Rais kutumia ndege ya abiria badala ya ndege yake binafsi, nani mshauri wake?

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,734
10,041
Jamani ndege kama hii BOEING 737-9 max ni ndege ya gharama sana achana na ununuzi wake tu bali hata maintenance pia.

Inasikitisha kuona Rais anatumia ndege hii yenye gharama kiasi hiki huku ndege ya Rais ikiwepo bado.

Sitashangaa ikipata hitilafu tukaitelekeza mahali kwa sababu matumizi yake hayakuendana na faida kutokana na ubinafsi wa watu wachache.

images (5).jpeg
 
Jamani ndege kama hii BOEING 737-9 max ni ndege ya gharama sana achana na ununuzi wake tu bali hata maintenance pia.

Inasikitisha kuona Rais anatumia ndege hii yenye gharama kiasi hiki huku ndege ya Rais ikiwepo bado.

Sitashangaa ikipata itilafu tukaitelekeza mahali kwa sababu matumizi yake hayakuendana na faida kutokana na ubinafsi wa watu wachache.

View attachment 2914630
Ningefurahi kama ungeeleza bayana mantik ya hoja yako kwa ufupi kama hutojali 🐒

Becoz let's face it, hujaeleweka bayana
 
Nadhani ni bora atumie hizo za ATCL, kuliko kuanza kununua ndege mpy za viongozi. Maana sasa wameshapitisha ndege za viongozi ziongezwe; wakati Mama anakata mawingu kwa ndege ya ATCL. Sasa si itakuwa gharama mara mbili, bora tu atumie hiyo - mambo yaishe. Akiwa hana safari - ndege yetu iendelee tu kuhudumia abiria.
 
Unajitoa ufahamu sana mwamba. Inamaana kusoma hujui hata picha huoni? Weka uchama pembeni face uhalisia
Niwie radhi Mkuu Kwa maoni yangu.

Nilitaka kujua kwamba umejuaje anaitumia, yaani Kuna alama yeyote imeonekana kwenye hiyo ndege.

Maana ninachojua nilipanda Mwaka Jana, kwahiyo suala la kubadirishwa Matumizi ndiyo nilikuwa silijui.

Kwakuwa Mkurugenzi Mkuu wa ATCL ni teuzi ya Rais, hivyo hawezi kumgomea boss wake akihitaji kuitumia hiyo ndege

Ndiyo maana wenye mawazo Chanya walishauri Wakuu wa Taasisi na Mashirika waajiriwe Kwa kuzingatia Merits badala ya kuteuliwa tu, vivyo hivyo Rais apunguziwe madaraka Kwa Mujibu wa Katiba Pendekezwa
 
Back
Top Bottom