Rais Kikwete kuzungumza na Wazee wa Dar jioni ya leo (Nov 18, 2011)

Status
Not open for further replies.
sitegemei jipya toka kwa huyu jamaa.....ameona mambo hayaendi sawa sasa anataka kubadilisha upepo
 
Hawa wazee ndo wanapigwa mabomu wakisotea malipo yao ya jumuiya ya Africa Mashariki. Lakini kwa kuwa wameshaanza kupoteza kumbukumbu, wakitangaza vijana watawakumbusha hivyo hawataenda.

Kama hawa wazee wana busara waache kwenda au kama wana umoja, huu ni muda mzuri kwenda na kugoma kuhutubiwa na wao wakamuuuliza maswali juu ya malipo yao.

Wazee wanaopigwa mabomu sio hao. Hawa wa JK ni wale wacheza bao, karata tangu asubuhi hadi jioni wakishindana kuhusu ujuaji wao wa matajiri wa kiarabu. utasikia 'Bakhresa kanunua hiki au kile; Mohammed trans ana magari mengi; Islamu anaongoza njia ya morogoro etc
 
yeye hata aseme vipi anachotakiwa kujua ni kwamba wananchi wengi hawamtaki......kama anaona kinga yake iko kwa hao wazee na anatafuta public sympath sis wengine hatufai hata kidogo.....aongoze hao hao wazee
 
Kwa wale wanaopanga maandamano kuhusu katiba mpya, hamuoni kuwa hii ni fursa ya kuitumia kuanza kumpelekea mheshimiwa ujumbe, hata mkamsuburi hapo getini na mabango ya kupinga jinsi mchakato wa katiba unanyoendeshwa.
 
Watanzania wana hula ya ajabu sana. Vita ya ufisadi ilianzia JF na media then cdma na vyama vingine hata CUF na NCCR wakiwamo na TLP piaM baada ya JK kusikia na kuunga mkono, watu wamemgeuka na sasa wanamtetea Lowassa na kundi lake kama hawana akili nzuri. Suala la katiba nalo pia, sasa mambo yamekua kinyume kabisa, tunataka yashuke toka mbinguni bila kuundwa chombo cha kusimamia mchakato.

JK amekasirika sana na hatuelewi Watanzania tunataka nini, maana kila kitu tunapinga.
 
Nini MAANA YA kuzungumza na mtu niujua vyo mimi ni kubadilishana maneno,JK Hana uwezo wa kuzungumza na Watanzania hawa wenye shida na ugumu wa maisha wanaibiwa Mali ya umma bila mtu kushitakiwa,wanaiba wanyama hai bila hata Mtu kuwajibika.

Kama kweli JK ANAUBAVU ITISHA MKUTANO WA TWO WAY MIC KWAKE MIC KWA WANANCHI TUMUULIZE MASWALI KWANINI TUMEFIKA HAPA TULIPO, anakimbilia kuwahutubia wachovu wazee wa Dar wanaomwogopa.

Kwanini asizungumze na wazee wastaafu wa EA?
Hao wananchi wanaibiwa na nani? Mbona humu ndani tunawatetea wezi? Mbona makanisa yanaanza kuwatetea wezi? Eti wasiogope kuitwa mafisadi? Leo mafisadi si tatizo tena? Uko wapi ule waraka wa kanisa unaopinga ufisadi? Kuna nini?
 
Naona kwa siasa za bongo marais ni mwiko kutoa hotuba za kitaifa kupitia vyuo vikuu!
Hata waliomtangulia ukimtoa Nyerere hawakuwa na huo utaratibu kabisa, hii mbaya sana mbona hzo nchi wanazoshinda kuzurura huko na kutembeza bakuli wenzao hotuba za msingi za kitaifa zinafanyikia vyuo vikuu??
Hii na wazee wa dar si kwa zama hizi tena, jamaa ameshindwa kwenda na beat.
Hamna kitu hapo!
 
Mheshimiwa Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete leo ataongea na wazee wa Dar-es-salaam kuanzia saa kumi jioni. Itarushwa live na vituo vya TV kama TBC.

USIKOSEEEEEEEEEEEEEEEEE.


Kuzungumza na wanachama wa ccm na sio wazee wa DSM
 
Hapa kuna kitu kipo nyuma ya hiki anachotaka kuzungumza na kuna uwezekano mswada ukapita kwa 100% huku yeye Jk akijifanya kuupamba huu mswada kwamba una manufaa kwa waTz,da kweli nchi imekosa dereva na muda wowote gari itapinduka
 
Si mbaya kwa rais kufikisha ujumbe kwa adhira kupitia wazee,ila je ni wazee wa aina gani atakaongea nao?si kua nawatusi wazee atakao ongea nao la hasha,pili kama ni ataongelea suala la katiba pia,kwa nini iwe wazee tu na si wanaharakati,wanavyuo,walimu wa level zote,wawakilishi wa jukwaa la katiba wananchi wa kawaida nk?
 
Hao wananchi wanaibiwa na nani? Mbona humu ndani tunawatetea wezi? Mbona makanisa yanaanza kuwatetea wezi? Eti wasiogope kuitwa mafisadi? Leo mafisadi si tatizo tena? Uko wapi ule waraka wa kanisa unaopinga ufisadi? Kuna nini?
makanisa ya siku hizi yamejaa wanafiki watupu kama bakwata tu

hawa viongozi wa dini wanaongoza kuua dini nchini
 
Rais wetu amekuwa na kawaida ya kukutana na wazee at times of pressure like this, ni anatafuta baraka za wazee au ndo kama kawaida yake kwenda kuwamwagia sumu wananchi kupitia kwa wazee. Ngoja tuone leo ana kipi kipya zaidi ya his handsome face!!
 
Lakini ujumbe unatufikia wote..atakayoongea hawalengi tu wazee..bali taifa kwa ujumla. Wazee wantumika tu kama sample ya hadhira

Mbona kila mara ana sample Wazee na si Vijana? Au ndo ile vijana wa leo, Taifa la kesho?
 
makanisa ya siku hizi yamejaa wanafiki watupu kama bakwata tu

hawa viongozi wa dini wanaongoza kuua dini nchini

Kweli na hakika, Waabudu mashetani wapo humo Makanisani na Misikitini, tena ni Wachungaji, Mapadri, Maaskofu na Mashekhe, Maimamu.

Mafirauni na wazinzi wakuu ndio wenyewe.
 
Mheshimiwa Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete leo ataongea na wazee wa Dar-es-salaam kuanzia saa kumi jioni. Itarushwa live na vituo vya TV kama TBC.

USIKOSEEEEEEEEEEEEEEEEE.

Inaposemwa kuwa anaongea na wazee si kweli,
ingesemwa kuwa anawahutubia kwa kuwa kuongea
ni pamoja na kupeana nafasi ya kutoa hoja kama
vile yeye kusikiliza hoja zao na kuwaacha waulize
maswali kisha ayajibu. Lakini kinachofanyika ni
kwamba yeye anasema wao wanapiga makofi tu
bila kuhoji...
 
Nendeni mkamsikilize, sina muda huo. Kwani tangu ameingia awamu ya pili amefanya nini cha maana hadi nipoteze muda wangu kuchungulia TV.

Zaidi sana gharama za maisha zinakwenda juu kila uchao kwa kasi zaidi.
 
Inaposemwa kuwa anaongea na wazee si kweli,
ingesemwa kuwa anawahutubia kwa kuwa kuongea
ni pamoja na kupeana nafasi ya kutoa hoja kama
vile yeye kusikiliza hoja zao na kuwaacha waulize
maswali kisha ayajibu. Lakini kinachofanyika ni
kwamba yeye anasema wao wanapiga makofi tu
bila kuhoji...

Sawa mkuu, anaenda kusema ya moyoni mwake, wazee watapata nafasi ya kupiga makofi na akina mama kurusha vijembe kwa CHADEMA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom