Rais Kikwete, Watanzania wana imani na wewe achana na hoja dhaifu za Chadema

Unajua Ritz, wengi wa wanaochangia humu (hope hawa wakilishi taswira halisi ya wa-Tanzania) inaonekana ni watu ambao hawataki kufikiri, na au hawajui kufikiri, sina uhakika hii ndiyo dhana hasa ya JF. Watu nadhani wana jazba na matatizo yanayowakumba kimaisha, ila haiwezi kubadilisha ukweli wa ulichosema.
 
Samahani kama nitakuwa nimetoa lugha mbaya ila si kwa kumdhalilisha mtu;Naomba kuuliza hiv huyu mwanzisha uzi ana akili timamu? Kwani mi nahisi kuwa unatania,na kama unatania basi nenda jukwaa la utani hapa zinawekwa maada zenye uzito unaoonekana wenyewe na sio unaoonyeshwa na mtu,kwa kukusaidia chagua watu wa aina yoyote,(waweza kuwa wanafunzi,wasomi,wazee,wapiga debe,mama ntilie nk)halafu jaribu kuwauliza yaani hii maada yako iwe swali kama kipimajoto cha ITV kinavyoulizwa,halafu tathmini majibu utakayoyapata halafu ndo uje upost maada kama hii hapa nadhani kuna kitu utajifunza.Weekend Njema
 
Hawa wakulima wadogo (peasants) kule Ruvuma , Njombe, Mbeya, Rukwa, Iringa............ambao hawapati pembejeo za kilimo nao wanamchukia kwa kuwa wamezibiwa mianya ya rushwa?

asilimia kubwa wanaomchukia rais wa tanzania, ni vijana ambayo ni jobless tena wengi waliokimbia shule,wanafunzi wanaosomea siasa pamoja na vijana waliotekwa kimawazo na wanasiasa!na sio wakulima kama unavyodai!! Tena vijana wavivu wa dar es salaam ndio wanaongoza kumchukia rais wa jamuhuri ya muhungano wa tz.
 
Hawa wakulima wadogo (peasants) kule Ruvuma , Njombe, Mbeya, Rukwa, Iringa............ambao hawapati pembejeo za kilimo nao wanamchukia kwa kuwa wamezibiwa mianya ya rushwa?

Si nyinyi mnashindwa kusambaza, wakati pembejeo Kikwete kisha idhinisha zamani, kwa mara ya kwanza, mlitaka aje kuwasambazi?
 
Si nyinyi mnashindwa kusambaza, wakati pembejeo Kikwete kisha idhinisha zamani, kwa mara ya kwanza, mlitaka aje kuwasambazi?

Sasa kama wanashindwa kusambaza hizo mbolea,rais anawachukulia hatua gani? Yeye si ndiye bosi wao mkuu?!

Kwa namna hiyo kwanini wakulima wasimwone rais ni dhaifu,kwa kuwa anashindwa kuwawajibisha wasaidizi wake.
 
Ngoja nikukumbushe udhaifu wa Kamanda wako Mbowe mwaka 2005 alipogombea Urais sera yake kwenye mikopo kwa wanafunzi wa vyuo na elimu ya juu, alipendekeza dhamana ya mikopo hiyo kuweka rehani nyumba au shamba endapo mwanafunzi atashindwa kurejesha mkopo wake, mali za mzazi wake ziuzwe kufidia deni...kama Chadema wangechukuwa nchi kipindi hicho wazazi wengi wangekuwa wamekwishafilisiwa...huu ni Udhaifu wa kiwango cha juu kabisa.
Ritz,
Mimi nilipokuwa naenda kusoma, na hii ilikuwa miaka mingi tu kabla ya kuwepo Chadema au vyama vya upinzani, ilibidi baba yangu aniwekee dhamana, na alichofanya ni kuweka dhamana nyumba yake. Kwa bahati nzuri, nilimaliza masomo bila rabsha na mpaka leo nyumba ya baba bado imo mikononi mwa familia. Kwa hiyo usibeze wazo ambalo kwa wengine limewasaidia kuwakomboa na adui ujinga.
 
Samahani kama nitakuwa nimetoa lugha mbaya ila si kwa kumdhalilisha mtu;Naomba kuuliza hiv huyu mwanzisha uzi ana akili timamu? Kwani mi nahisi kuwa unatania,na kama unatania basi nenda jukwaa la utani hapa zinawekwa maada zenye uzito unaoonekana wenyewe na sio unaoonyeshwa na mtu,kwa kukusaidia chagua watu wa aina yoyote,(waweza kuwa wanafunzi,wasomi,wazee,wapiga debe,mama ntilie nk)halafu jaribu kuwauliza yaani hii maada yako iwe swali kama kipimajoto cha ITV kinavyoulizwa,halafu tathmini majibu utakayoyapata halafu ndo uje upost maada kama hii hapa nadhani kuna kitu utajifunza.Weekend Njema

Kajifundishe kwanza kuandika unaleta utoto JF hujui hata matumizi ya herufi kubwa na ndogo.
 
Hadi kufika mwaka 2015 barabara ya kutoka Nyakanazi-Uvinza- Mpanda- Sumbawanga hadi Tunduma itakuwa imekamilika kwa kiwango cha lami, huku barabara ya kutoka Mwandiga jimboni kwa Zitto Kabwe hadi Kidahwe-Nguruka-Urambo hadi Tabora itakuwaimishakamilika baada ya kukamilika ujenzi wa daraja la Mto Malagalasi ambalo lilizishinda serikali zilizotangulia kabla ya JK.
Fedha hizi zilitoka wapi? Unaweza kutuwekea hapa pia? Na ulianza kubuniwa lini mradi huu wa hizi barabara?
Na je kwa uhakika ulio nao wa maana ya Uraisi, kwa kukamilisha barabara hizo na hilo daraja atakuwa si dhaifu tena?
Ni hayo tu tulitegemea kwa Raisi kwa kipindi cha miaka kumi? Je ukipiga hesabu sawa sawa ukalinganisha hasara za yaliyoshindikana kudhibiti, kutekeleza nk. na machache atakayokuwa amefanikisha (kama yatafanikiwa) uwiano ni wa kuridhisha?
 
Hoja Dhaifu ya Kuteua Mawaziri wanaokatwa Mikono kwa Kufanya Ngono na wake za watu, na wanaoibiwa na machangu vitu vyote.
 
Ritz,
Mimi nilipokuwa naenda kusoma, na hii ilikuwa miaka mingi tu kabla ya kuwepo Chadema au vyama vya upinzani, ilibidi baba yangu aniwekee dhamana, na alichofanya ni kuweka dhamana nyumba yake. Kwa bahati nzuri, nilimaliza masomo bila rabsha na mpaka leo nyumba ya baba bado imo mikononi mwa familia. Kwa hiyo usibeze wazo ambalo kwa wengine limewasaidia kuwakomboa na adui ujinga.
Mkuu Jasusi, asante sana kwa kutuwekea wazi mfano huu. Mimi naamini Elimu kwa Taifa ni muhimu sana kiasi kwamba inabidi kila mbinu zitumike ili kuelimisha wananchi. Juhudi zote zitumike ili kupata Taifa lililoelimika. Uwekezaji kwenye jamii jambo muhimu kuliko hata kujenga barabara wanazotutamkia kila siku. Hawa ni wapenda sifa tu. Kutaka kufanya vile wanavyotegemea viitwe majina yao. Wapo ambao hawakuweza hata kungoja watoke madarakani wakayaita majengo majina yao, barabara majina yao. Nilitegemea vitu kama hivi hupewa jina la kiongozi aliyekwisha itikia wito wa mwisho. Kumbe kwetu hata wanaoendelea kula mishahara yetu eti wanamajina yao kwenye majumba makubwa. Hii ni indicator za kupenda kusifiwa bila kufanya yanayostahili kwa Taifa letu. Kiongozi anafanya yanayowaridhisha na kuwanufaisha wenzake chamani anajiona kafaulu. UPUUZI MTUPU!
Wameanzisha shule za kata tukitegemea wana nia nzuri, wakaziacha bila kuziendeleza hadi zimepata jina la utani St. Kayumba! Huku watoto wao wakipelekwa kusoma nje au shule nzuri zenye kila kitu. Hii ni fedheha na ndio udhaifu wenyewe unaozungumziwa. Ni afadhali ukafanya mambo manne tu yakawa safi kabisa kuliko kujikita kufanya vitu mia moja na hakuna hata kimoja kinachosimama imara na safi. Leo hii tunaambiwa kuna fedha kiasi cha $178 milioni zimefichwa na Watanzania kwenye mabenki ya Uswiss. Chama tawala kitawaambia nini wananchi kuhusu hili??? Huu ni UDHAIFU! Kama Raisi yeyote atakuwa Ikulu na fedha kiasi hicho kinahamishwa nje ya nchi basi huo ni udhaifu! (Na hapa sina maana kuwa zote zilitoka kipindi cha Kikwete, lakini Chama tawala ni hicho hicho na ndicho kiliruhusu mambo haya kutokea).
 
Memory ya 1kb haiwezi kubeba faili la 1GB!, Bajeti ya mwaka huu inatekeleza ile ya miaka 8 ilopita! Sasa sijui hii itatekelezwa lini? Selikali dhaifu husama budget in advance!
 
Mkuu Jasusi, asante sana kwa kutuwekea wazi mfano huu. Mimi naamini Elimu kwa Taifa ni muhimu sana kiasi kwamba inabidi kila mbinu zitumike ili kuelimisha wananchi. Juhudi zote zitumike ili kupata Taifa lililoelimika. Uwekezaji kwenye jamii jambo muhimu kuliko hata kujenga barabara wanazotutamkia kila siku. Hawa ni wapenda sifa tu. Kutaka kufanya vile wanavyotegemea viitwe majina yao. Wapo ambao hawakuweza hata kungoja watoke madarakani wakayaita majengo majina yao, barabara majina yao. Nilitegemea vitu kama hivi hupewa jina la kiongozi aliyekwisha itikia wito wa mwisho. Kumbe kwetu hata wanaoendelea kula mishahara yetu eti wanamajina yao kwenye majumba makubwa. Hii ni indicator za kupenda kusifiwa bila kufanya yanayostahili kwa Taifa letu. Kiongozi anafanya yanayowaridhisha na kuwanufaisha wenzake chamani anajiona kafaulu. UPUUZI MTUPU!
Wameanzisha shule za kata tukitegemea wana nia nzuri, wakaziacha bila kuziendeleza hadi zimepata jina la utani St. Kayumba! Huku watoto wao wakipelekwa kusoma nje au shule nzuri zenye kila kitu. Hii ni fedheha na ndio udhaifu wenyewe unaozungumziwa. Ni afadhali ukafanya mambo manne tu yakawa safi kabisa kuliko kujikita kufanya vitu mia moja na hakuna hata kimoja kinachosimama imara na safi. Leo hii tunaambiwa kuna fedha kiasi cha $178 milioni zimefichwa na Watanzania kwenye mabenki ya Uswiss. Chama tawala kitawaambia nini wananchi kuhusu hili??? Huu ni UDHAIFU! Kama Raisi yeyote atakuwa Ikulu na fedha kiasi hicho kinahamishwa nje ya nchi basi huo ni udhaifu! (Na hapa sina maana kuwa zote zilitoka kipindi cha Kikwete, lakini Chama tawala ni hicho hicho na ndicho kiliruhusu mambo haya kutokea).
MpendaTz,
Tukirudi kwenye suala la kuweka dhamana, hivi kweli kuna Mtanzania yeyote atakayetaka nyumba au shamba la wazazi wake lichukuliwe kwa kukwepa kulipa mkopo wa shule? Sidhani. Ila tatizo litakuja kwamba siku hizi wanafunzi wanamaliza chuo kikuu hawana ajira na hawajui waanzie wapi. Na hilo ni suala ambalo serikali inapaswa kulishupalia. Mtu anapomaliza shule na anapata kazi nzuri, kweli itakuwa vigumu kwake kufanya mpango awe anakatwa kiasi fulani kila mwezi kulipia deni lake la shule? Hapa Marekani kuna kampuni, na baadhi ya ofisi za serikali, wanapokuajiri na ukikubali kufanya nao kazi kwa muda fulani wanakulipia deni lako la shule. Na ukitizama jinsi serikali yetu inavyofuja hela kwa semina elekezi zisizo na tija, inaonyesha fedha zipo za kuwalipia wafanyikazi wake ambao walichukua mkopo kujielimisha. Inawezekana.
 
Jasusi,
Hakuna Mkopo Mzuri katika maisha kama wa Elimu. Maana Elimu akishaipata mtu na familia itakayofuata kwake unamategemeo kuwa itaelimika. Zao hilo katika jamii linakuwa na mategemeo ya mwendelezo mzuri.
Kinachosikitisha kwa sasa ni kama ulivyoeleza hapo juu kuwa mtu achukue mkopo halafu akimaliza masomo hana ajira. Huu ni udhaifu wa serikali. Nakumbuka enzi zetu ilikuwa ni jambo liliwekwa kwenye "five year plan" za serikali, kuwa kila mwaka tunaelimisha vijana kiasi hiki na kazi zinakuwepo. Na kwa kuwa ulipata elimu bure basi ulitakiwa kufanya kazi angalau miaka mitatu mahali ambapo serikali imekupangia. Na hiyo ilimaanisha kulipia deni la Elimu. Walipoondoa mapango huo bila kuwa na mpango mbadala nashindwa kuelewa.
 
Sasa kama wanashindwa kusambaza hizo mbolea,rais anawachukulia hatua gani? Yeye si ndiye bosi wao mkuu?!

Kwa namna hiyo kwanini wakulima wasimwone rais ni dhaifu,kwa kuwa anashindwa kuwawajibisha wasaidizi wake.

Tatizo kubwa la Watanzania ni kungoja kufanyiwa kila kitu. Kuna ngazi za kupita na njia za kufanya na matatizo yanaweza kutatuliwa kabla hayajafika kwa Rais, lakini sikusikitikii, bado tuna miaka mingi sana ya kujifunza (wengine wamejaaliwa kujifunza haraka na wengine wamejaaliwa kuchelewa kujifunza).

Ni juzi juzi tu tumefunguliwa kutoka kwenye udikteta ambao tulikuwa hatuwezi hata kuuliza kwanini kandambili hatuna na tunavaa matairi mabovu ya gari. Leo tuna kila sababu ya kutaka Rais atufanyie kila kitu kwa kuwa katufanya tumekuwa tuko nae karibu sana, kabla ya Kikwete, tulikuwa tuko nao mbali sana, hata kumuuliza kitu huwezi. Hii ndio demokrasia.
 
Wanabodi.

Watanzania bado wana imani kubwa na Rais Jakaya Kikwete, kuna baadhi ya watu ambao wanaishambulia serikali ya JK kuwa kuna ufajaji wa fedha za umma, ufajaji wa fedha za umma kwa vigogo wa serikali hayakuanza leo bali tangu serikali zilizopita.

Rais Kikwete amezipa meno na mamlaka za kisheria Takukuru na ofisi ya CAG kuwafungulia mashtaka moja kwa moja mahakamani, Rais ameweza kuvunja hata mtandao mkongwe wa viongozi kulindana na ndio maana hata wabunge sasa wanakamatwa kwa rushwa tofauti na huko nyuma.

Baada ya uchafu wa hesabu fedha za umma kubainika, kwa mara ya kwanza Kikwete kuunda kamati ya ukaguzi inayojumuisha wataalam wa ukaguzi wa hesabu, Takukuru, Polisi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Maofisa Upelezi, Usalama wa Taifa, kwa kutumia ripoti ya CAG wanaweza kubaini wizi, kiasi kilichoibiwa kwa njia gani na wahuisika wote.. Kuna normal auditing (ukaguzi wa hesabu wa kawida) na forensic auditing (ukaguzi wa hesabu unaobaini wizi na vielelezo vya kumshtaki mahakamani mhusika) kwa miaka yote Ofisi ya CAG imekuwa ikifanya ukaguzi wa normal auditing na kugundua uchafu na serikali kukaa kimya na wizi wa fedha umma ulikithiriri sana.

Utaratibu wa forensic auditing Wakurugenzi wengi katika halmashauri zetu wengi lazima wafikishwe mahakamani.

Rais Kikwete kwa muda wake takribani miaka sita ameweza kuvunja rekodi ya ujenzi wa barabara kakamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa takriban kilomita 11,000 kwa kiwango cha lami, ikilinganishwa na kilomita takriban 6.000 tu zilizojengwa na serikali zilizomtangulia, za Mwl Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa.

JF Daima

Na ww ni dhaifu kama Rais wako uwezi kujilinganisha na mtu yeyote. WEWE NI WEWE HAKUNA MWINGINE KAMA WEWE. Hivyo uwezi kushindwa kuwakamata wezi wa Epa, meremeta au kuwadhibu wavuja pesa ya umma eti kwa vile hata marais waliopita walikuwa ivyo. Tumeona udhaifu wako katika kuchangia ni sawasawa na rais wako.
 
Nikisoma vijipost kama hivi vya Ritz huwa nakumbuka Kikwete alivyowasamehe wale wezi wa EPA waliorudisha hela...dhaifu...
 
Kikwete dhaifu, ccm dhaifu, wenye imani na kikwete ni wana ccm, na kamwe si watanzania wote.
 
Back
Top Bottom