Rais Kikwete kuzungumza na Wazee wa Dar jioni ya leo (Nov 18, 2011)

Status
Not open for further replies.
Hana Jipya!!!!
Magamba yamemshinda ataweza kuzungumza hoja zenye mashiko? Anataka atupige changa la macho kuhusu katiba.
Msanii, simuamini!
 
Mheshimiwa Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete leo ataongea na wazee wa Dar-es-salaam kuanzia saa kumi jioni. Itarushwa live na vituo vya TV kama TBC.

USIKOSEEEEEEEEEEEEEEEEE.

Why not wanazuoni......au hawapigi makofi hovyo kwenye ngonjera na vibwagizo visivyo na tija kwa taifa??
 
Halafu akiongea na vizee hivi vya CCM huwa anatema povu sana huyu bwana!!

anakusanya vizee vya wa2 akivinunulia kahawa bas amevimaliza kila ki2 vitabaki kupiga makofi na kuitikia NDIYO MZEE.

kwanin asikusanye vijana,wanaharakati au hata wasomi. Anaongea nawazee ambao mtazamo wao haufiki hata 2yrs?
 
Nimesikia mweshimiwa dr jana au leo asubuhi kaenda Dom? Sasa jioni anarudi tena? Halafu kesho anaenda tena dom kwenye mkutano wa ccm? Duuh kama ni hivyo mzee anakula nchi sana,
 
Mheshimiwa Rais Dr Jakaya Mrisho Kikwete leo ataongea na wazee wa Dar-es-salaam kuanzia saa kumi jioni. Itarushwa live na vituo vya TV kama TBC.

USIKOSEEEEEEEEEEEEEEEEE.
Hotuba yake inapaswa kujibiwa instantly!! Tunahitaji mtu smart ataeweza kuandika majibu ya hoja zake pale pale anapozungumza ili majibu yatoke kesho sambamba na hotuba yake itayotolewa na vyombo vya habari!! Lakini pia akili pia tuziweke na dodoma,ili akili zisihamie kwenye hotuba huku bungeni mambo yanapitishwa! Wananchi wengi hawataona kinachoendelea bungeni live maana watakuwa wanasikiliza porojo!!
 
kwa nini wazee tena wa DSM???hawa ni rahisi kuhongeka ghahawa
akaongee udsm tutamwelewa tu
 
Ndiyo tatizo la kiongozi huyu. Mambo mazito yanayohitaji wasomi, yeye anaongea na wauza kahawa. Wapi na wapi!!
 
Hao wazee si ndiyo aliongea nao kipindi kile kuwa hatapandisha mishahara wakashangilia. Matokeo yake ni shida mpaka leo. walijisahau kuwa wtoto wao au wanaowategemea ni wafanyakazi. Sitegemei kipya zaidi ya kuongelea CHADEMA
 
wale wazee ni noumer.leo mtaona vituko vyao, yaani hata akiongea pumba wao ni kushangilia kupiga makofi na vigeregere.hawa wazee washarogwa ndo maana anawatumia kama boya.kwanini asiongee na wazee wa mwanza au Arusha?sio kweli kwamba akiongea na wazee wa dar anakuwa anaongea na watanzania bali wana ccm, kwa sababu wale wazee leo jioni utaona watakavyotinga ndani ya nyumba na kanga za ccm na kofia za yanga.mia
 
Ndiyo tatizo la kiongozi huyu. Mambo mazito yanayohitaji wasomi, yeye anaongea na wauza kahawa. Wapi na wapi!!
Mkuu hushangai kwanini inafanyika sambamba na mkutano wa bunge ukiendelea? Subiri muone! Hapa wanaharakati ndio wanapaswa kufikiri kwa kasi and very smart!!
 
Nini MAANA YA kuzungumza na mtu niujua vyo mimi ni kubadilishana maneno,JK Hana uwezo wa kuzungumza na Watanzania hawa wenye shida na ugumu wa maisha wanaibiwa Mali ya umma bila mtu kushitakiwa,wanaiba wanyama hai bila hata Mtu kuwajibika.

Kama kweli JK ANAUBAVU ITISHA MKUTANO WA TWO WAY MIC KWAKE MIC KWA WANANCHI TUMUULIZE MASWALI KWANINI TUMEFIKA HAPA TULIPO, anakimbilia kuwahutubia wachovu wazee wa Dar wanaomwogopa.

Kwanini asizungumze na wazee wastaafu wa EA?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom