hekima itokayo juu kuwa ni ile iliyo safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Wewe anapendekeza tuwaombee viongozi wetu wapate kitu gani?