SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,616
- 7,863
Miaka mitano ya urais wa JK ndio hiyo inaelekea kuisha. Kuna kila dalili kuwa atapendekezwa na chama chake kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Na pengine akaendelea kuwa Rais wetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika kipindi chake cha uongozi kwa hakika kumetokea mambo mengi tu na mengi mengine yanaendelea kutokea. Kama Rais, JK anawajibika kwa yote yanayotokea (mabaya na mazuri) katika nchi yetu. Kuna mengi ‘mabaya' kumuhusu JK tumekuwa tukijadiliana sehemu mbalimbali hususani hapa JF. Kuna wengine walienda mbali zaidi na kuorodhesha sababu zaidi ya hamsini, ni kwa nini JK hafai kuiongoza Tanzania.
Pamoja na mabaya yake, naamini kuna mambo mazuri amefanya. Kwa kutambua mazuri yake amewahi kutunukiwa PhD (ya heshima) huko Kenya na kuna taarifa kuwa atapewa PhD nyingine huko Uturuki.
Nadhani si vibaya tuanze pia kujadili mazuri aliyoyafanya kwa nchi yake (badala ya kutizama mabaya na kulaumu muda wote!). Unadhani ni kitu gani kizuri amekifanya katika kipindi cha utawala wake?