Rais Kikwete, Watanzania wana imani na wewe achana na hoja dhaifu za Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete, Watanzania wana imani na wewe achana na hoja dhaifu za Chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Jun 23, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Watanzania bado wana imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete, kuna baadhi ya watu ambao wanaishambulia serikali ya JK kuwa kuna ufajaji wa fedha za umma, ufajaji wa fedha za umma kwa vigogo wa serikali hayakuanza leo bali tangu serikali zilizopita.

  Rais Kikwete amezipa meno na mamlaka za kisheria Takukuru na ofisi ya CAG kuwafungulia mashtaka moja kwa moja mahakamani, Rais ameweza kuvunja hata mtandao mkongwe wa viongozi kulindana na ndio maana hata wabunge sasa wanakamatwa kwa rushwa tofauti na huko nyuma.

  Baada ya uchafu wa hesabu fedha za umma kubainika, kwa mara ya kwanza Kikwete kuunda kamati ya ukaguzi inayojumuisha wataalam wa ukaguzi wa hesabu, Takukuru, Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Maofisa Upelezi, Usalama wa Taifa, kwa kutumia ripoti ya CAG wanaweza kubaini wizi, kiasi kilichoibiwa kwa njia gani na wahuisika wote.. Kuna normal auditing (ukaguzi wa hesabu wa kawida) na forensic auditing (ukaguzi wa hesabu unaobaini wizi na vielelezo vya kumshtaki mahakamani mhusika) kwa miaka yote Ofisi ya CAG imekuwa ikifanya ukaguzi wa normal auditing na kugundua uchafu na serikali kukaa kimya na wizi wa fedha umma ulikithiriri sana.

  Utaratibu wa forensic auditing Wakurugenzi wengi katika halmashauri zetu wengi lazima wafikishwe mahakamani.

  Rais Kikwete kwa muda wake takribani miaka sita ameweza kuvunja rekodi ya ujenzi wa barabara kakamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa takriban kilomita 11,000 kwa kiwango cha lami, ikilinganishwa na kilomita takriban 6.000 tu zilizojengwa na serikali zilizomtangulia, za Mwl Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa.

  JF Daima
   
 2. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  We koma kutusemea watanzania.

  Ni mjinga peke yake ndie anaweza kuwa na imani na mtu mdhaifu!
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Vipi ule utaratibu maalumu aliowaundia wezi wa EPA, aka "rudisha usamehewe wizi"??
   
 4. s

  simon james JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwache amdanganye kuwa huu ni upepo wa kisiasa utapita alafu asubiria kimbunga kije kumzoa!
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ritz,

  Kwa hayo hayo ndio Kikwete hapendeki. Ukitazama wengi wa wanaoleta chuki na kejeli utakuta wengi ni wale wale waliozibiwa mianya ya wizi kwa mara ya kwanza toka hii nchi ipate Uhuru katika kipindi hiki cha Kikwete.

  Baada ya muda mfupi, Kikwete anaanza kushughulikia fedha zilizowekwa nje ya nchi na hawa wizi wa mali za umma. Ni kazi ngumu sana, lakini ipo njiani inakuja, tutaona chuki zikizidi. Ukitazama kijuu juu tu hata bila ya uchunguzi wa kina utakuta wote wenye chuki ni wale wale 83%. Hao ndio "wasomi" bila kuelimika, hao ndio walioifikisha nchi ilipofika na hao ndio wezi wakubwa.

  Tunamtakia kila la heri Kikwete kwa hii kazi ngumu aifanyayo sasa, na matokeo tunayaona. Na hapo ndiyo eti "dhaifu".

  Subiri uone majibu sifuri sasa hivi.
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280

  zomba.

  Ni kweli kabisa watu wanamchukia Kikwete sababu kaziba mianya ya rushwa na kulindana...hata hoja inayosimamiwa na Chadema ya Ufisadi haina nguvu tena wanaofanya hivyo wameshulikiwa na ushahidi upo katika mahakama mbali mbali nchini.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Kuna mwandishi aliandika kitabu ambacho kinaelezea habari kuwa ni 'kinyumbe cha mambo'. Hakika uliyoyaandika hapa ni kinyume cha mambo!
   
 8. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Imani gani waliyonayo watanzania kuhusu Kikwete? kuwafanya wajutie kumchagua?
   
 9. m

  mamajack JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ndugu mtoa mada nadhani hujafanya reseach ya kutisha unachokiongelea.

  Kila siku unasikia watu wanashindwa kusafirisha mazao sababu ya ubovu wa miundo mbinu ya barabara, hata hao wabunge wanaliliamikia hili japo wanakosa uzalendo na wanaogopa kwenda kinyume na maelekezo ya wakuu wao.
   
 10. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Hawa wakulima wadogo (peasants) kule Ruvuma , Njombe, Mbeya, Rukwa, Iringa............ambao hawapati pembejeo za kilimo nao wanamchukia kwa kuwa wamezibiwa mianya ya rushwa?
   
 11. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 866
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Sikutegemea mchabuzi kama wewe una hoja dhaifu za kuwaelzea chekechea umesahau kuwa hapa ni jamii forum. Tunashukuru kutambua upeo finyu wa fikra yako.Ila punguza kujipendekeza na kuwa mchumia tumbo. Watanzania wa sasa ni waelewa na wanazitambua ghiriba na propanganda za akina TAMBWE HIZA.

  Nchi hii ina matatizo mengi na hasa kwa wananchi walio wengi, kwasas iefikia kuwa nchi iliyo na upungufu wa chakula , wakati ina ardhi kubwa yenye rutuba, mabonde mengi na nguvu kazi inayotosha na asili ni kuchapa kazi za kilimo.

  Sasa kama wananchi hawasaidiwi kwa hili bali bla bla watakuwa na imani naye kivipi? Namna anavyochukua hatua kuhusu kufufua ushurika ni vichekesho tupu. Nakumbuka wakati anatoa mafedha ya kikwete wachambuzi wengi tusihi fedha hizo zitumike kufufua ushirka na kilimo kwa ujumla ndo hapo impact ingeoneka. Leo hii ukiuliza fedha hizo ni blabla tu na nadharia kubwa.

  Kumsifia JK ni uendewazimu. Alingia madarakani kukiwa na tatizo la umeme, leo miak takribani miaka ifikayo 8 bado blabla. Kama angekuwa si dhaifu ingechukua miaka miwili tu lazima tungeona mageuzi katika sekta hii. Tuna tatizo la kupanda bei ya mafuta , lakini maelezo yanatoka bado blabla na hakuna hatua za dhati kuonyesha wanachukua hatua gani.

  Hata hao EWURA ni blbabla tu wameshikiliwa na matajiri wa mafuta, tabu kabisa. Uje sekta ya usafirishaji kama ATCL, TRL jamani tunamzimu gani wa kijinga? Halafu unakuja na hoja za chekechea!inaonyesha shule ulikuwa unabebwa sana kwa degree za chupi wewe
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Sikuwai kufikiri kama ritz una uwezo wa kumtete JK.

  Kweli nime amini inabidi nichanganyikiwe kwanza ndio nikubali huo utetezi wako!

  Hivi lowasa amefikishwa mahakama gani?
   
 13. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mwenye data halisi atoe, JK na serikali yake wanasema wamejenga barabara zenye urefu wa km 11,000.

  Ninazozifahamu ni Minjingu Babati km 160 Babati Singida km 163, Manyoni Singida Kamalizia km 60 zilizobaki katika barabara ya Dodoma mpaka kanda ya ziwa, Ndundu Somanga km 60 alizoacha Ben bado hazijaisha, Handeni Mkata km 110, hazijakamilika, Babati Kondoa km 5 tu zina lami, Kondoa Dodoma imeanza kujengwa km 3 (kuna jumla ya km 290 za barabara hii), Dodoma Mtera Iringa km 320 zimekamilika km 35. Hizo nilizozitaja zina jumla ya km 1,163.

  Tuwekeeni mambo hadharani hizo barabara zenye urefu wa km 10,000 nyingine ni zipi? Au ndio zile za Tabora - Nzega, Tabora - Manyoni, Sengerema, Nyakanazi - Kibondo, Kigoma - Kasulu - Mpanda, Tunduma - Sumbawanga na kadhalika. Tuwekeeni data tupate km 11,000 as per magufuli data.
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Aachane na hoja Dhaifu za CHADEMA? Kwani yeye ni Imara kuliko hizo hoja?
   
 15. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ritz kuna yale ya mtu mmoja moja na yale ya ujumla ambayo waliomchagua na wasiomchaguwa jk anatakiwa ayafanye kama kiongozi mkuu ...kila mtu anakusanya kodi au anachangia kila ukinunua kitu hata kiberiti mafuta ya taa na bia nk lakini msimamizi mkuu ni yeye
  hebu fikiria hakuna kinachoenda hakuna maji ya uhakika hata hapo anapoishi yeye dar kila siku bomba linapasuka ninahamaki ka vile yapo mengi ya kipuuzi kuliko mazuri...hatuna takukuru wala police wala mahakama ndio maana nasema wewe labda haupo nchini.hujawahi kuibiwa ili police na mahakama itende kazi yake inabidi wewe mwenye kuibiwa utoe pesa ili usaidiwe ..ili mtoto wako asome lazima umpeleke privata au st fulani ndio apate eelimu...nyumba ikiwaka moto unaomba mungu hakuna gari za zimamoto...taka unavizia usiku unatupa kwenye chaka lolote'
  hivi hata wale wanaochota maji kwa ndoo huwaoni wapo pembeni ya ziwa au mito .
  kinachouma zaidi michango yetu wanakula watu wachache yaani rafiki zake waajiriwa serikalini hasa viongozi sio walim na dactari

   
 16. U

  Ubongo Silaha Senior Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Unapojenga barabara kwa kuomba misaada badala ya rasilimali unazoachia ziondoke!
  Unaposamehe kodi kiasi kikubwa kuliko misaada ya masharti
  Unapokubali bei ya kujenga barabara kwa kilomita iwe inflated na usiwe na system ya ku-verify
  Unapotoa amri zisitekelezwe mfano kiushusha bei ya sukari na usichukue hatua
  Unapoanzisha mada kama ya kuvua gamba na isitekelezwe na uliruhusu gamba likusute kwenye kikao unachokiongoza wewe
  Unapoita madaktari ukawabembeleza warudi kazini wakakuheshimu na siku ya pili ukawasuta mbele ya 'Wazee wa Dar
  Unaporuhusu mbunge aliyepokea milioni moja akamatwe lakini waliooiingiza Tz kwenye mikataba ya kipuuzi na ikathibishwa wameweka fedha zaidi ya bilioni ughaibuni wapete
  Unapoangalia wasaidizi wako wakipanda na kushabikia udini
  Unapotumia Bakwata kama kipaza sauti chako
  Unaposhindwa kuwaadabisha mawaziri wako hadi ushinikizwe na Bunge

  Nashindwa kuwa na imani na wewe
   
 17. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye nyekundu.Naona unajaribu kutudanganya bila mafanikio ,Jk ameingia madarakani fedha za barabaza zilishatengwa na awamu ya tatu.Labda utoe takwimu sahihi kwamba ni barabari ipi mpya ambayo haikuwa kwenye mipango na utekelezaji wa serikali ya awamu ya tatu ameinzisha yeye.Alipoingia madarakani miradi mingi imekwama kutokana na kukosekana kwa fedha.Fedha nyingi amezielekeza kwenye miradi mipya hewa ili wafanye ufiiadi mfano RICHMOND na safari za nje nyingi zisizo na tija kwa taifa.

  Ukweli ni kwamba miradi mingi mikubwa wamepindisha ukweli kuwa hakuiazisha wala kuwekea mipango Jk ila wanadanganya uma kwa kujitafutia umaarufu.Mfano daraja la Umoja (Mpakani na Msumbiji) na EPZ (Export Processing zone).

  Bado nakubaliana na kauli ya J.Mnyika kwamba Jk ni dhaifu.
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Hadi kufika mwaka 2015 barabara ya kutoka Nyakanazi-Uvinza- Mpanda- Sumbawanga hadi Tunduma itakuwa imekamilika kwa kiwango cha lami, huku barabara ya kutoka Mwandiga jimboni kwa Zitto Kabwe hadi Kidahwe-Nguruka-Urambo hadi Tabora itakuwaimishakamilika baada ya kukamilika ujenzi wa daraja la Mto Malagalasi ambalo lilizishinda serikali zilizotangulia kabla ya JK.
   
 19. j

  joystaff77 Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pumbaaaaaa!!!! Kwenu kuna wanawake mpe mmoja uone imani yake acha kukurupuka
   
 20. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  JK rais dhaifu Africa
   
Loading...