Rais Kikwete: Nabii asiyekubalika nyumbani kwake?

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,862
Miaka mitano ya urais wa JK ndio hiyo inaelekea kuisha. Kuna kila dalili kuwa atapendekezwa na chama chake kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Na pengine akaendelea kuwa Rais wetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Katika kipindi chake cha uongozi kwa hakika kumetokea mambo mengi tu na mengi mengine yanaendelea kutokea. Kama Rais, JK anawajibika kwa yote yanayotokea (mabaya na mazuri) katika nchi yetu. Kuna mengi ‘mabaya' kumuhusu JK tumekuwa tukijadiliana sehemu mbalimbali hususani hapa JF. Kuna wengine walienda mbali zaidi na kuorodhesha sababu zaidi ya hamsini, ni kwa nini JK hafai kuiongoza Tanzania.

Pamoja na mabaya yake, naamini kuna mambo mazuri amefanya. Kwa kutambua mazuri yake amewahi kutunukiwa PhD (ya heshima) huko Kenya na kuna taarifa kuwa atapewa PhD nyingine huko Uturuki.

Nadhani si vibaya tuanze pia kujadili mazuri aliyoyafanya kwa nchi yake (badala ya kutizama mabaya na kulaumu muda wote!). Unadhani ni kitu gani kizuri amekifanya katika kipindi cha utawala wake?
 
Hajali ubora wa elimu kwa watoto wetu. Natumaini SMU umesoma kuhusu matokeo ya vijana wetu waliomaliza sekondari katika shule zetu za kata. Ni aibu iliyovuka mipaka.
 
Hilo ni sawa. Kuna mazuri amefanya?
Amevunja records kwa kuwa kiongozi wa kiafrica muungwana,mwanademokrasia,anayeheshimu utawala wa sheria,kipenzi cha watu na mwenye uzalendo wa kweli...
Tatizo ni kwamba, anatawala moja ya nchi za kiafrika(tanzania).Waafrika hatujazoea utawala wa aina hii.tumezoea kupelekwa kidikteta.na ukiwa raisi wa aina hii utaitwa DHAIFU,na usiyeweza kutoa maamuzi magumu.
Mkapa benjamin alikuwa akisema neno hata kama ni tusi kwa waandishi wa habari,watu wote walikuwa wanafyata mkia...
that's a kind of president we deserve bcause we are naturally oppressed society
 
Hilo ni sawa. Kuna mazuri amefanya?

Yes, Mh. Kikwete ame-cement kwa upana mahusiano ya kimataifa kati ya Tanzania na nchi mbalimbali duniani. Pia ameonesha ukomavu wa Tanzania kwenye ulinzi wa sovereignty za nchi nyingine kama vile kule Comoros na upelekaji wa majeshi yetu pande mbalimbali zenye migongano under UN.

Ukiachilia hayo ya kimataifa, pamoja na kasoro chache zilizotokea, i.e. kufungia magazeti na kukamata baadhi ya wenye vyombo vya habari, Mh. Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele kuendeleza uhuru wa vyombo vya habari. Nadhani wengi mtakubali kwamba ni mengi ambayo yanaandikika hivi sasa kwenye frontpages ambayo yasingeweza kugusa walau tu middle pages ndani ya magazeti miaka 6 iliyopita. Kwa haya machache namsifu Mh. Kikwete.

Hayo mambo ya PhD mimi naona ni ulimbukeni tu wa kuoneshana fadhila.
 
Amevunja records kwa kuwa kiongozi wa kiafrica muungwana,mwanademokrasia,anayeheshimu utawala wa sheria,kipenzi cha watu na mwenye uzalendo wa kweli...

...

Uzalendo wa kweli ukiwemo kwenye kuuza mgodi wa buzwagi kwa wageni kwa bei ya karanga, kuiba mabilioni ya watanzania kupitia richmonduli na dowans, na na na na kubwa zaidi ... bajeti ya trilioni moja kwa ajili ya stimulus (kilimo kwanza, etc?)
 
Vipi kuhuusu kampeni ya kutokomeza malaria, hata kama haitafanikiwa ameonyesha nia.
 
Dah shame on you man. Jk karuhusu freedom of speech tunayo enjoy hapa

JK hakuruhusu freedom of speech ... hii ni right ya kila mtanzania (in fact kila binadamu) and it has nothing to do with JK.

BTW - unadhani JK hata kama hapendi ataweza kuzuia tunachoandika hapa? The answer is ...... NO.

-- JK ni mtu anayependa sana safari za nje (u vasco da gama), na anapenda sana kwenda nchi za magharibi (mf marekani kwa wiki mbili). Anajua kabisa kuwa akianza choko choko dhidi ya watu kama mimi na wewe hapa JF, hataweza kabisa kufanya utalii kwa "amani na utulivu" kama ilivyo sasa.
 
Vipi kuhuusu kampeni ya kutokomeza malaria, hata kama haitafanikiwa ameonyesha nia.

Kwa nini unadhani haitafanikiwa? BTW - haya mambo ya kuonesha nia yamekuwepo kuanzia uhuru, inatakiwa sasa mafanikio yaanze kuhesabiwa na sio nia tu.
 
Miaka mitano ya urais wa JK ndio hiyo inaelekea kuisha. Kuna kila dalili kuwa atapendekezwa na chama chake kugombea nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Na pengine akaendelea kuwa Rais wetu kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Katika kipindi chake cha uongozi kwa hakika kumetokea mambo mengi tu na mengi mengine yanaendelea kutokea. Kama Rais, JK anawajibika kwa yote yanayotokea (mabaya na mazuri) katika nchi yetu. Kuna mengi ‘mabaya’ kumuhusu JK tumekuwa tukijadiliana sehemu mbalimbali hususani hapa JF. Kuna wengine walienda mbali zaidi na kuorodhesha sababu zaidi ya hamsini, ni kwa nini JK hafai kuiongoza Tanzania.

Pamoja na mabaya yake, naamini kuna mambo mazuri amefanya. Kwa kutambua mazuri yake amewahi kutunukiwa PhD (ya heshima) huko Kenya na kuna taarifa kuwa atapewa PhD nyingine huko Uturuki.

Nadhani si vibaya tuanze pia kujadili mazuri aliyoyafanya kwa nchi yake (badala ya kutizama mabaya na kulaumu muda wote!). Unadhani ni kitu gani kizuri amekifanya katika kipindi cha utawala wake?
Sii,na hawezi kuwa nabii kamwe!!
 
hizo degree anapewa kwa sababu wenzetu wanajuwa economic diplomacy na wanajuwa mzee wetu wa kudesa anapenda ujiko ......wakimpa degree za heshima inakuwa mswano....

......rais weak kuliko wote afrika mashariki na kati ni jk....kinachosaidia hadi sasa hatuyumbi ni misingi mizuri ya syetem ya nchi yetu na despline na professionalism ya vyombo vyetu.......
 
Kusema la haki mnyonge mnyongeni but haki yake mpeni. Kikwete kuna mazuri aliyoyafanya. Mosi hii nadharia ya utawala bora na misingi ya utawala bora isingelikuwapo ndani ya midomo yetu isingelikuwa kuwapo kwa uhuru wa vyombo vya habari (Big Ben alikuwa akisikia umemsema anatuma majasusi kukumaliza). Ndio maana hii leo tunaweza kuzungumza EPA, Import support, Radar ni kwasababu ameruhusu transparency katika utawala wa serikali.

Pili amepitisha muswada wa kuseparate biashara na uongozi ambacho kimesaidia kupunguza walafi serikalini. Hii itasaidia hata wabunge wajao wafikirie waendelee na uongozi wa ubunge au wafanye biashara. Kwa hilo nakubaliana nae sana tu na namuombea lifanikiwe tutapata kuondoa pathetic leaders kama kina Lowassa katika serikali ambao wanakaa kwa maslahi yao binafsi.

Tatu infrastructure economy nani asiyeona idadi ya barabara zilizojengwa dar acheni kumsema huyu mbagamoyo kuna barabara kibao kilwa road kwenda mbagala, vingunguti, mikoa ya kusini lami tupu kitu ambacho kinasaidia uchumi wa nchi. Upanuzi wa bandari utakuza uchumi na pamoja viwanja vya ndege. Nia na madhumuni ni kwamba Tanzania iwe ni business centre. Just ask yourself why?? Tizama ni nchi iliyokuwa na financial and political stability in the past decade kwa east and central africa. Jibu unakuta ni bongo tu. Tizama the amount of FDI zilizowekeza Tanzania compare to the rest of East Africa. Kwa kweli amejitahidi but nadhani amekosa watu innovative kujaribu kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwani pamoja na mafanikio haya yamekuwa overshadow na viongozi walafi ambao wanafikiria kujinufaisha wenyewe without kuangalia wananchi matokeo yake pesa nyingi za maendeleo zinaenda mifukoni mwa watu.

Tuje katika social welfare. Recently BOT walipewa pesa na World Bank kwaajili ya kuendeleza makazi mazuri ya mtanzania wa kawaida na kipato cha chini. Hizi pesa kama zitatumika inavyotakiwa na kutakikana basi makazi ya wananchi wa kawaida yataboreka (na sio makazi ya wafanyakazi wa BOT na mabosi wao). Kimsingi kama watatumia hizi pesa inavyotakiwa maisha bora ya mtanzania yatakuwapo na sio hivi sasa. Pia matumizi ya IT (Information Technology) ni jambo la kupewa heko kwani itaboresha mawasiliano, biashara na huduma za kibenki.

Hayo ni baadhi tu mengineyo watajazilia wengine ila tatizo la Kikwete ni anashindwa kuweka msimamo wake na ndio kitu kinachofanya mafanikio yasionekane. Katika uongozi kama maisha kuna watu watakupenda na wengine kukuchukia but la msingi tanguliza misimamo yako. Kikwete anaogopa kuudhi watu akihofia ubadhirifu wa kiongozi but hilo ndio linalopelekea kukosekana uadilifu katika uongozi, watu kutoona mafanikio yake na mwishoe kudharaulika maana haongozi bali anaongozwa. Kikwete angelitanguliza misimamo yake wasingelikuwapo mawaziri wabovu kama akina simba kwani angelichagua mawaziri wanaokabiliana na misimamo yake na sio vengine. This I hope kama atachaguliwa tena 2010 hatalirudia ama sivyo atakumbukwa na legacy ya kiongozi asiyekuwa na msimamo !!!!
 
Ile phd ya kenya hakuna kazi aliyofanya..waliofanya kazi kubwa ni annan,mkapa na graca....yeye aliitwa siku ya kusaini..in his capacity as au chairman by then.......it was not a big deal at all.....na angekuwa ana akili ile phd angeipokea na ku dedicate kwa annan na kamati yake....kama kuonesha heshima kwao.....ange prove u falsafa....
 
hizo degree anapewa kwa sababu wenzetu wanajuwa economic diplomacy na wanajuwa mzee wetu wa kudesa anapenda ujiko ......wakimpa degree za heshima inakuwa mswano....

......rais weak kuliko wote afrika mashariki na kati ni jk....kinachosaidia hadi sasa hatuyumbi ni misingi mizuri ya syetem ya nchi yetu na despline na professionalism ya vyombo vyetu.......

Phd ya uheshima inategemea kaka but ni kweli wanamfagilia ili wapate uranium waarabu hao wajanja sana.
 
Ile phd ya kenya hakuna kazi aliyofanya..waliofanya kazi kubwa ni annan,mkapa na graca....yeye aliitwa siku ya kusaini..in his capacity as au chairman by then.......it was not a big deal at all.....na angekuwa ana akili ile phd angeipokea na ku dedicate kwa annan na kamati yake....kama kuonesha heshima kwao.....ange prove u falsafa....

Kaka umesahau kuwa Brown alimuita Kikwete wakati akiwa kiongozi wa AU wajadiliane wakati zilipofumuka hizo fujo Kenya. Ingawa hatujui walichozungumza but inawezekana yeye ndie aliyependekeza Koffi anan, Mkapa na Graca waifanye hiyo kazi na bear in mind wote hawa watu wanaipenda sana Tanzania kwa sababu ya effort za baba yetu wa taifa Mwl Nyerere hivyo basi wangeliitikia wito wakiombwa. Sasa ambaye anajukumu la kuwaomba ni rais Kikwete hivyo I think he deserve a credit for that!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom