Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
"United Nations Foundation wametupa tuzo ijulikanayo kama “2011 Social Good Award†kwa kuendeleza midia jamii na kutumia teknolojia ya kisasa kukabili changamoto za maendeleo ikiwa ni pamoja na huduma ya afya ya kina mama. Pili,tumepewa tuzo ya the South-South News Award kutokana na mafanikio tunayoyapata katika kuboresha afya nchini na kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili hiyo. Pia, kwa kutambua mchango tunaoutoa kwa maendeleo ya dunia. Na tatu, kutoka Soko la Mitaji la NASDAQ tumepewa tuzo kwa kutambua mchango wangu na mafanikio tunayoyapata katika kupunguza vifo vya kina mama na watoto."
Umeshaziona hizo Tanzania hii kabla ya Kikwete, hususan hiyo ya utawala bora? Bila "nidhamu kwa watumishi wa umma" utapewa hiyo?
Kikwete hakisii, anafanya kweli, na kwa hilo la "nidhamu kwa watumishi wa umma", si mimi nnaesema hayo, ni Mataifa yaliyoipa Serikali yake tuzo ya utawala bora. Kuna uongozi wa Rais wa kabla yake uliopata hiyo tuzo au ya Umoja wa Mataifa au japo inayofanana nayo?
Hizo tuzo zote zimeleta manufaa gani kwa taifa, ikiwa taifa ni la tatu kwa kuombaomba duniani?!
Hizo tuzo danganya toto tu..hawafahamu ukweli katika ground zero. Ina maana akina mama huduma zao zimeboreka zaidi?! Mbona mahospitalini wanalala zaidi ya watano katika kitanda kimoja?!? Vifo vya akina mama na watoto navyo vimepungua kweli? Kwa takwimu zipi? Zilizoandaliwa na nani?
Jamaa anapewa matuzo meni ya kudanganyika kwa sababu ni dhaifu na anadanganyika kuliko watangulizi wake. Anapewa vituzo hivyo na kuuza nchi!! Hata rais Mwinyi hasingekubali utaratibu huo.