Kurunzi
Platinum Member
- Jul 31, 2009
- 10,196
- 11,624
tunatakia uponyaji wa haraka.
NOte: kwenye red ?!
Umeona eh ni hotel maalumu au hospiatal maalumu? ukitaka kumsafisha mtu lazima uwe na uwelewa mzuri.
tunatakia uponyaji wa haraka.
NOte: kwenye red ?!
Wewe dr wa mifugo au wa nyuki kwanini unadhani ni kubwa.sio dogo hata chembe
Hotel maalum ndio inakuwaje hiyo?
Hapo kwenye red, ndipo pana walakini! Uangalizi wa mara kwa mara wa madaktari ambapo yupo chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote maana yake rais yupo ICU, period!Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.
Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.
Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.
Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2014
Mh. Rais ana uchungu na pesa za walipa kodi huyo angeongeza bajeti kuwa kubwa. Si unajua mambo ya mama zetu mara shopping pale mara akamsalimie fulani hapo pesa za wavuja jasho zinatumikaWaungwana,
Katika hizi picha zote za Kikwete akiwa hospitali USA sijaona hata picha moja inayomuonyesha mkewe Salma Kikwete, ni aje Wakuu? Hasa ukitilia maanani mara nyingi wanaambatana na Kikwete kwenye safari zake.
Mungu akulinde rais wetu mpendwa.
Hata mie nimeanza kushtuka aisee,mkuu wa Nchi anaweza kuwa anaumwa sana,isije ikawa mambo ya king cobra sasa!!!
Hivi huyu jamaa alimkaimisha nani wakati anaondokA?
Kwa hiyo huyu Profesa anataka sympathy ya wananchi baada ya kukwapua mabilioni ya pesa za walipa kodi? Huyu mtu kwa kweli tulichagua HASARA! Safari hii watanzania tumepatikana. Bill ya safari na matibabu yake wala hakuna atakayethubutu kuisema, labda ichakachuliwe!