Rais Kikwete kuhamishiwa Hoteli Maalum

Rais Kikwete kuhamishiwa Hoteli Maalum

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,028
Reaction score
2,732
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume
(prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.

Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao
nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.

Akiwa kwenye Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembele
wa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.

Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2014
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaendelea na matitabu yake nchini Marekani, leo, Jumatano, Novemba 12, 2014, anatarajiwa kutoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye Hoteli Maalum ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Rais Kikwete amekuwa kwenye Hospitali ya Johns Hopkins tokea Jumamosi iliyopita wakati alipofanyikwa upasuaji wa tezi dume
(prostrate) na afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea.

Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao
nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete baadaye leo atahamishwa kutoka wodini kwenda kwenye
Hospitali Maalum yenye uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko karibu na hospitali hiyo.

Akiwa kwenye
Hoteli Maalum hiyo, Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.

Wakati huo huo, kwa sababu ya wingi wa ujumbe mfupi wa simu (sms) ambazo amekuwa anazipokea Rais Kikwete, imeanzishwa namba maalum ya simu ambako wananchi wanaweza kuwasiliana kwa sms na Mhe. Rais. Namba hiyo ni +1-646-309-2295.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
12 Novemba, 2014

tunamtakia uponyaji wa haraka.

NOte: kwenye red utata?!
 
Sasa watu nae watakuJa kusema kwa nini apelekwe kwenye hotel maalum tunao elewa tumeelewa kwa nini.
 
OMG....!PAYE yangu nnayochangia inaendelea kuteseka nje ya nchi.
Pona haraka JK urejee magogoni.
 
Hii Kurugenzi huwa wananishanganza sana. Mara kwa mara wanafanya makosa ya kiuandishi.
 
Hii sio cancer lakini ? Maana yule dokta ni bingwa wa mambo hayo ? Na kama imeshamuenea mwilini na wamechelewa kuiwahi ndio tumuombee dua tena au keshakolimbiwa mtu hapa ,tunabaki kuchezeshwa gwaride tusilolijua ?
 
Yeye apone lakini imani ya wananchi haitarudishwa kwa tararira za ikulu. Na akirudi tutampokea kwa shamra shamra kubwa sana ,na hizi ni mbinu za viongozi wengi sana duniani ,kwenda ughaibuni na kisha kurudi kupokewa kwa shangwe ili kurudisha imani kwa chama tawala ,ila kwa chama hiki CCM hairudi imani ya mtu hapa !
 
Back
Top Bottom