Gwalihenzi
JF-Expert Member
- Oct 21, 2011
- 5,125
- 1,300
Tatizo lako unashinda kwenye key bord hutembei huku saiti tuliko wenzako, wenzio tunaoshinda na hawa wakulima tunajua kinachoendelea. Ole wako uje na visuti vyako huku au uwe kwenye gari lenye namba za serikali jaribu kuongea nao au waulize kitu uone hasira zao. Juzi tulikuwa na gari la elimu kutembelea shule moja ya kata tukapotea njia tulipoulizia kwenye kundi la wakulima waliokuwa hapo njiani hatukuamini kama walikuwa ni watanzania wenzetu! walivurumisha mitusi ya nguvu na kutuambia tukamuulize kikwete anayetulipa mishahara. We wacha kabisa.asilimia kubwa wanaomchukia rais wa tanzania, ni vijana ambayo ni jobless tena wengi waliokimbia shule,wanafunzi wanaosomea siasa pamoja na vijana waliotekwa kimawazo na wanasiasa!na sio wakulima kama unavyodai!! Tena vijana wavivu wa dar es salaam ndio wanaongoza kumchukia rais wa jamuhuri ya muhungano wa tz.