Rais Macron naye ailalamikia US: Mnatufanyia hujuma isiyo ya kawaida katika kipindi hiki kigumu

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku tatu mjini Washington, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewaambia wabunge wa Marekani kwamba nchi yao inaifanyia Ufaransa "hujuma isiyo ya kawaida hasa katika kipindi hiki cha mdororo wa nishati na uchumi kutokana na Covid-19 na mzozo ya Ukraine".

Macron amewaambia wajumbe wa Congress na viongozi wa sekta ya biashara wa Marekani kwamba: "Sera hizi hazifai kabisa kwa wafanyabiashara wa Ufaransa." Macron alikuwa akiashiria sheria ya kupunguza mfumuko wa bei iliyotiwa saini hivi karibuni na Rais Joe Biden inayojulikana kama Inflation Reduction Act of 2022 (IRA). Kwa mujibu wa sheria hii, mabilioni ya dola yatatolewa kwa viwanda ambavyo ni rafiki kwa mazingira kwa ufadhili wa serikali ya Marekani.

Ikulu ya White House imeitaja sheria ya IRA kuwa ni juhudi za kufufua uzalishaji wa Marekani na kukuza teknolojia jadidika. Hata hivyo nchi za Umoja wa Ulaya zinaamini kuwa Marekani imeanzisha vita vya kibiashara dhidi ya Ulaya kwa kutoa ruzuku kwa sekta ya uchumi wake wa kijani, na wakati huo huo, itazinyima kampuni za Ulaya fursa ya kushindana kwa haki na washindani wao wa Marekani kwa kutoza ushuru kwa bidhaa za makumpuni ya Ulaya.

Waziri wa Uchumi wa Ufaransa, Bruno Le Maire akikosoa "ushindani wa ruzuku" ambao anasema ni kinyume na kanuni za biashara ya kimataifa, ametoa wito wa kutolewa "majibu ya pamoja na yenye nguvu ya Umoja wa Ulaya dhidi ya mshirika wake, Marekani, na kusema, juhudi kubwa ndizo zitakazozaa matunda."

Ameongeza kuwa: Baadhi ya makampuni makubwa ya kigeni ambayo yalikuwa na nia ya kuwekeza Ulaya sasa yanasitasita kati ya kuwekeza maeneo ya Ulaya au Marekani. Amesema katika baadhi ya matukio, kiasi cha usaidizi wa kifedha unaotolewa na utawala wa Biden kwa makampuni ya Marekani ni mara nne hadi kumi ya kiwango cha juu kinachoruhusiwa na Tume ya Ulaya.

Akisisitiza kwamba tabaka la kati la Ufaransa linahitaji ajira, Macron amesema: "Hatutaki kuwa soko la kuuza bidhaa za Marekani kwa sababu tuna bidhaa sawa na zile zinazozalishwa nchini Marekani. Matokeo ya sheria ya IRA ni kwamba yumkini nyinyi mkatatua matatizo yenu, lakini itazidisha matatizo yetu."

Karine Jean-Pierre, katibu wa waandishi wa habari wa Ikulu ya White House, amejibu matamshi hayo ya Macron akidai kwamba, maendeleo ya Marekani katika uchumi wa nishati safi yatawasaidia watu wa Ulaya. Katika wiki chache zilizopita, viongozi na maafisa wa ngazi za juu wa nchi za Ulaya wameonya juu ya hatari ya vita vya kibiashara na Marekani na kutishia kwamba iwapo Washington itaendelea kupuuza ukosoaji wa Umoja wa Ulaya, watawasilisha malalamiko yao katika Shirika la Biashara Duniani dhidi ya Marekani.

Wasiwasi wa makampuni ya Ulaya umeongezeka sana kuhusu ongezeko la hatari ya bara hilo kuingia katika mdororo wa kiuchumi mwaka ujao kutokana na madhara ya kiuchumi ya vita vya Ukraine na kupanda kwa bei ya nishati kusikokuwa na kifani

Note:
Wiki hii viongozi waandamizi wa EU wanabweka, Kuna nini??




- Rais wa Ufaransa: "Muundo wa usalama wa Ulaya lazima utoe 'guarantee' kwa usalama wa Urusi"

- RAIS WA EU: Ulaya itashuhudia kipindi kigumu sana hivi karibuni


-
- Ulaya ‘haina nguvu za kutosha’ kukabiliana na tishio la Urussi – Finland


- Idadi ya wanajeshi wa Ukraine wanaotoroka vitani inaongezeka baada ya matamshi ya Ursula Von der Leyen - LPR

- EU: Wanajeshi 100,000 wa Ukraine wamekufa katika vita
 
Back
Top Bottom