Rais Kikwete awapandisha vyeo makanali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
KWA UFUPI
"Napenda kuwakumbusha suala na nidhamu ni jambo muhimu kwani ndiyo kioo chetu katika jeshi hivyo nasisitiza kuendelea kuzingatia jambo hilo.

Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, amewapandisha vyeo maofisa 28 kutoka Kanali na kuwa Brigedia.


Huku Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba akiwataka maafisa hao kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza ufanisi wa Jeshi.

Hatua ya Rais Kikwete kuwapandisha vyeo maofisa hao imefanywa kwa mujibu wa kanuni za Majeshi ya Ulinzi inayompa mamlaka kufanya hivyo.

Wakati Rais Kikwete akiwapandisha vyeo maofisa hao, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Samweli Ndomba kwa niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amewataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuleta tija na maendeleo jeshi.

Pia mnadhimu huyo amewasisitizia maafisa hao kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwa sababu ndiyo msingi wa mafanikio katika utendaji wa jeshi.

"Napenda kuwakumbusha suala na nidhamu ni jambo muhimu kwani ndiyo kioo chetu katika jeshi hivyo nasisitiza kuendelea kuzingatia jambo hilo. Lingine ambalo ningependa tuendelea kulizingatia ni kufanya kazi kwa weledi," alisema.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na JWTZ, maofisa waliopandishwa vyeo ni pamoja na Kanali Denis Raphael Janga, Kanali Jason Nestor Musikula, Kanali Jackson King Mrema, Kanali Martin Amos Kemwaga, Kanali Joseph Cosmas Chengelela, Kanali Martin Nikubuka Mwankanye, Kanali Harold Kidundi Mziray, Kanali Emmanuel Peter Kapesa na Kanali Mwita Wambura Isamulyo.

Wengine ni Kanali Francis Asilia Njau, Kanali Pendo Uledi Kamungwele, Kanali Moses Adolph Shinyambala, Kanali Ibrahim Abdarahamani Kimario, Kanali Michael Garo Luwongo, Kanali Nelson Hosea Msanja,Kanali Blasius Kalima Masanja, Kanali Aloyce Damian Mwanjile, Kanali Rajabu Goma Hanti na Kanali Ignas Beatus Mubofu.

Pia wamo Kanali Dominic Basil Mrope, Kanali Hamis Issa Majumba, Kanali Salehe Omari Semtaua, Kanali Henry Sweko Kamundo, Kanali Sylivester Msafiri Minja, Kanali John Bangantagoka Bishoge, Kanali Anselm Shigongo Bahati, Kanali Robinson Mboli Mwanjela na Kanali Kaisy Philip Njelekela.

Source: Mwananchi
 
Mh. Capt. Komba na uchangiaji wotekatika katiba mpya hayumo?
 
Mkuu, kwani kama ana sifa hawezi kumpandisha cheo eti kwa vile ni mpambe wake?

Hata wewe umesema "kama ana sifa", sasa wewe unadhani huyo Kimario ana sifa gani ya ziada zaidi ya huo upambe wake kwa M.k.w.e.r.e? Hebu zitaje basi kama wewe unazijua!
 
Hata kwenye majeshi hawamo,inatisha,inabidi wazingatie mawaidha ya Mufti kuwa wasiitupe elimu dunia na kuangalia upande mmoja,watabaki kulalamika kila siku.
 
Nikitumia slogan ya book 7, mbona wengi wao ni wa Kaskazini, ina maana Mkuu wa Majeshi naye ni CDM?

Tiba
 
Kwani Capt Komba ni Kanali?
Kwenye siasa za Tanzania amemzidi hata huyo Kanali. Maana sasa ni raia, hivyo makanali wanampigia saluti sasa labda akirudi kwenye uniform ndiyo atawakaukia hao makanali.
 
Hata wewe umesema "kama ana sifa", sasa wewe unadhani huyo Kimario ana sifa gani ya ziada zaidi ya huo upambe wake kwa M.k.w.e.r.e? Hebu zitaje basi kama wewe unazijua!

Hivi mnadharau ADC kwa kuwa Ana Beba bag ...huyoo Ana kazi kubwa Sana ....anamwandalia Rais mambo mengi ..na ni Mkuu wa motorcade popote Rais alipo...na mengine mengi....anatumika pia kuangalia Usalama wake akishirikiana na maafisa wa Usalama .....kuacha hayo anatakiwa kuwa na Elimu ya field na utambuzi ...yaani uwezo wa kusoma mazingira haraka...na kuamua...hayo yote hayapatikani..bila mafunzo STAHIKI ......kimsingi cheo chake Huwa kanali...na pale ni Kama anatongoza kikosi Kizima...kwa kazi zake......
huwezi kupewa cheo bila kufanya mafunzo jeshini.....KIMSINGI KAMA UTARATIBU UTAFUATWA ..ATAKOMA KUWA ADC....Kwani kwa cheo cha Brigedia Sasa AdC ni jukumu dogo kwake atahitaji kupewa more roles jeshini....NI WAZI KARIBUNI RAIS ATAANZA KUONEKANA NA ADC MPYA.....HUYO ATARUDISHWA KAMBINI......
ADC WA RAIS MKAPA ( brig gen simuli )ALIPANDISHWA CHEO BAADA YA RAIS MKAPA KUMALIZA TU ...NAYE AMERUDI KAMBINI...
 
Hongereni makanda. lakini mbona makamanda kama kina Sukambi Mahela, au kina Msindai, Mfikirwa, Msingiri, Mwaya, Masalamado n.k- walioshughulika kule Comoro hawamo? Amiri Jeshi tafadhali wakumbuke!!
 
Nikitumia slogan ya book 7, mbona wengi wao ni wa Kaskazini, ina maana Mkuu wa Majeshi naye ni CDM?

Tiba

Mimi nashangaa,Lumumba hapa hawatasema kitu tena na ile chuki yao ya udini wameisahau
 
Hongereni makanda. lakini mbona makamanda kama kina Sukambi Mahela, au kina Msindai, Mfikirwa, Msingiri, Mwaya, Masalamado n.k- walioshughulika kule Comoro hawamo? Amiri Jeshi tafadhali wakumbuke!!

Hupandishwi cheo tu kwavile ulikuwa vitani ; nilazima pia uoneshe weledi wa kijeshi. Hao jamaa zako mliokuwa wote Comoro wao bado wana rank za chini na bahati yao mbaya Shimbo aliyekula mshiko wa Comoro yuko China!!!
 
Kwenye siasa za Tanzania amemzidi hata huyo Kanali. Maana sasa ni raia, hivyo makanali wanampigia saluti sasa labda akirudi kwenye uniform ndiyo atawakaukia hao makanali.

Hii inathibitisha hukupitia JKT no way afisa wa jeshi akampigia sluti raia wa kisiasa kuna exception kadha lakini si kwa wa aina ya huyo mchumia tumbo.
 
Back
Top Bottom