Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.
Rais JK anatarajia kuzungumza na wazee wa Pwani leo saa 10 jioni. Je ni mambo gani anayotarajia kuzungumza na wazee hao?
 
Refer hotuba JUU YA MGOMO WA wAFANYAKAZI aka MBAYUWAYU!
Itakuwa ni copy and Paste ya ile!
 
Ingawa utu uzima ni dawa, lakini huwa wananiudhi wanapopiga vijembe, vigele gele na kuzomea. Huwa najiuliza, wanatufundisha nini na sisi tutakapokuja kuwa wazee wa Dar es Salaam?
 
Nimesahau head phone yangu lakini hakuna cha maana hana jipya ataenda kucheka cheka tu pale apigiwe makofi basi. Lakini nimpe ushauri wa bure anapokimbia wanaompinga akaongea na hao mafisadi wastaafu akajidanganya ameungwa mkono analiua taifa. Ee bwana watu muhimbili wanakufa kama hujui kufa nenda kazubae zubae mle ndani uone.
 

quote_icon.png
By Pasco
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.




Mkuu Companero, kwani mimi Salva mpaka nijue?. Au na wewe unadhania na mimi ni mtu wa sehemu?. Mimi ni mwananchi tuu kama wewe, naisubiri hotuba hiyo ili niongeze katika mazuri ya JK au mabaya!.

Pasco,

With your due respect hapa umechemka tena babu kubwa!!!

Kwa akili ya kawaida tulitegemea mtu kama wewe ujadiri namna ya kuumaliza huu mgogoro na si nani atakomolewa hapa. Hivi wewe kweli unaona Rais kwenda kuongea na the so called wazee wa Dar ambao wengi wetu hatujui huwa wanaalikwa kwa kufuata utaratibu upi kwa kuwa wazee wetu hawaalikwi wakati nao ni wakazi wa Dar. May be mwenzetu Mzee wako huwa anaalikwa pia!!

Yaani kwa vile Nyerere aliongea na wazee miaka ya sabini, Mwinyi akaongeanao miaka ya Themanini, Mkapa akafanya hiyo miaka ya 90, bado tu mwaka 2012 Rais anatumia mtindo huo huo. Hii inaonyesha ni jinsi gani viongozi wetu wasivyo na ideas bali ni kucopy copy tu. No wonder uchumi wetu unadorora kila siku................. viongozi hawana new ideas bado wanaendesha uchumi wetu kama alivyofanya Julius miaka ile!!!

Kugoma wagome madaktari, kuongea aongee na wazee wa Dar................ Hiyo ni akili kweli?? Mbona last time alimtuma Pinda aongee nao?? Ninachokiona hapa atatia mafuta kwenye moto especially kama atatumia ile lugha aliyotumia kwa akina Mgaya!!! Asifikiri madaktari ni walimu au akina Mgaya!!
 
Mkuu JK haendi kuongea na "wazee wa CCM" DSM pekee isipokuwa anaongea na Taifa kupita "wazee wa CCM SDM" na hata wakiwa one side kuna athari gani labda?
Labda nikukumbushe JK anweza kuongea kuhusu taifa hata kama yupo kwenye vikao vya chama acha "wazee wa CCM DSM" Sijui unatatizwa na nini hapo


Mkuu "mkakakmavu wa fikra" unafikiri JK anakwenda kujadiliana na wazee wa dsm? NOPE
You're wrong Jk atalihutubia taifa kupitia wazee wa DSM. hivi hili lina ugumu gani kuelewa jamani.... kila nchi ina utaratibu wake. kama wewe unaona ni mazoea mabaya sio mbaya sema basi ubaya wake ni nini maana watu wameacha kuongea nataka kusema nini na taifa wamekomalia wazee tu utadhani hao wazee ndio wana hitimisho lolote, ni utamaduni tu na hauna ubaya wowote

Tunaona ugumu kuelewa mantiki ya kuongea na Taifa kupitia wazee wa Dar. Tungemuelewa kama angeongea na waandishi wa habari au madaktari wenyewe ili aweze kuulizwa na kujibu maswali. Kama ni kuutubia tu basi angefanya hivyo kutokea ikulu na si kutumia pesa zetu kukusanya wazee wa kumpigia makofi!!
 
Hivi hayo ni mazungumzo au hotuba? Maana sijawahi kuona hao wazee wa CCM wakijibizana nae au wanafanya hivyo kabla ya hiyo hotuba?
 
Rais JK anatarajia kuzungumza na wazee wa Pwani leo saa 10 jioni. Je ni mambo gani anayotarajia kuzungumza na wazee hao?

Ina maana imetangazwa kwamba anataka kuzungumza na wazee wa "pwani" au ni msukomo wako wa kibaguzi ndio uliokufanya useme "wazee wa pwani?!"
 
wakuu nadhani kuna haja ya kukomaa aongee na sisinvijana pia, maana baada ya kutulagai sana 2005 tukamtia ikulu,hakuna kuhutubia ni kumpiga maswali magumu mwanzo-mwisho
 
Rais Jakaya Kikwete anahutubia wazee wa Dar es Salaam leo.

Zipo tetesi kuwa lipo kundi la wanaharakati linalowanunua baadhi ya
wazee hao ili wamzomee Rais ukumbini. Kundi hilo la wanaharakati
ni mpango unaosimamiwa kwa karibu na Ananilea Nkya na Hellen Kijo
Bisimba.

My take: Huu ni uchochezi na zomea zomea haina maana yoyote,
wamuache Rais ahutubie ili tujue anayotaka kuzungumza kwa wananchi
kupitia wazee hao.
 
Mkuu Mag3
Ninacho danganya hapa ni kipi hasa? Nimejaribu kueleza
(1)kwanini marais hadi leo wanaongea na taifakupitia wazee wa DSM.
Issue hapa sio namna na uwezo wa kila raisi anavyoweza kudeal na matukio mbali mbali , HAPANA
(2)Issue hapa ni kwamba Rais anataka kuongea na Taifa, haijalishi ana maamuzi au hana.

Ninacho shangaa mimi ni kwanini basi iwe nongwa kufanya hivyo kupitia wazee wa DSM hata kama karibu wote ni CCM(na sababu za kuwa CCM nimeeleza)
Rais habanwi wapi pa ku address maswala ya kitaifa jamani hata kama atakachoongea leo ni ujinga wa kiasi gani lakini hii haiondoi
(3) mantiki nzima ya yeye na mahali pa kuongelea

Hivi umejiuliza what it make a difference kama angeongea anayotaka kuongea akiwa ziarani Bukombe au akijifungia ikulu na makamera na au popote pale na akiongea kupitia wazee wale?
(4)Kwanini hoja kuu iwe kuongea na taifa kupitia wazee wa DSM? je wana impact gani kwa atakachoongea

Vipi kama akisema ameamua kuvunja bara la mawaziri au ameamua kujiuzuru? vipi kama ameamua kuwatimu akina Mponda na naibu wake? vipi kama akisema na kupiga mkwara kama waliopigwa walimu?
(5)hivi hayo yote yana impact gani na hawa wazee tunao watolea matusi yote humu ndani utadhani wao ndio waamuzi wa mwisho au sijui vipi

Mkuu hebu nishawishi nini mbaya kuhutubia taifa kupitia wazee wa DSM? may be I miss something katika hili
Narudia siridhiki na utendaji wake hata kidogo, alikuwa kimya tuka mtaka aongee, akaamu OK nitaongea na taifa kupitia wazee wa DSM sasa tunahoji kwanini wazee wa DSM? au kwasababu wengi ni wana CCM?

1. Naona una akili sana tu the way you argue but the problem with you is that YOU ARE NOT A FREE THINKER........
Hivi ni kweli huoni doubts na questions humo kwenye red????

2. Jamani tunamuheshimu sana huyu Rais wetu ila kila analolifanya lina impact kubwa sana kwenye fikra zetu na maisha yetu kwa ujumla wake sisi kama wananchi. Sasa kunapokuwa na maswali mengi namna hii hapa nyie mnaomtetea bila kujibu haya maswali kwa kweli hamjengi na mnajua kuwa hamjengi na nawachukia kwa sababu you are consciously destroying the status quo......kweli wewe huoni walakini kwenye bolded lines????? Are you serious????

3. Kwa status hiii kwa taarifa yako hata style ya nguo na rangi atakazovaa leo wakati wa kuhutubia zina maana sana kwa scene hii sasa kama na hili haliingii vichwani mwa baadhi ya watu pia hili ni tatizo achilia mbali haya ambayo tayari yameleta mjadala kama hili linaloendelea

4. Watu wako sensitive and very much expecting na lolote linalomuhusu RAIS kipindi hiki kama ambavyo wananchi walikuwa muhimu sana kwake kipindi cha kampeni na uchaguzi......give and take (RECIPROCITY) principal ndo inatawala sasa........it is a DELICATE situation and thus it needs no HOOKS to handle
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom