Watu wa Kurugenzi ya Ikulu wamezoea lugha za mipasho.Hivi kulikuwa na haja ya kusema hotel maalum? Kwa nini wasingesema atahamia hotelini. Ingekuwa hotel maalum kama ingekuwa imetengenezwa kwa ajili ya JK tu au kwa ajili ya wagonjwa wa aina yake tu.
Prostate/prostrate!!!hah hah hah!!
umeongea neno!maana watu wanabwabwaja tu na lawama nyingi.kwa hadhi na status yake anastahili kwenda popote kutibiwa.nyie mnaopinga rais kutibiwa marekan kama kwel ni wa zalendo huwa mnaenda kutibiwa hospital za kwenye kata zenu?jibu ni hapana.kila mtu huwa anatafuta pale anapoona patastahili kupata huduma kutokana na hadhi yake.tuache siasa wakat mwingine tuongee ukweli.
wambandwa... hit me with your email.... kwanza kabla ya kufikiri ni jinsi gani tutatununua.. tunahitaji watu waliojicommitt. Halafu kwa pamoja tutaamua ni jinsi gani tutafanya hili liwezekane.
Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea
Na hisi umekosa kazi ya kufanya mkuu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume(prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.
Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.
Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.
Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2014
Ngoja nimtext mkulu sijui atanijibu nimeona tumewekewa namba hapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.
Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.
Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.
Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2014
...anaendelea na matitabu yake ......anatarajiwa kutoka wodini ....na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
....tezi dume (prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.
.......mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, ........leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum ......
Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote.
Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.
...... imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.
...
Hilo tatizo si dogo kama tunavyoaminishwa.
Hata mie nimeanza kushtuka aisee,mkuu wa Nchi anaweza kuwa anaumwa sana,isije ikawa mambo ya king cobra sasa!!!
sio dogo hata chembe
Hii sio cancer lakini ? Maana yule dokta ni bingwa wa mambo hayo ? Na kama imeshamuenea mwilini na wamechelewa kuiwahi ndio tumuombee dua tena au keshakolimbiwa mtu hapa ,tunabaki kuchezeshwa gwaride tusilolijua ?
Taarifa muhimu sana hii , lazima tujue kiongozi wetu mkuu anaendeleaje na yuko wapi.
Wanabodi,
Haya shime Watanzania, tuweke tofauti zetu pembeni, tutume ujumbe mfupi wa maandishi kwenda number +1-646-309-2295, kumpa pole Mpendwa rais Wetu, Prof, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, apate nafuu, apate uponyaji wa haraka na kurejea nyumbani salama uu salmini, kuja kuendelea na juhudi zake za kulijenga hili taifa letu changa!.
Mimi ni miongoni mwa waumini wakuu wa kitu kinachoitwa "will power!" yaani ukidhamiria jambo kwa dhati, jambo hilo, linakuwa kama ulivyolidhamiria. Yaani "where there is a will, there is a way!".
Unaweza kunisoma hapa [h=3]Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Kila Jambo na Linatokea!. Wengi wanazo Lakini Hawajijui!.[/h]
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Ni Nguvu za Uponyaji Kwa Kudhamiria!.
Hivyo Watanzania tuko zaidi ya milioni 45, kati ya hao, milioni watu milioni 30 wana simu za mkononi, hivyo kama kila Mtanzania mwenye simu ya mkononi, akituma ujumbe mfupi wa maandishi SMS kwenda namba +1-646-309-2295 ili kupa pole JK, kwa uchache atapata jumla ya pole milioni 30!. Will power ya hizi sms milioni 30!, sii haba!.
Natoa wito kwa makapuni yote ya simu za mkononi mchini, kutoa tangazo la Kutuma SMS kwenye number +1-646-309-2295 kwa madhumuni ya kupa pole rais, iwe ni bure!, ili kuwawezesha Watanzania kuonyesha upendo kwa rais wao, (haswa kwa kuzingatia ile precedence ya kumbukumbu ya Hospitali ya St. Thomas ya London, na ile reference ya majuzi ya jirani zetu wa Zambia!), Watanzania katika umoja wetu, utaifa wetu, bila kujali tofauti zetu za kisiasa, tofauti zetu za kidini, tofauti zetu za kikabila, tofauti zetu za rangi, tofauti zetu za jinsia, tofauti zetu za kiuchumi, yaani matajiri, masikini, wenye vocha kwenye simu zao, wasio na vocha, wote kwa pamoja, tumtumie JK SMS ya kumpa pole na kumtakia uponyaji wa haraka.
Tangazo la number hii +1-646-309-2295, limetolewa na jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ambapo sio tuu wametuahidi kuwa rais JK atazisoma SMS zote, bali pia Rais JK, atazijibu SMS zote!.
Kwa kuanzia mimi nimeishatuma SMS yangu, ilikuwa hivi!.
"Dear Mr. President, Pole Sana!, Get Well Soon!.- Pasco wa JF.
NB. Nimekutafuta sana bila mafanikio!, watu wako wananiwekea kauzibe!, natumaini kwa SMS hii sasa nimekufikia!. Ukirudi naomba nikuone, nina taarifa muhimu sana!". Get Well Soon!.
Pasco.
NB. Ila pia wanaodhani this is nothing, wajue this is not nothing!. Bulky SMS Milioni 30!, kwa kuzingatia kura za ushindi 2010 zilikuwa ni milioni 5 tuu!, hebu tumpeni pole rais wetu, tumtakie uponyaji wa haraka!, na akiisha rejea, tumsikilize kwa makini na kuyatekeleza yale yote Rais wetu
Mpendwa, atayo tuelekeza tuyatekeleze, Mwezi April, na Mwezi October, 2015!.
Ukiwa Rais wewe unafikia Hotel Maalum, unatibiwa Hospitali Maalum, unapanda ndege Maalum, unaishi sehemu maalum, unatembelea gari maalum, unakalia kiti maalum, unafanya ziara maalum, nk.