Rais Magufuli akutana na Viongozi wa vyama vya Siasa nchini, Maalim Seif(ACT-Wazalendo), Prof. Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi)

Wapinzani wamepigwa marufuku kuendesha shughuli zao halali za kisiasa, wanabambikiwa kesi, wanafanyiwa kila aina ya uonevu na vyombo vya dola, halafu leo kukutana na baadhi ya viongozi wa upinzani ikulu ndiyo igeuke kuwa habari kubwa, yenye kushereheshwa na picha za hamasa.

Tuelezwe mazungumzo ya viongozi hawa yalikuwa na tija gani kwa mustakabali wa Taifa letu.Tuache siasa nyepesi, tuzungumze kuhusu uwanja wenye haki na usawa kwa vyama vyote vya siasa hapa nchini, hasa tuelekeapo uchaguzi wa mwaka huu. Zaidi ya hapo itakuwa ni udwanzi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Screenshot_20200303-141241-picsay.jpeg
 
Ikulu wamefanya vetting vizuri sana, hakuna viongozi wenye kesi mahakamani walioruhusiwa kwenya Ikulu.
 
Hata ufanyeje Jiwe kukutana na viongozi wa upinzani,haitakusaidia mabeberu hawakuachi iwe jua iwe mvua.
 
Ni lazima nimpongeze Raisi Magufuli kwa kukutana na upinzani na kuwasikiliza. Nashukuru kwa washauri wa hili ambao wamemwambia ukweli.

Nilishasema na kuandika huko nyuma faida ya kuwanyima uhuru upinzani hautasaidia CCM wala taifa. Tunavyoongea leo hii pamoja na migawanyiko ambayo haina maana tulikosa $550M kwa sababu ya uchaguzi wa Zanzibar, tumezuiwa kusafiri kwa nchi nyingine, na nimesikia kula list mpya yenye majina ya viongozi ambao wanaingia kwenye list ya Makonda aliyopewa na US lakini inasubiri uchaguzi tu kama hautakuwa wa haki list hii itaongezeka kwa viongozi na familia zao.

Lakini vilevile nina wasiwasi shughuli nyingine za maendeleo.

Ujumbe wa Magufuli unatakiwa uwekwe wazi kwa watendaji ambao ni wafaidi wakubwa wa kugombana CCM na vyama vya upinzani.

Hebu angalieni Mkuu wa Wilaya ya Hai hata siku moja hatujasikia anaongelea kusaidia utalii pake KIA na kuhimizwa ujenzi wa hoteli kwa wasafiri badala yake na majungu kwa mbowe sasa hii inasaidia vipi nchi? lakini kwa ujinga huu hafukuzwi kwasababu za kisiasa!.
 
Mkuu Magufuli hajakutana na hao wapinzani kwa kuwa anataka muafaka, bali kukutana na hao wapinzani ili kuhadaa dunia kuwa anatenda haki kwa wapinzani wake. Lengo hasa la hiyo hadaa ni ili kujitoa kwenye mbinyo wa kimataifa na sio kutenda haki. Kama kweli angekuwa mtenda haki angekubali tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Usiwe mwepesi kuhadaiwa na siasa nyepesi.
 
Ulioitwa Ikulu ulikuwa “Upinzani Maalum“. Upinzani original unavurugiwa mikutano na polisi CCM wanakatisha mikutano yao.
 
Sasa mnaanza kuelewa uhovyo wa Magufuli, kwangu mtu asiye heshimu binadamu nzie kisa utofauti wa mtazamo huwa na mrank chini ya sifuri.
 
wandamba,
Naam na hilo ndo lilikuwa lengo kuu la mkutano ule na si kuondoa tatizo la msingi! Baadaye mtaelewa mnavyo ongozwa na wanafiki waandamizi wanao tenda pasipo kuzingatia ustawi wa jamii bali kujikosha mbele ya mataifa.
 
Back
Top Bottom