Rais Kikwete kuzungumza na wazee wa CCM Dar leo jioni!

Status
Not open for further replies.

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
..JK mambo yameanza kumfika shingoni kesho atatafuta huruma za wazee kwa kuongea nao jijini DSM saa kumi jioni.Bila shaka hawa watakuwa wazee wa CCM tu.

Tutakumbuka kuwa JK alifanya hivi wakati mgomo wa walimu chini ya TUCTA ulipotangazwa..na hapa ndipo ile kauli ya akili ya mbayuwayu changanya na ya kwako ndipo alipoitoa.

Mgoja tuone..tutegemee hotuba yenye kujaa hoja zenye kutaka huruma za wazee dhidi ya matatizo mengi yanayoisumbua hii nchi kwasasa.

SOURCE:CHANNEL TEN
 
Kesho jioni JK anategemewa kuongea na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam..


source: Channel Ten

 
JK mtu wa ajabu, badala ya kukaa na kuzungumza na Drs yeye ameamua kwenda kusema na Wazee wa DSM kesho jioni.

Chanzo: NEWS Channel Ten
 
Kesho Rais kikwete ataongea na taifa kupitia wazee wa Dar kuelezea mambo mbali mbali yanayolihusu taifa. source Ch 10 news
 
Habari hii imetangazwa na kituo cha channel ten katika taarifa ya habari ya saa 1 usiku leo hii. Chanzo kinasema ataongelea mambo mbalimbali yanayoihusu nchi .Je anaongelea Mgomo wa Madaktari? Kwanini asiongee na madaktari je wazee wa Dar ni walewale makada wa CCM?
Nashindwa kuelewa hili ngoja kesho apigiwe makofi na wazee wa CCM.

kweli viongozi tunao
 
..JK mambo yameanza kumfika shingoni kesho atatafuta huruma za wazee kupitia kuongea na wazee wa DSM hawa watakuwa wazee wa CCM tu saa kumi jioni.

SOURCE:CHANNEL TEN

Yaani magamba wazee katika chama chake! Asichanganye wazee wote hapa Dar kuwa na mawazo kamo hao wazee wanaopioga makofi katika kila kitu -- na ndo maana wamelifikisha taifa lilipofika.
 
mbayuwayu speech.........kesho analitibua

Wale wazee ningekuwa daktari siwahudumii wanaenda kujaza ukumbi na wanasinzia wanaashwa pale makofi yanapopigwa nao wanajikuta wanapiga makofi bila kujua wanapigia nn.

Kuna haja ya kuwakusanya wote na kuwatupa mto ruvu
 
Huyu m-kwere ana matatizo gani lakini? alipogombana na Mgaya akaenda kumsuta kwa wazee wake wa CCM Dar, sasa kesho anaenda kuwasuta Dr Namala na Ulimboka. hapo ndo mgomo utaisha??? kweli tunaye RAHISI wa Nchi!
 
..JK mambo yameanza kumfika shingoni kesho atatafuta huruma za wazee kupitia kuongea na wazee wa DSM hawa watakuwa wazee wa CCM tu saa kumi jioni.

SOURCE:CHANNEL TEN
Ngoja tutege sikio labda anataka kujivua gamba....
 
Akiwasema tu madaktari itakula kwake. Kuna taasisi zingine ziko tayari kugoma pia kama hana habari. Huyu mjamaa ana ana washauri wa namna gani? Ndiyo mwisho wake.....
 
Sio wazee wa dar. Ni magamba makongwe

Wale wazee ningekuwa daktari siwahudumii wanaenda kujaza ukumbi na wanasinzia wanaashwa pale makofi yanapopigwa nao wanajikuta wanapiga makofi bila kujua wanapigia nn.

Kuna haja ya kuwakusanya wote na kuwatupa mto ruvu
 
Kesho ni siku ya hotuba kama ile ya mbayuwayu!. Madokta ambao hawatarejea kazini baada ya hotuba ya kesho, chamoto watakiona!. Yaani watakiona kisa cha mtema kuni, kilichomnyoa kanga manyoya!.

Naisubiri kesho kwa hamu kumsikiliza rais wetu JK ambae ili nijue nitaongeza post kwenye thread ya mazuri yake au mabaya yake!.
 
Nina Babu yangu anamiaka 75 nimemuuliza kama kapata mualiko wa JK kasema hajapata. Nimemuuliza kama yeye ni mwanachama wa Jumuhia ya Wazazi wa CCM Kasema si mwanachama na wala hawajawai kuwa mwanachama wa hiyo Jumuhia. Basi nikawa nimepata jibu la hao wazee wa CCM.
 
Ngoja tutege sikio labda anataka kujivua gamba....

Hapana. washauri wake wamemwambia aonyeshe jeuri ya kuwarudisha Nyoni na Mtasiwa! Nyie ngojeni tu. Marais wote waliomtangulia hawakuwahi kufanya kitu ya namna hii.
 
Sasa wazee watamsaidia ushauri gani kuhusu mgomo wa madaktari? Kweli Jk ameishiwa uwezo wa kufikiri
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom