"Rais Kagame na mamilioni ya wananchi wa Rwanda wa kabila la Watutsi na Wahutu wachache wenye msimamo wa wastani, ni waathirika wakubwa wa ukatili na unyama uliofanywa na FDLR, na bila shaka hawajasahau wala kusamehe.
Rais Kikwete alipaswa kuzingatia ukweli huu kabla ya kuamua kutoa ushauri wake. Kama angezingatia ukweli huu kabla, bila shaka asingethubutu kumshauri Rais Kagame kukaa meza moja na kundi ambalo halijawahi kuomba msamaha kwa Wanyarwanda wala kuonyesha kujutia uovu wao.
Halafu Rais Kikwete alikosea kutoa ushauri huo mbele ya mkutano ule. Hapakuwa mahali sahihi kwa jambo zito kama hilo. Angetafuta nafasi nyingine, na kwa maoni yangu angezungumza na marais wenzake kwa faragha, ama wote kwa pamoja au mmoja mmoja.
Angepata nafasi nzuri zaidi ya kufafanua dhamira ya ushauri wake, na pia angeweza kuona mwitikio wa Rais Kagame juu ya ushauri huo. Ninaamini msuguano wa sasa usingekuwepo kwa sababu wangejadiliana kwa kina na kuyamaliza mambo yote katika chumba kilichofungwa milango.
Sasa ushauri unataka kuzaa vita ya majirani wawili wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Bila shaka madhara yake ni makubwa. Mbali na kusababisha kuharibika kwa mahusiano kati ya nchi hizi, pia zitapoteza maisha ya watu wake na rasilimali, na hivyo kuteteresha uchumi wa kila moja.
Ni imani yangu Watanzania wengi hawataki na hawawezi kuunga mkono uamuzi wa kuingia vitani na Rwanda. Watanzania hawapo tayari kwa vita vingine, baada ya vile vya Uganda vya mwaka 1978. Tunataka kujenga nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii kukimbizana na wakati kwa sababu tupo nyuma sana.
Namshauri Rais Kikwete awaombe radhi Wanyarwanda, amuombe radhi Rais Kagame. Ampigie simu amwambie yaishe kwa kuwa hakukusudia kumuudhi wala kumkumbusha machungu ya unyama wa Interahamwe, amwalike Dar es Salaam wanywe chai na mnyinyo."
!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Bw. Easyjet a.k.a Maziku,
Ushauri wako kwa Raisi Kikwete tumeusoma. Lakini ni ushauri tu ! Lakini kabla haujazingatiwa ingekuwa vizuri utusaidie kuweka mambo kadhaa muhimu wazi:
1. RPF chini ya Kagame walivyodungua ndege ya kiraia iliyokuwa imebeba maRais wa nchi huru mbili( hivi sasa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki) wakitokea Tanzania kuzungumzia amani na Rais Mwinyi -Rais Habyalimana wa Rwanda na Rais Ntaryamira wa Burundi, wafanyakazi wa ndege hiyo na kusababisha vifo vyao hudhani kwamba raia wa nchi hizo na Afrika kwa ujumla tulistahili kuombwa msamaha ?. Au magaidi hawaombi msamaha ?
2. Majeshi ya Rwanda hadi sana yamesababisha vifo na mateso makubwa nchini Congo, weka pembeni uporaji wa rasilimali na uharibifu wa maliasili-Lini waliwahi kuwaomba Wakongo msamaha? Idadi ya vifo vya Wakongo kutokana na vita ambavyo wapiganaji wakuu ni vikosi aidha vya serikali ya Rwanda, makundi ya waasi wa Rwanda na Uganda vimekadiriwa kufikia milioni tatu. Easy jet ungemshauri kwanza Kagame kuwaomba Wakongo radhi kabla ya kufikiria viginevyo.
3. Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikisikia baadhi ya Great Thinkers wakihusisha kifo cha Prof Jwani Mwaikusa na Kigali. Huenda siku moja Rais Kagame ataulizwa kuhuzu jambo hili. Lakini kwa familia ya Prof Mwaikusa, Watanzania na hata Mungu wake angeomba msamaha.
4. Zaidi ya hapo, EasyJet ungemshauri Raisi Kagame kuendelea kuishukuru Tanzania, kama jirani mwema kwa kuwapa hifadhi Wanyarwanda kuepuka mauaji na vurugu kila inapobidi. Hakika hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi husababisha athari za kiuchumi, kimazingira, kijamii , kiusalama na kisiasa.
5. Ukiangalia yote hayo hapo juu na kuwalinganisha Raisi Kikwete na Raisi Kagame, Rais Kikwete may be a 'Saint'. Kagame je ? Hili nawaachia Wakongo, Warundi, Watanzania, wanajamvi na Waganda mahali ambapo Kagame alipigana vita vya msituni Luwero Triangle, na kuacha marundo ya mafuvu, na baadaye kutumika kama Mkuu wa idara ya ujasusi jeshini.
Nchi kadhaa ikiwemo Marekani wameanza kujifunza kutomhandle Kagame using a kid's gloves. Wengine wameanza kupunguza misaada ili ajirekebishe na kutoa uhuru zaidi wa kidemokrasia katika nchi yake, pamoja na kuacha uvamizi wa nchi za watu bila kuzingatia sheria za kimataifa.
Wakuu naamini kwa yote hayo Riasi Kikwete hana sababu ya kuomba radhi ila kutompuuza huyu jirani kutokana na historia yake.