Rais Kikwete jijini Kampala, akutana na Satta (leo)

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,415
kikwete-museveni2.jpg

Rais Jakaya Kikwete akimuwekea chaneli ya kupata lugha Rais Mwai Kibaki wa Kenya katika siku ya pili ya mkutano huo wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo Disemba 16, 2011

kikwete-museveni.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na Rais Yoweri Museveni wa Uganda huku Katibu Mtendaji wa Kamati ya Kimataifa ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) anayemaliza muda wake Balozi Liberata Mulamula akitega sikio katika siku ya pili ya mkutano huo wa viongozi wakuu wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo Disemba 16, 2011

kikwete-kampala.jpg

Rais Jakaya Kikwete akichangia mada katika siku ya pili ya mkutano huo wa ICGLR wa kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia hoteli ya Speke Commonwealth Resort kitongojini Munyonyo, Kampala, leo Disemba 16, 2011

kikwete-kmpl.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Rais Michael Satta wa Zambia na mkewe usiku wa kuamkia leo, Disemba 16, 2011
 
Satta's actions and manifesto plans are powerful na
aonekana kaja kikazi kweli kweli katika kiti cha Uraisi....
Hopefully he lives up the expectations of most.
 
Satta's actions and manifesto plans are powerful na
aonekana kaja kikazi kweli kweli katika kiti cha Uraisi....
Hopefully he lives up the expectations of most.
Satta aliomba Urais na sio Urahisi,
Sisi tuna Rahisi lakini hatuna Rais,
Nchi inaongozwa na Automatic Pilot.
 
Marais majirani na wenye mitazamo tofauti kabisa na malengo tofauti ya madaraka yao!!tafakari
 
Hivi bado bandari ya dar na TAzARA ni best option kwa zambia(Land locke country) kupitisha mizigo yao.

Au msumbuji na South africa kusaidiana na sisi wenyewe watanzania ndio tunamaliza influnce na opportuities kwa nchi zinazotuzunguka.
 
Satta aliomba Urais na sio Urahisi,
Sisi tuna Rahisi lakini hatuna Rais,
Nchi inaongozwa na Automatic Pilot.


Matola IMO saizi bado ni mapema mno kumpongeza...
Unakumbuka nguvu alokua amekuja nayo JK ile awamu
ya kwanza ya Uraisi wake?

My assumption ni kwamba ni maraisi mengi huwa
na malengo mazuri kwa wananchi, but once on the kiti
wanakuta system imesukwa in a way kuibadilisha inamuia
ngumu, kwamba being a president haimaanishi kua wewe
(raisi) ndio waendesha inchi... Kua kuna maraisi nyumba ya
raisi ambao ukienda tofauti na wao, inchi lazima ikushinde!
In the end anakua such a dissapointment for the
expectations put on him zilikua sky high.... I may however
be wrong... BUT that is my BELIEF on the matter.
 
hivi kwa nini hawakumwalika siku ya kuapishwa sata?
sata amekaa kikazi zaidi hakuna kutake chances
 
Uganda%281%29.jpg


Rais Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza na Rais wa Zambia na Mwenyekiti wa ICGLR aliyemaliza muda wake, Michael Chilufya Sata (kushoto) na Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.

Rais Jakaya Kikwete, aliondoka jana nchini kwenda Kampala, Uganda ambako ataungana na viongozi wenzake wa nchi za Maziwa Makuu kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Nchi za

Maziwa Makuu wa International Conference on the Great Lakes Region (ICGLR).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana ilisema mkutano huo wa siku mbili, miongoni mwa mambo mengine, utakuwa na kikao maalum cha kujadili Ukatili wa Kinjisia kama ilivyoamuliwa katika

mkutano wa mwaka jana uliofanyika Lusaka, Zambia. Ukatili huo ni moja ya changamoto kubwa zinazolikabili eneo la Maziwa Makuu.


Kikao hicho cha Kampala pia kitawapa nafasi wakuu hao wa nchi kujadili na kuangalia upya ripoti ya Mkutano wa Mawaziri wa Ulinzi na Usalama wa eneo la ICGLR kuhusiana na majeshi hasi yanayoendelea kusumbua na kuyumbisha eneo hilo la Maziwa Makuu.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa ICGLR, Balozi Liberata Mulamula, wakuu hao wa nchi pia watapata nafasi ya kujadili na kuamua kuhusu ombi la taifa jipya la Sudan Kusini kujiunga na ICGLR.


Aidha, Rais Kikwete na wakuu wenzake wa nchi wanachama wa ICGLR pia watapokea ripoti ya maendeleo ya utekelezaji kuhusu maamuzi yaliyofanyika katika kikao cha mwaka jana mjini Lusaka na hasa kuhusu jitihada

za nchi wanachama wa ICGLR kupambana na uvunaji na biashara haramu ya maliasili ya nchi wanachama.

Kikao cha Kampala pia kitateua Katibu Mtendaji mpya wa ICGLR kuchukua nafasi ya Balozi Mulamula wa

Tanzania ambaye aliongezewa muda wa mwaka mmoja katika kikao cha mwaka jana ili kutoa nafasi kwa nchi wanachama kuwasilisha majina ya wanaofaa kuwania nafasi hiyo.


Mpaka sasa wagombea watatu wamejitokeza kuwania nafasi hiyo ambao ni Profesa Lumu Alphonse Ntumba Luaba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Balozi Philip Richard Okanda Owade wa Kenya na Dk. Mohammed Abdleghaffar wa Sudan.





CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom